Dudumizi inayofuraha kuzindua mtandao wa kuuza na kununua vitu kwa njia ya mtandao. Mtandao huu unaojulikana kwa jina la Kitonga unakuwezesha wewe muuzaji kuweka taarifa za huduma au bidhaa zako na wanunuzi watakutafuta popote ulipo. Bidhaa hizi zinaweza kuwa ni mpya au zilizotumika (used products). Kuna makundi mengi ya bidhaa kama magari, viwanja, nyumba, vifaa vya electronics, vifaa vya michezo, vifaa vya urembo, nguo, bidhaa za kilimo, huduma za kitaalamu na nyingine nyingi, tembelea https://kitonga.co.tz kujiona zaidi.

 Tofauti na mitandao mingine ya aina hii (C2C) ambayo wengi huishia kuonesha taarifa za muuzaji na hakuna njia nyingine rahisi ya kuchunga ubora, kuonesha matokeo ya tangazo lako nk. Kitonga hupitia bidhaa zote kabla hazijaonekana kwenye website, hii husaidia kupunguza matapeli ambao wanaweza kutumia nafasi hii kuwatapeli wengine. Pia, inasaidia kuhakikisha siku zote, Kitonga Tanzania inaendelea kuwa jukwaa tegemewa kwa huduma na bidhaa bora Tanzania.

Pia, kwa kutumia mtandao wa kuthaminisha (rating & feedback System) ulio ndani ya Kitonga Tanzania, wanunuzi pia wanaweza kutoa taarifa juu ya hali na ubora wa huduma au bidhaa kutoka kwa muuzaji ili wengine wanaotaka kufanya naye biashara wawe makini.

Pia, kwa kutumia mtandao wetu mpana wa Dudumizi, wauzaji watapata nafasi nzuri ya kujulikana zaidi, kwani sisi focus yetu kubwa ni kuhakikisha unafikia wanunuzi wengi na kwa haraka.

Kwanini kitonga?

Kama inavyojieleza, Kitonga linamaanisha mteremko au urahisi wakati wa kushuka na ugumu wakati wa kupandisha, hivyo Kitonga inachukua kazi ngumu ya Kutafuta wateja na kuwa mteremko, hivyo kwa kuweka bidhaa au huduma zako kwenye Kitonga Tanzania, utafikia wateja wengi kama unaserereka.

Jinsi ya kutuma bidhaa kwenye Kitonga

Ni rahisi sana kutuma bidhaa zako kwenye Kitonga Tanzania, fuata hatua zifuatazo,

1. Tembelea https;//kitonga.co.tz na ubonyeze kitufe cha Post an add (Kama haujajisajili, utatakiwa kujisajili. Kama tayari umeshajisajili, basi utatakiwa kuingia (login) kwenye Website) ili uweze kuendelea

2. Baada ya kuingia, basi utafunguka kurasa utakaokuwezesha kuingiza taarifa za bidhaa yako, hakikisha unaingiza kiufasaha na kuweka maelekezo ya kutosha ili watumiaji wa Kitonga Tanzania waweze kuielewa na hatimaye kuwasiliana nawe.

 

Baada ya kutuma kitonga chako, kitapitiwa na timu yetu ndani ya masaa 24, na kitaonekana kwa watumiaji, hakikisha unaweka taarifa zako na za bidhaa ili kuweza kutambulika kiurahisi. Muonekano wa bidhaa / huduma ndani ya Kitonga Tanzania utakuwa hivi.

 

Call us now