Jinsi ya kufikisha uthamani wa huduma (How to deliver service value)
Tangu kuanza kuchanganya kwa maendeleo ya Teknolojia Tanzania, tumeona makampuni mengi yakizaliwa siku hadi siku, kila moja likiwa na lundo la huduma wanazotoa kwa wateja wao. Iwe kwa yale ya simu, yale ya kibenki, yale ya kutengeneza programu na hata yale ya kuuza majina ya website (Domain names), wote hawa wamejikitia kuhakikisha mteja anapata anachokitaka.
Kitu ambacho mengi ya makampuni haya yemeshindwa kufahamu ni kuwa, je huyu mteja ANATAKA NINI? mteja hanunui huduma ama bidhaa kama bidhaa, bali ni faida/thamani (Value) inayokuja na ile huduma au bidhaa. Chukulia mfano, wewe ni Bank na unatoa huduma ya kibenki kwa mtandao (Online banking), mteja anayeamua kutumia huduma hii ya kibenki toka kwako, siyo kwa sababu anataka kuwa na akaunti ya bank au kutuma pesa tu, bali nini kinakuja na hii huduma.

