Siku ya ijumaa, tarehe 28/09/2018 ilikuwa ni siku yenye furaha kwa wadau wote wanaopenda ubunifu haswa katika sekta ya Afya. Ilikuwa ni siku ya uzinduzi rasmi wa jukwaa la Afya linalopatikana kwa njia ya Website na Application ya simu.

Timu ya TanzMED inayoundwa na vijana wanne akiwemo MD wa Dudumizi ndiyo waanzilishi wa mtandao huo, walikuwa na hafla fupi ya kuitambbulisha rasmi. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Buni zilizopo katika jengo la Sayansi (COSTECH).

 Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mablimbali wa sekta ya afya, waanishi wa habari, pia sherehe hii ilihidhiriwa na Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania Dr Amos Nundu akiwa ndiye mgeni rasmi. Akiongea juu ya vijana na ubunifu, Dr Nundu aliwaasa vijana kuongeza ubunifu katika kusaidia jamii, huku wakiunga mkono juhudu za Mh Rais za serikali ya viwanda kwani hakuna maendeleo ya viwanda katika jamii isiyo na Afya njema. Pia, aliwapongeza vijana wanaounda timu ya TanzMED kwa ubunifu wao kkatika kuielemisha jamii kwani siyo tu wataweza kuwasaidia wanajamii kuwa na Afya njema, bali pia, inaweza kuzalisha ajira nyingi.

Kazi yao itakuwa na msaada mkubwa ukizingatia imepata baraka zote kutoka Wizara ya Afya. Na kupokelewa kwa mikono miwili na jamii. kazi hii kwa kiwango kikubwa imefanyiwa kazi kwa ushirikiano wa Dudumizi, tanzMED na wadau wengine. Unaweza kuiona moja kwa moja kwenye playstore 

Call us now