
Jinsi Tehama inavyoweza kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwenye sekta ya Afya
Miaka saba iliyopita wakati tunajiandaa na utengenezaji wa jarida la Afya, niliwahi kuandika makala inayohusiana na umuhimu wa tehama kwatika sekta ya Afya, makala hii inapatikana katika wavuti ya TanzMED Tekinolojia, ni ufanisi au chanzo cha ugoigoi kwenye afya? . Wakati huo, nilikuwa na mawazo chanya kwenye umuhimu wa IT katika sekta hii muhimu kwa Afya njema kwa wote.
Katika ulimwengu wa IT wa sasa, tunaamini kuwa, IT si muwezeshaji tena, bali ni sehemu ya kazi, hii inamaanisha, katika mipango kazi yoyote, IT ni lazima iwe ndani ya mipango hiyo na si sehemu ya kutekeleza mipango kazi. Maisha yetu ya kila siku yamekuwa yakitegemea IT kwa kiwango kikubwa.
Afya ni moja ya maeneo ambayo yamefaidika sana na ukuaji wa IT, sasa imekuwa rahisi uhifadhi wa kumbukumbu kwa kutumia Hospital Management Systems, upatikanaji wa matokeo ya vipimo kutoka maabara umekuwa ni wa papo kwa papo, na hata ufanyaji kazi umeimarishwa sana kwa madaktari kuweza kubaini matatizo kwa uharaka sana kwa msaada ya Teknolojia, tumekuwa tukisikia Robot zikifanya vyema upasuaji kuliko watu tena kwa kiwango kikubwa cha ufanisi.
Kitu au sehemu ambayo bado kuna changamoto ni kuwezesha maarifa na taarifa za Afya kupenya kwenye maisha ya kila siku ya watu, taarifa za Afya bado hazijakuwa rahisi kupatikana haswa kwa nchi zetu zinazoendelea. Leo hii ni watu wachache wenye uelewa wa magonjwa, ni wachache wenye kusoma matokeo ya tafiti mbalimbali duniani ili kuwa na uelewa wa masuala ya Afya. Hii ni kwa sababu bado hakuna njia rahisi na rafiki ya kuwafikishia taarifa na maarifa.
TanzMED, ni moja ya jukwaa la Kiswahili lililo jikita kwenye kufikisha taarifa na maarifa ya Afya kwa njia rahisi na kirafiki. Likiundwa na timu ya wataalamu wa sekta za Afya, Tehama na Mawasiliano, Jukwaa hili hutumia Application ya simu (Mobile App) na pia kwa njia ya Website. Jukwaa hili limesheheni taarifa na maarifa ya Afya yenye kukuwezesha kuchukua maamuzi sahihi. Hii ni kwa sababu, kama una maarifa na taarifa za kutosha, basi utachukua maamuzi yaliyo bora na na unayo yaelewa.
Mfano, kwa sasa kuna kampeni nyingi kuhusu uhamasishaji wa watu kupima virusi vya Ukimwi, Wanawake kufanya uchunguzi ili kubaini Saratani za matiti, wanaume kupima maambukiz au saratani ya tezi dume nk, harakati hizi haziwezi kuwa na matokeo chanya kama jamii haitokuwa na maarifa na kujua umuhimu na mahali husika pa kufanya vipimo hivi, na hili si jukumu la serikali pekee, hivyo wadau wa sekta mbalimbali ni lazima tushirikiane kusaidia kwenye kuelimisha jamii kwa maendeleo chanya, hivyo TanzMED inakuwa ni jukwaa lenye kuleta manufaa kwa jamii.
Mfano, leo hii ukiwa Google na kutafuta ugonjwa au jambo lolote la Afya, utapata tovuti ya TanzMED au Application ya TanzMED, siku ya mwisho jamii nzima inanufaika.
TanzMED ina kuwezesha;
- Kusoma makala za afya zilizoandikwa na madaktari bingwa
- Kusikiliza simulizi za makala za Afya
- Kupata orodha ya hospitali, zahanati, maduka ya madawa, maabara za vipimo, nk
- Kupata zana za Afya (medical tools) kama ya kutambua siku za hedhi (metsrual tracker), Kikokotoa uwiano wa uzito (BMI Calculator), Kumbusho (Medical Reminder), K
- Kloniki ya Watoto
- Kuweka miadi (Appointment) na hospitali
- Kupata ushauri wa wataalamu wenye kulenga kukupa muongozo wa masuala ya Afya ya watoto, wanawake, magonjwa nk
- Elimu ya magonjwa kama kisukari, ukimwi, saratani nk
Hivyo, ujio wa TanzMED ambayo imepewa nguvu na DLI taasisi yenye kutoa ruzuku kwa mawazo yenye tija kwa jamii, utakuwa na manufaa kwa wengi. Tembelea Website https://tanzmed.co.tz au Download Application kwenye playstore https://play.google.com/store/apps/details?id=com.dudumizi.tanzmedtz