Matumizi ya email za kampuni (Corporate Business Email Address) ni moja ya njia rahisi kabisa ya kutangaza biashara yako kwa wateja. Mfano, miaka sita iliyopita nilinunua mashine ya kutotolesha vifaranga kutoka China na mawasiliano mengi tulifanya kwa kutumia email. Juzi mmoja wa watu wangu wa karibu alitaka kununua machine, alitumiwa quotation nyingi tu, aliponionesha,kulikuwa na emails 13. Kati ya hizo, 3 zilikuwa zenye domain za kampuni 2 Yahoo 5 Gamil 3 QQ. Kupitia email hizo,niiliweza kubaini moja wapo ya hizi email zilizotumia domain za kampuni (Corporate Business Email Address) ni wale walionuzia mashine ambayo inatumika hadi leo. Hivyo, ilikuwa rahisi kwangu kuwabaini na kupelekea kumshauri afanye nao kazi.

 Kitu ambacho nilikuwa ninajiuliza sana, inawezekana vipi mtu akatuma taarifa za kampuni kwa kutumia email za gmail? Utamuhakikishia vipi mteja kama anadili na kampuni na si mtu binafsi (mfanyakazi wa ndani ya kampuni aliyeamua kuifanya hiyo kazi mwenyewe)?

 Matumizi ya emails za bure siyo tu yanakuondolea uthamani (Value), bali kunaweza kukukimbizia wateja wengi. Pia, kumbuka kuwa, si lazima uwe na website ili uwe na email ya kampuni. Unachotakiwa ni kuwa na jina la website na ukanunua bando la email. Dudumizi tunayo huduma ya email kwa kampuni (Business Emails).Huduma hizi zote zinapatikana kwenye website yetu ya Hosting https://Duhosting.co.tz

Faida za kutumia email ya kampuni

Uaminifu: Siku zote wateja hupenda kufanya biashara na watu wanao waamiini. Kwa kutumia emails za kampuni kutakusaidia kujenga uaminifu kwa wateja na kuondoa maswali maswali.

Inakufanya uwe kikazi zaidi: Wazo la haraka ambalo huwajia watu pindi wanapopokea email yako toka gmail au Yahoo ni kuwa, huyu hayupo makini na kazi yake. Hata email hana bado anatumia Gmail kikazi. Hivyo epuka kupoteza thamani na kuonekana haupo makini.

Inaongeza upatikanaji wako online: Email za kampuni hubeba jina la kampuni, kwa mfano, sisi tunatumia This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., hii inamaanisha mtu akienda dudumizi.com ataonana na website yetu.

Hata kama hauna Website, unaweza kuweka kurasa ya matengenezo ya website (Under Construction page) na taarifa kadhaa zinazotoa ujumbe wa biashara yako, mfano unaweza kutembelea http://striderengineering.co.tz na kujionea kurasa ya matengenezo yenye taarifa muhimu na nini wanafanya, ni mmoja wa wateja wetu wa Business Email.

Msaada wa haraka: Kwa kutumia email za kampuni, inakuwezesha kupata msaada wa haraka pale unapokutana na tatizo lolote, mfano kuvamiwa na hackers nk kwakuwa unakuwa umejiunga na huduma ya malipo toka kwa kamouni husika.

 

Jinsi ya kupata Emails za kampuni:

Ili uweze kupata email ya kampuni, unatakiwa upate jina la website (domain name) na kifurushi cha email. Unaweza kupata kwa kutafuta Makampuni yanayotoa huduma hii (Website Hosting Companies)  ambapo Dudumizi ni mmojawapo. Gharama na huduma zinategemeana na kampuni. Kwa mfano, Dudumizi inatoa huduma hii kwa gharama nafuu Zaidi ikijumuisha kurasa ya matengenezo bure.

Hivyo, hauna sababu ya kuendelea kupoteza uthamani na wateja kwa kuendelea kutumia Gmail na Yahoo kwa mawasiliano ya kibiashara. Ni wakati wa kumiliki email ya kampuni leo na kuitumia.

 

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now