Ujumbe wa mwaka 2015 kutoka Dudumizi

Ujumbe wa mwaka 2015 kutoka Dudumizi

 Na kama ilivyo ada yetu, sisi siyo tu inakupa huduma ya IT, bali pia jinsi gani ya kuitumia IT kwa ajili ya biashara, na hii ndiyo hazina kuu ya Dudumizi.

Kwa mwaka 2014, Dudumizi imekuwa ikitumia muda mwingi kujijengea uwezo wa ufanyaji kazi na kuelewa mazingira halisi ya ufanyaji kazi, kwa mwaka huu wote Dudumizi tumekuwa tukifanya kazi zilizokuja toka kwa wateja wetu, na sehemu kubwa (zaidi ya 80%) ya wateja wetu wa Dudumizi walikuja moja kwa moja toka online, na 17% walikuja kama utambulisho toka kwa wateja wetu wa awali (Referrals) na waliobaki walikuja kutokana na mazungumzo ya moja kwa moja.

Moja ya vitu muhimu ambavyo uendeshaji wa Dudumizi umevipa vipaombele ni huduma bora kwa wateja wetu na kuwafanya waridhike. Na hili tumeridhihirisha kwa kuhakikisha hakuna mteja aliyetukimbia Dudumizi kwenda kwenye kampuni nyingine. Wateja wetu wengi wamekuwa wakisema, Akhsante Dudumizi.

Mwaka 2015 ndiyo umeanza, kama nilivyodokeza awali, neno hili limetoka katikati ya mwezi na siyo mwanzo ni kwa sababu, tulihitaji muda kukamilisha mpango kazi wa Dudumizi na malengo yake na kujiridhisha nao kabla hatujaenda mbele zaidi. Hivyo, kwa mwaka 2015, Dudumizi inatarajia kufanya yafuatayo;

Uboreshaji na Upanuzi wa huduma kwa mteja: Kwa mwaka huu wa 2015, Dudumizi itaendelea kukupatia wewe mteja huduma zilizo bora zaidi. Dudumizi imepanua wigo wa huduma kwa mteja kwa kuanzisha dawati maalumu la huduma, kuanzia sasa kuna muhusika wa huduma kwa wateja mwenye ufahamu wa IT ambaye ndiye atahusika kupokea simu zote toka kwa wateja wetu, kuwa na muhusika mwenye ufahamu wa IT na huduma kwa wateja, kutasaidia kupungua kutoelewana kati ya wateja na muhudumia wateja. Kutana Maneja wa dawati la wateja (Service Desk Manager) kwa namba 0768816728 au barua pepe support(at)dudumizi.com.

Utengenezaji wa systems zetu wenyewe: Katika mkakati wa ukuaji wa mwaka 2015, Dudumizi pia inatarajia kuanza kutoa bidhaa (products) zake yenyewe. Bidhaa hizi, zitalenga kuja kuongeza ufanisi kwenye ufanyaji wa kazi hapa Tanzania. Muda ukifika, mutaweza kupata taarifa za kina juu ya bidhaa husika. Tukiwa ni kampuni ya wazawa wenye uelewa na uzoefu kwenye idara hii, tegemea kupata web systems zenye tija kwa maisha ya kila siku ya Mtanzania,na siyo kukuongezea mzigo.

Utambuzi wa vipaji: Pia, Dudumizi inatarajia kuanza kuwashirikisha wadau mbalimbali toka mavyuoni, ni programu endelevu yenye kulenga kukuza vipaji vya wanafunzi walio mavyuoni na kuwajengea uwezo wa ufanyaji kazi kivitendo huku tukiwatambulisha kwenye uwanja wa ujasiriamali. Programu hii ipo kwenye mchakato, nayo muda wake wa kuanza ukifika mutataarifiwa.

Makazi Mapya: Dudumizi, inatarajia kuhamima New Home kuanzia mwezi wa pili, ofisi madhubuti zitakazoendana na mpango kazi wa Dudumizi wa mwaka 2015 kama ulivyopewa jina, Dudumizi Vision2015. Bado tutakuwa maeneo ya Mbezi Beach, ila kwenye jengo bora zaidi na lenye miundombinu muhimu kwa ufanyajikazi bora.

Kufikia wateja wengi zaidi kiubora: Katika kuhakikisha tunatanuka na kukua zaidi, Dudumizi tumeanzisha kitendo kipya, Business Development, ambacho kitahusika na kukuza mahusiano kati ya wateja na kampuni. Kitengo hiki pia kitahakikisha ubora wa bidhaa tunazozitoa sokoni unakuwa wa kuaminika. Ziwe ni bidhaa zenye kukidhi matakwa ya wateja. Ni kitengo hiki kitakachojihusisha na kuhakikisha Dudumizi inafikia watu wengi zaidi na kuwa ni nenmbo inayotegemewa na kuaminiwa na wengi Tanzania.

Bodi ya ushauri: Ni mwaka huu ambapo Dudumizi itaunda Bodi ya ushauri itakayowahusisha wadau mbalimbali wenye uzoefu wa kina kwenye masuala ya IT, Biashara na Uongozi. Lengo ni kuhakikisha tunakidhi matakwa ya wateja wetu. Pia, tunaweza kukua siku hadi siku.

Jicho pevu kwa SMEs: Dudumizi, pia, itahakikisha inafanya kazi bega kwa bega na wafanyabishara wadogowadogo ili kuhakikisha wanatumia IT kama sehemu ya biashara zao. Na kwa jicho hili, Dudumizi itawatambua na kuwawezesha wafanyabiashara maarifa bora ya IT na Biashara.

Ubunifu zaidi: Kuumbuka, kama slogan yetu inavyosema, "Think.Innovate", sisi Dudumizi, hatutoisha kufikiria na kujenga zaidi.Na tutajijenga kiufanisi na kuhakikisha wale wote waliopo kwenye ngarawa ya Dudumizi wanakuwa salama na wengi furaha siku zote.

Ingawa kuna mengi Dudumizi inatajia kuyafanikisha, lakini bado tunathamini sana mchango wako kwenye kuyaboresha au kutupa mengine zaidi, Dudumizi inapenda kupata maoni yako na ushauri juu na nini unadhani kifanyike ili kukuza au kuongeza ufanisi kwenye ufanyaji kazi wetu? Tuandikie kwenda info(at)dudumizi.com.

Kumbuka, safari ya maili elfu moja, ilianza kwa hatua moja.

Kwa mara nyingine tena, tunawatakia Heri ya Mwaka mpya, 2015. 新年快乐!

Mkata Nyoni (马德)
Managing Director
Dudumizi Technologies LTD

Connect With Us

 

New Project?

We do not just put codes to make a system, we help companies in their digital transformation challenges. We automate business process, workflows and communication.

Image