Wakati tunaelekea kukamilisha mwaka wa 2018 na kuukaribisha mwaka mpya 2019 na kuhakikisha tunaendelea kuwa Kampuni bora kwa Website Design, App Development , Domain registration na Hosting huku tukihakikisha bidhaa zetu kama Michongo TanzMEDDuhosting na Kitonga Tanzania zinawafikia walengwa kwa ufanisi wake, timu ya Dudumizi mwaka huu tumeendeleza kuboresha mahusiano ya timu kwa zoezi la zawadi. Zoezi hili lilianza wiki iliyopita ambapo kama ilivyo ada ya Dudumizi, siku ya jumanne huanza na 15 minutes presentation kutoka kwa team member mmoja wapo. Baada ya hapo, kila mmoja alitakiwa kuchagua jina la mtu atakayekuwa ndiye msiri wake kutoka kwenye bakuli.  Sheria ya hili, ilitakiwa kuwa siri na hakuna mtu aliyetakiwa kujua ni nani atamuandalia zawadi.

Baada ya wiki moja, siku ya leo, zoezi lilianza vyema kwa presentation ya asubuhi ambapo Developer wetu Sophia Mangapi alianza kwa mada yake nzuri ya Personality, baada ya hapo zoezi la zawadi lilianza. Na kila mtu alitakiwa kuchagua namba ili kujua nani anaanza. Zoezi lilikuwa lenye kuvutia na wengi walilipenda, alisikika Meneja wa Huduma na Wateja Bi Lucy Vicent akisema, hii ilitakiwa iwe imeanza zamani saaaana.

Umuhimu wa zoezi hili ni kuhakikisha mahusiano bora ya wana Dudumizi, pia kuongeza kujaliana na kujuana ili kuhakikisha tunawapa wateja wetu huduma zilizo bora kabisa.

 

Sophy akifurahia zawadi yake kabla ya kuifungua

 

Service manager wa Dudumizi, akikabidhi zawadi yake kwa mmoja wa Interns

 

Dudumizi MD akimkabidhi Herbert (PM) zawadi yake akiwa ni secret mate wake.

Product Manager wa Michongo, Bi Getruda akifungua zawadi yake huku akichungulia kunani ndani.

Product Manager wa Kitonga Tanzania Bi Hadija akipokea zawadi kutoka kwa Sophy

Lucy akifurahia ujumbe uliopo kwenye zawadi aliyopatiwa.

Vifungashio vya zawadi vilitapakaa kwenye meza ya project Manager (Herbert)

 

Call us now