Hatua 5 za kupitia ili kumiliki website

 

2. Andaa vitu unavyotaka au website unazozipenda

Website ni sehemu ya kampuni, mara nyingi watu huanzisha kampuni baada ya kuwa na wazo fulani, wazo hili ama linaweza kuwa limetoka kwao moja kwa moja ama ni baada ya kuangalia toka kwa wengine. Hivyo, katika hatua hii, andaa vitu unavyotaka viwemo kwenye website yako pia na orodha ya websites ambazo unapenda vitu fulanifulani toka huko.

Kwa kampuni ya kawaida, unahitaji vitu kama kuhusu sisi, huduma tunazotoa, wasiliana nasi pia fomu ya mawasiliano ambapo mtu anaweza kukutumia maombi ya huduma moja kwa moja online.

3 Tengeneza Website

Katika hatua hii, ambayo nayo ina viji hatua kibao ndani yake, utatengeneza website, ama kwa kutumia timu yako au kwa kuajiri kampuni nyingine. Siku hizi Tanzania kuna makampuni mengi sana yanayojihusisha na utengenezaji wa website, unaweza kugoogle na kuyapata. Dudumizi.com ni chaguo murua kabisa juu ya hili.

Pia, unaweza kutumia programu nyingi za bure zinazopatikana online kutengeneza website kama Wix.com. Kitu cha muhimu kwenye hili, hakikisha unatengenezewa Website yenye kukuwezesha kubadili na kuichunga website bila kuwa na utaalamu wowote. Siku hizi kuna programu (CMS) nyingi kama Joomla, Wordpress, Drupal nk ambazo zitakusaidia kwenye hili. Bajeti ya website ya kawaida hucheza laki tatu hadi milioni moja kulingana na ukubwa wa kampuni itakayokutengenezea na aina ya Website unayotaka na pia nini kitakuwemo (features). Kumbuka, sio kila king'aracho ni dhahabu, kuna kamampuni mengi yanayosema watakutengenezea website kwa gharama ya chini, ila siku ya mwisho unajikuta unaishia kujuta.

Kama utaamua kuajiri kampuni, hakikisha umepitia kazi zao walizofanya na kuridhika na ubora wa kazi zao. Pia kama utaweza hakikisha unawasiliana na wateja wao kujua ubora wa huduma zao baada ya kazi kuisha. Kwenye hili, kitu cha muhimu kuzingatia pia, ni juu ya uchungaji na uboreshaji wa website, kwani kuna kipindi website italeta matatizo, je nani ni muhusika? (website Maintenance Service)

Kama wewe ni mmiliki wa biashara ndogo, hakuna haja ya kuajiri mtu wa IT kwa ajili ya hili, hivyo unaweza kuwapa jukumu hili watengenezaji wa website wakusaidie kuichunga website yako na wewe ukaendelea na mambo mengine ya biashara. Ila, kumbuka kutaka taarifa za maendeleo ya website yako (web analytics).

4.Chagua jina bora la website

Hii ni moja ya sehemu inayowachanganya wengi mno, wengi wamekuwa wakichanganya na kudhani kwamba jina la website ni lazima liendani na jina la kampuni.Hii siyo lazima, jina la website linaweza kuwa tofauti kabisa na lile la kampuni, ingawa kama litakuwa sawa bila kuleta mkanganyiko ni bora zaidi.Ukweli ni kwamba, majina mazuri mengi tayari yameshachukuliwa, hivyo kuna wakati kama nataka jina la website liendane na la kampuni yako, basi itakuwia ugumu na kukulazimisha kuongeza majina ya ziada ili kulifanya liwe la kipekee.

Jina la website ni roho ya website, kwani ni jina ambalo litasambaa kwenye mitandao na watu wote kulifahamu. Hakikisha jina lako lipo la kipekee, epuka kutumia majina ya website ambayo yana maneno mengi, yenye kuchanganya lugha mbili tofauti, yenye maneno yanayofanana; mfano to, two, 2, II nk. Jina la website lazima liwe linalotamkika kwenye simu na pia lisilo na miambatano mingi. Chukulia mfano, Dudumizi.com, linatamkika kiurahisi karibu toka kwa watu wa sehemu zote Duniani.

Mambo mengine ya kuzingatia hapa ni kuepuka kununua jina la Website toka kwa makampuni ya uchochoroni, kwani jina lako ni ruru yako kama hii kampuni itakufa katikati ya safari basi unajiweka kwenye hatihati. Pia, hakikisha jina linasajiliwa kwa kutumia taarifa zako na si za kampuni iliyokusajilia.

Mwisho kabisa, msisitizo ni kuwa, jina la Website siyo lazima liwe jina la kampuni, mfano jina la kampuni yetu ni Dudumizi Technologies, ila tunatumia jina la Dudumizi kwenye website kwani tungetumia Dudumizitechnologies.com lingechanganya watu kwakuwa ni refu na limechanganya lugha mbili hivyo kuleta utata kutamkika, pia kuna watu wangeliita Dudumizitechnology.com nk.

Gharama za kununua jina la Website ni shilingi elfu 20 kwa .com, .net elfu 24 kwa .org wakati ile ya .co.tz inaanzia shilingi elfu 25.

5. Chagua wapi pa kuweka Website (Hosting)

Baada ya kuchagua jina, na kununua, ingawa wengi hupenda kufanya hatua ya nne na ya tatu pamoja, kinachofuata ni kuchagua mahala ambapo website yako itakaa (Hosting).Siku hizi , gharama za kuhost website zimeshuka sana, kulingana na Dudumizi Hosting gharama ya kuhost website haizidi elfu 60 kwa website ya kawaida, hii ikijumuisha email ya kampuni.

Kwenye kuchagua wapi pa kuweka website yako, kama ilivyo kwenye jina, hakikisha unachagua kampuni inayoeleweka. Hakikisha umetembelea website yao na kuona baadhi ya website zinazohostiwa huko. Tembelea hizi website kabla ya kuamua. Mambo ya kuzingatia hapa ni kama;

-Muda ambao website itakuwa online bila kupata tatizo (Reliability); Ukweli ni kuwa, haiwezekani mitambi ikaka mwaka mzima bila kuleta hitilafu hata siku moja, hivyo hakikisha hizi hitilafu sio nyingi,

-Muda wanaotumia kutatua hitilafu (Maintainability); hakikisha, wanatatua tatizo haraka iwezekanavyo kunapotokea hitilafu na huduma kurudi kwenye mstari.

Vitu hivi, unaweza kuvipata kwa kuwasiliana na wamiliki wa website zilizohostiwa kwao au kwenye mkataba wa makubaliana ya huduma (SLA).


Hadi hapo utakuwa tayari una website inayofanya kazi, na sasa unaweza kuiweka kwenye kadi na matangazo ya biashara yako na kuwaambia wateja.

 

Connect With Us

 

New Project?

We do not just put codes to make a system, we help companies in their digital transformation challenges. We automate business process, workflows and communication.

Image