Katika ulimwengu wa mtandao, biashara nyingi sana zimekuwa zikitegemea mitandao ya utafutaji (search engine) katika kuwafikishia watu taarifa au bidhaa zao. Tumekuwa tukisikia maswali mengi kama, nimekugoogle ila sijakuona, mbona haupatikani google, nk. Watu wengi sana wamekuwa wakitumia Google wakimaanisha search engines na kinyume chake. Lakini, tunapoongelea search engine, tunamaanisha mtandao yote kama Google, Bing, Baidu, yahoo nk, ingawa Google ndiyo inayoongoza kwakuwa na watumiaji na taarifa nyingi.
Kwakuwa search engine ni moja ya sehemu muhimu katika maisha ya biashara, hivyo ni kitu muhimu sana kuelewa jinsi inavyofanya kazi au ni njia gani inatumia kupanga website za kuzionesha kwanza. Na hii ni moja ya changamoto kwa watu wengi.
Katika makala hii, tutakufafanulia jinsi Search Engine inavyofanya kazi, tutajikita kwenye muundo na wala si moja moja.
Kwanini tuna search engine?
Lengo kuu la search engine ni kuhakikisha linakupatia taarifa unayoitafuta tena yenye uhakika. Aliwahi nukuliwa meneja wa Google akisema, "Tunapokuonesha Dudumizi kama namba moja katika matokeo ya utafutaji kwenye huduma ya Website, App, Domain name registration na Web Hosting kwa Tanzania, tunataka kuhakikisha ya kuwa, unapoenda Dudumizi kwenye ofisi zao, hautojuta. Hii inamaana, Google wanataka kufanya kazi kama binadamu.
Kwa kuwapa taarifa sahihi na zenye kuaminika, ina maana watembeleaji wataongezeka na taarifa zitakuwa nyingi zaidi na zaidi. Na hii ndiyo moja ya sababu Google inatumiwa na watu wengi kila siku. Pia, kwa kupata watembeleaji wengi, ina maana hii mitandao ya utafutaji itatengeneza faida kupitia matangazo tunayoyaona wakati tunatembelea au kutafuta kurasa mbalimbali.
Hivyo, ili watu waendelee kutembelea, ni lazima search engine zihakikishe zinaboresha huduma zake na kuwa za uhakika. Hii ndiyo sababu, kanuni za ukokotoaji wa upangaji wa matokeo ya utafutaji (search results) ni siri kubwa ya Google. Ingawa wametoa madokezo na vitu vya kuzingatia kama unataka kutokea kurasa za mbele.
Vielelezo vya taarifa (Search Engine Index)
Ili search engine itimize jukumu lake la kukupatia taarifa iliyo bora karibu na uhalisia, inatakiwa iwe na taarifa nyingi kama siyo zote zilizo online na baada ya hapo itafanya ulinganishi kulingana na kanuni zake ili kubaini nani wa kumuonesha kwanza.
Baada ya kuwa na taarifa za kutosha kutoka kila website iliyo online, mitandao hii hutengeneza uhusiano kati ya keywords na taarifa ilizonazo kutoka kila kurasa ya website.
Siyo hivyo tuu, pia, search engine inatakiwa kupanga hizi kurasa kulingana na ubora wa taarifa wake (page rankings). Upangaji huu hutegemeana na kanuni za search engine na si za kibinadamu. Kitendo hiki cha kukusanya vielelezo vinavyohusiana na Website ndiyo huitwa utengenezaji wa vielezo vya Website (website index)
Ukusanyaji na utambuzi wa taarifa (Website Crawlers)
Ili search engine ziweze kutengeneza vielezo vya kurasa za website, inatakiwa lazima izitembelee, izisome na hata kuhifadhi taarifa muhimu inazoona inazihitaji.
Hivyo, mitandao hii hufanya ukusanyaji huu mara kwa mara ili kutambua kurasa mpya, zilizoboreshwa na hata zile zilizofutwa. Matokeo ya ukusanyaji ni utengenezaji wa vielezo (Index). Na ndiyo sababu, kuwa na Website Hosting nzuri, ni moja ya vitu muhimu kama unataka kutokea kurasa za mbele za Google kwakuwa, kama mitandao hii itashindwa kutembelea website yako kwakuwa haipatikani, basi haitokuwa na taarifa zako,na wala haitoweza kutengeneza vielezo (index), hivyo wakati watu wanatafuta huduma kulingana na keywords zao, website yako haitotokea au itatokea mbali sana kwakuwa search engine haina taarifa za kutosha kukulinganisha na wengine.
Unaweza kuharakisha ukusanyaji wa taarifa za Website yako kwa kutuma sitemap.
Kanuni za ukokotoaji (Search Engine Algorithms)
Hii ni moja ya sehemu muhimu kwa search engine, mfano, search engine imetafuta na kuzitambua website elfu moja zinazohusika na uuzaji wa nguo za akina dada, sasa inafanyaje ili kuzipanga kulingana na ubora?
Ili kutatua changamoto hii na hatimaye kuwa na matokeo yaliyo bora kwa watafutaji, mitandao yote ya utafutaji, wametengeneza kanuni (algorithms) zinazokokotoa na kupanga website zote kulingana na taarifa ilizokusanya.
Vitu gani huzingatiwa kwenye upangaji wa ubora? (Ranking factors)
Kuna vitu ningi sana huzingatiwa katika upangaji wa matokeo ya utafutaji na nani atokee wa kwanza na nani wa mwisho, kwani kuna wakati website huwa zinafanana na pia kuna baadhi ya vitu vinachangia kiwango kikubwa ya vingine na uzito wake kwenye kanuni ya ukokotoaji si sawa.
Orodha yetu hii mpangilio wake haina uhusiano na search engine, hivyo tulichokiweka namba moja haimaanishi ni bora zaidi. Kipi kinabeba uzito gani, hii imekuwa siri kubwa ya ndani ya mitandao hii.
1. Umri wa Website
Jinsi Webite inavyokuwa na umri zaidi ina maana inaaminika (truthworthy) na kutegemewa zaidi ya zile mpya. Lakini haina maana, website ikiwa mpya basi haiwezi kutokea mbele ya ya kwanza. Kuna vitu vingi huwa vinazingatiwa.
2. Linki
Linki ni moja ya vitu muhimu na vyenye uzito mkubwa katika upangaji wa website, na linki zinazopendwa sana na mitandao hii ni zile za nje, mfano, ndani ya Website ya Dudumizi.com tukaweka linki ya duhosting.co.tz au tanzmed.co.tz. Endapo website yako imewekwa kwenye website nyingine nyingi, hii inamaanisha unaaminika na kutegemewa zaidi, hivyo unapata daraja kubwa zaidi kwenye matokeo ya utafutaji.
Ingawa linki ni kitu kizuri, lakini pia,inabidi ziwe linki bora. Linki bora ni zile zilizo katika website zenye watembeleaji wengi au nazo zina rank ya juu. Mfano, kwakuwa Dudumizi.com inatokea namba moja kwa Google, hii inamaana Google wanaiamini Dudumizi, hivyo website yoyote ambayo kutakuwa na linki yake Dudumizi inamaana nayo inapewa thamani kwakuwa wanaamini Dudumizi.com.
3. Keywords
Lengo kubwa la search engine ni kukupa matokeo ya utafutaji kulingana na keywords ulizoingiza, mfano, unapotafuta Website Hosting Companies in Dar es Salaam, utaona kuna keywords kama Hosting, website, dar es Salaam. Hivyo mitandao hii, inatakiwa iende kwenye vielelezo vyake vyenye keywords hizi na kuleta orodha ya website zote zenye uhusiano na vielelezo hivi halafu kuvionesha kulingana na ubora wa website kama ilivyokokotolewa kulingana na kanuni.
Kwa siku za karibuni, kumekuwa na mabadiliko mengi, hivyo, keywords hizi zinatakiwa zitoke kwenye contents za website na siyo kuziweza kwenye tag kama ilivyokuwa zamani. Hivyo, kama unataka kupata nafasi za juu, hakikisha unaandika contens za huduma yako yenye keywords zinazoendana nazo.
4. Muonekano rafiki wa simu
Google wamekuwa mstari wa mbele sana kuwafanya watengenezaji wa website zenye kuonekana vyema kwenye vifaa vyote zaidi ya komputa pekee (mobile usability). Hivyo, kama website yako inaonekana vizuri kwenye kompyuta lakini ukija kwenye simu haionekani vyema, basi utakuwa unapoteza alama muhimu.
5. Spidi ya Website
Ni kweli, Google hupendelea website zinazofunguka haraka, hivyo hakikisha website yako umeihost vyema na ipo fast.
6. Ubora na uhalisia wa taarifa
Google huwa wanafuatilia mtumia aliyetembelea website yako baada ya kukutafuta. Kama mteja atatembelea website yako na haraka anaboyeza kurudi tena Google kuja kutafuta tena, ina maana hakupata alichokitaka, hivyo hakikisha unapangilia vyema website yako na kumuwezesha mtu kupata alichokitaka kwa jicho la kwanza.
Search Engine Optimization
Kuna vitu vingi sana vimefichwa juu ya ukokotoaji wa matokeo ya upangaji wa Website. Lakini, kuna taarifa nyingi kama tulivyozianisha hapo juu ambazo zinaweza kutumiwa vyema na zikaleta matokeo chanya.
Dudumizi tunatoa mafunzo pamoja na huduma ya SEO & Maintenance kukusaidia unatokea kurasa za awali kwenye utafutaji, hivyo kama utahitaji huduma hii wasiliana nasi hapa