Dudumizi sasa yaanza kutoa huduma kwa lugha ya Kichina
Uhusiano kati ya Tanzania ni moja kati ya mahusiano ya muda mrefu, mahusiano haya yameanza tangu enzi za Baba wa Taifa na wakati huo wachina hawakuwa na nguvu au uwezo mkubwa kama walivyo sasa. Mahusiano haya yamedumu kwa miongo bila kutetereka. Na kwa wachina huwa wanatuita, marafiki wazuri (好朋友). Tumekuwa tukishirikiana na China kiuchumi, kijamii, kiulinzi na kadha wakadha.
Katika miaka ya karibuni, nchi ya China imekuwa ikiendelea kwa kasi na hatimaye hata kuwa nchi ya pili kwa uchumi duniani. Ukuaji huu wa Uchumi umepelekea China kujitanua zaidi kibiashara. Leo hii, bidhaa nyingi muhimu ama zinatoka China ama zimetengenezwa China. Pia, makampuni mengi ya kichina yamekuwa yakimiminika Tanzania kutafuta nafasi za kibiashara.
