Njia bora ya kuanza kujifunza kazi na kuingiza kipato ukiwa Chuoni, Michongo Affiliate
Kwenye nchi nyingi, wanafunzi wa chuo ni moja kati ya makundi yaliyo active katika kufanya kazi, na mapinduzi mengi ya uchumi hutegemea kundi hili, kwani wana nguvu na uwezo mpana. Kazi nyingi za vipindi (part time) huwa zinafanywa na kundi hili. Hii siyo tu inawasaidia kuongeza kipato, bali inawafanya wawe na ubongo ulio active haswa kwenye sehemu ya pili ya maisha, maisha halisi.
Kinyume na hiki, tunakuwa tunatengeneza kundi kubwa la vijana wasomi lakini wanakuwa wamedumaa kwenye kujishugulisha. Na, ni moja ya sababu bumu linapochelewa, inakuwa shida kubwa na maandamano yasiyoisha.
Hali hii, huwa inaathiri sana sekta binafsi pale unapomuajiri mwanachuo moja kwa moja kutoka chuoni, kwani kunakuwa na kazi mbili kwa pamoja, kumbabidili kutoka mwanafunzi kuwa mfanyakazi (huku ukipambana na uhalisia vs ndoto) and kumfundisha kazi kitu ambacho kwenye Uchumi wa viwanda italeta shida, na ni moja ya sababu waajiri wengi hukimbilia kuajiri raia wa kigeni kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.
Kuna sababu nyingi kwenye hili na kila upande anaongea lake, Upande wa wanachuo wanasema, Wakufunzi wanabana sana hivyo unashindwa hata muda wa kusoma, na upande wa wakufunzi wanajitete kuwa wanafunzi ni goigoi wanapenda mambo rahisi hivyo hawajishugulishi kutwa kuchinda kwenye mitandao jamii, ukiwaachia huru utavuna mabua.
