Zijue faida za domain ya .co.tz badala ya .com
Ni mara ngapi umekuwa ukiumiza sana kichwa kwa sababu majina yote ya .com yanayoendana na jina halisi la biashara yako tayari yameshachukuliwa? mfano, wewe kampuni yako inaitwa Dudumizi, na kila ukitafuta dudumizi.com , Dudumizi.net na hata Dudumizi.info unakuta tayari yameshachukuliwa, hakuna sababu ya kuchanganyikiwa, tunayo .co.tz, majina ya kitanzania zaidi.
Watu wengi wamekuwa wakipendelea kutumia majina ya .com. Wengi wamekuwa na imani kuwa kwa kutumia majina ya .com kinawafanya waonekana kimataifa na kitaalamu zaidi, ingawa hili lina ukweli wake kiasi fulani, ila kwa upande mwingine, inategemeana sana na aina ya biashara unayoifanya na mlengwa mkuu wa biashara husika, majina ya .co.tz nayo yana faida tele kwa baadhi ya mazingira.



