Wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na sekondari, wana mchango mkubwa sana katika ukuaji wa sekta ya kenolojia ya habari. Moja ya changamoto wanayokutana nayo ni kazi zao kutoweza kuonekana au kutumika kwa uma. Hivyo, siku ya mwisho huishia kuwa historia na jamii kutonufaika na kazi hizo ambazo kama zingepata nafasi ya kutumia, zingeweza kuboreshwa na kuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa letu.
Moja ya sababu inayowafanya wanafunzi wengi washindwe kupandisha kazi zao online ni kushindwa kumudu gharama za hosting. Katika kulitatua hili kivitendo, Dudumizi kupitia Duhosting, tunakuletea kifurushi mahususi kwa ajili ya wanafunzi (Mwanachuo Plan), kifurushi hiki rasmi kwa ajili ya kufanya hosting kwa kazi ambazo zimetengenezwa na wanafunzi wenyewe, iwe ni final year year project, iwe ni kwa ajiili ya kujifunzia.
Kwa gharama za kawaida, mwanachuo utaweza kununua kifurushi cha 1GB, email, .tz domain na Unlimited bandwith kwa 50,000Tsh tu. Habari njema ni kuwa, kifurushi hiki huweza kupatika hadi bure kabisa pindi ukitupatia ushahidi kuwa hauna uwezo wa kulipia na pia kazi yako ni nzuri na ina manufaa kwa jamii. Hivyo tuandikia kwenda This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ukifafanua project yako unayofanya, ila hauna uwezo wa kulipia hosting, nasi baada ya kuipitia tutakuwezesha.