Njia 7 za kuongeza wasomaji wa Blog yako

Njia 7 za kuongeza wasomaji wa Blog yako

 1. Ishi kwenye blogu yako, chagua uelekeo unaokufaa.

Kama umekuwa ukifuatilia tasnia hii ya blogu, utagundua kuwa makala nyingi zinazoandikwa kwenye blogu nyingi za Tanzania huwa zinafanana sana, na hata muelekeo wa hizi blogu huwa ni uleule. Ingawa ni jambo la kawaida kwa kila mtu kukimbilia sehemu inayopendwa na wengi (blogu za habari), lakini jinsi unavyokimbilia sehemu yenye watu wengi, ndivyo jinsi unavyongeza ushindani.

Siyo tu ushindanni, bali wengi wamejikuta wakiingia kwenye uelekeo ambao hawaumudu hivyo siku ya mwisho wanajikuta wakikopi na kupaste.

Hivyo, jambo la muhimu ni kuchagua uelekeo unaoupenda na kuuweza, mara nyingi kazi ya kublog huwa rahisi kama unablogu kitu unachokipenda, mfano, binafsi nikiwa ninaandika makala zenye uelekeo wa IT kwenye Blog ya Dudumizi, kwakuwa ninapenda IT na ndiyo maisha yangu ya kila siku hivyo kwangu kuandika makala za IT ni sehemu ya maisha yangu, na jinsi kazi inavyokuwa rahisi ndivyo utakavyoweza kuandika makala nyingi zaidi na zenye mvuto zaidi, hivyo huvutia wengi zaidi.

Pia jinsi unavyokuwa wa kipekee, ndivyo unavyopata watemebeleaji wengi zaidi, mfano, badala ya kukimbilia kwenye blogu za habari na michapo, kwanini usijikite kwenye blogu za yanayoendelea vyuoni na kuonesha maisha ya wanafunzi, kwanini isiwe blogu ya hadha ya usafiri na foleni nk.

Wana blogu wanatakiwa kuwa wabunifu, wawe watu wanaofikisha maono yao juu ya mambo ya kijamii kwa kutumia intaneti, na wao ndiyo wataisaidia jamii yetu.

Kumbuka; Unapochagua uelekeo,itakusaidia kujua nani mlengwa wako, na vitu gani muhimu huyo mlengwa wako vinamuhusisha, hapa utaangalia mambo kama elimu, upeo wa uelewaji na hata vitu wanavyopenda kusoma. Kwa kujua vitu hivi itakusaidia kuandika makala zinazosomwa na zenye kueleweka na wahusika. Kumbuka, haublogu ili usome wewe mwenyewe bali ni kwa ajili ya watemebeleaji wako. Hivyo kuwafahamu wao ni moja ya hatua muhimu itakayowawezesha kusoma na kuzipenda makala zako.


2. Tumia mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii ni kitu cha lazima kama unataka kuongeza watemebeleaji wa blogu yako. Mitandao hii ni vijiwe vya mamilioni ya watemebeleaji ambao pia ni watemebeleaji wa blogu yako pia, hivyo ni lazima uhakikishe unatumia vyema mitandao hii.

Hakikisha kila makala ya blogu yako inaenda moja kwa moja kwenye mitandao jamii, pia hakikisha kwenye kila makala kuna kitufe cha share, like, g+ nk mbavyo vitawawezesha muingiliano na mitandao jamii.

Ingawa mitandao jamii ni muhimu, lakini, epuka matumizi yaliyozidi na hata kuwachukiza watembeleaji, kuna baadhi ya blogu kila unapofungua unakutana na kidirisha cha
kulike ambacho hukuzuia kufanya lolote mpaka ulike kurasa ya Facebook. Hi inaweza kuwa kero kwa watembeleaji wa blogu yako. Kitu cha muhimu hapa ni, usiwalazimishe
watu kulike au kushare makala zako, bali washawishi kwa ubora wa makala.

3. Blogu yako iwe na spidi ya haraka

Je ni watu wangapi wapo tayari kusubiria dakika tano mpaka blogu yako ikawa tayari kufunguka? Kama wewe blogu yako ni mpya, ni dhahiri kuwa hakuna atakayesubiri, na kama wewe blogu yako ni maarufu, basi watasubiri kwakuwa hakuna mbadala na pindi watakapopata mbadala basi wataanza kupungua siku hadi siku.

Blogu kuchelewa kufunguka kunaweza kusababishwa na mambo mnegi kama uwingi wa makala, teknolojia iliyotumika na hata mrundikano wa vitu; mfano, kwenye blogu nyingi za Tanzania, kumekuwa na rundo la matangazo kabla ya kuanza kwa makala, na matangazo haya ni picha kubwa ambazo kila moja inachukua ujazo tosha na kuifanya blogu iwe taratibu sana.

Kuna njia nyingi za kuonesha makala na matangazo idadi sawa kwa mtindo ambao hautoathiri spidi ya blogu yako ambayo nimeielezea kwenye kipengele cha muonekano.


4. Fikiria jina kamili

Blogu kama ilivyo Website, inaweza kuwa na jina, leo hii kuna blogu nyingi sana maarufu zina majina, kama www.mjengwablog.com, www.8020fashionsblog.com nk, kuwa na jina kamili la blog yako kutasaidia kukumbukika na pia itakusaidia kwenye mitandao ya utafutaji. Si hayo tu, pia itakusaidia pindi unapotaka kuhamia kwenye website kamili kwani hautatakiwa kuwataarifu watembeleaji tena.

 Nimewahi kuandika mambo ya kuzingatia pindi uchaguapo majina ya website  / blog

Kwa wale wanaotumia Blogspot, unaweza kununua jina (domain) halafu ukalielekeza kwenye blogspot na watu wakatumia jina kamili kufungua blog yako na sio .blogspot.com tena ila wewe utaendelea kuichunga kwenye blogspot kama kawaida.

Gharama ya jina haizidi elfu 20 ya kitanzania, unaweza nunua kwa kwenda hapa


5. Muonekano bora ni kitu cha lazima


Kwenye falsafa ya watumiaji wa mitandao tunasema; mtembeleaji wa wavuti hutumia sekunde zisizozidi tatu kutafuta anachokitaka na kama atashindwa kukipata, basi kutimka, hivyo blogu yako ni lazima iwe na uwezo wa kufikisha ujumbe na kumvutia somaji ndani ya sekunde tatu.

Blogu isiyovutia haiwezi kuwa na watembeleaji wengi, na hata kama wengi wanakuja, basi hutimka (baunce) bila kusoma chochote. Leo hii kuna makampuni mengi sana yanayoweza kukusaidia kutengeneza blogu au website kwa gharama nafuu kabisa, unaweza kutafuta kwa kuandika website design in tanzania kwenye google na kuangalia makampuni yanayoweza kukusaidia.

Ingawa mitandao ya blog kama Bloggers ni mizuri kwa kuanzia, ila jinsi blog yako inavyozidi kukua, ndivyo umuhimu wa kuwa na blog inayojitegema unavyoongezeka.


Gharama za kutengeneza blog isiyo ya blogspot.com si ghali na hi itakupa uwanja mpana wa kuchunga na kuiboresha blog yako.

6. Takwimu ni muhimu pia
Ingawa mada ni jinsi ya kuongeza wasomaji wa blog yako, lakini hatuwezi kuacha kuongelea umuhimu wa takwimu. Kuna usemi unaosema, kama usipoipima, basi hautoweza kuiboresha. Hivyo kwa kuwa na takwimu ya watembeleaji wa blog yako, siyo tu itakuwezesha kujua mtiririko wa wasomaji, bali wanapotoka, wanatumia muda gani kwenye blog yako nk.

Takwimu zitakusaidia kupanga mikakati ya kujitanua na kujitangaza zaidi, pia zitakuwezesha kuthaminisha harakati zako za ukuaji. Na takwimu hizi zinapatikana kwa kwenda Google Analytics.


7. Usisahau watumiaji wa simu
Takwimu zinaonesha, watumiaji wa intanet wengi hutumia simu za mkononi kufungulia website, na idadi hii huongezeka siku hadi siku. Hivyo, kama wewe ni mmiliki wa Blog, hakikisha blog yako inaonekana vyema kwa watumiaji wa simu.

Kama website yako haifunguki kwenye simu, basi jua kwamba unapoteza mamia ya watembeleaji siku hadi siku. Hivyo wakati ndiyo huu, nenda kisimusimu zaidi.

Connect With Us

 

New Project?

We do not just put codes to make a system, we help companies in their digital transformation challenges. We automate business process, workflows and communication.

Image