Katika dunia ya leo ya mapinduzi ya Internet, website, Application za simu na hata mifumo ya komputa (Systems), vimekuwa ni nyenzo thabiti katika maisha ya binadamu. Wengi wetu tumekuwa tukitumia mifumo hii bila kujua jinsi inavyofanya kazi au ni wapi inapokaa. Ingawa kwa mtumiaji, hiyo si kitu muhimu, muhimu ni kuwa, inapatikana pale anapohitaji. Ila, upatikanaji huu huweza kuathiriwa na wapi mifumo inakaa. Na, kitendo cha kuwezesha mifumo hii kupatikana kutoka pale inapokaa, ndiyo tunayoiita Hosting, ama wengi wanavyoita Webste Hosting. Website Hosing, imegawanyika katika makundi mengi sana, kuna Shared, VPS, Dedicated Server au Cloud Hosting.

Kwa Tanzania, watumiaji wengi hutumia aina ya shared hosting (website zaidi ya moja kuwa sehemu moja), aina hii ya hosting imekuwa na msaada kwa wengi, hii ni kwa sababu ya urahisi wake katika gharama na hata uangalizi wa mazingira ya hosting kwakuwa kama mmiliki wa Website, hauhitajiki kuchunga mazingira hayo bali kwa yule anayetoa huduma (Website Hosting Company), mfano wa watoa huduma ni Duhosting.

Ili kuweza kuelewa, hebu tuangalie aina mbalimbali za Website Hosting.

Dedicated Hosting

Aina hii ya hosting ni ile ambayo, unakuwa na umiliki wa server nzima mwenyewe. Inaweza iwe kwenye sehemu yako (kama maofisi mengi wanavyofanya) au ya kukodisha server online. Aina hii ya hosting huwa tunaifananaisha na mtu kujenga ama kukodisha ghorofa nzima.

Faida ya dedicated server ni kuwa, unakuwa na hazina (resources) za kutosha, pia spidi na usalama unakuwa wa hali ya juu kama utaweza kufanya maboresho ya kiumfumo (optimization) yanayotakiwa.

Aina hii inawafaa sana, makampuni makubwa, watu binafsi wanaotaka kuanza biashara ya Hosting au wale wanaomiliki website zenye mahitaji makubwa ya resources, kama makampuni ya betting.

Hasara zake ni kuwa, unahitaji waangalizi na wataalamu wa kutosha watakaochunga server yako. Pia, gharama zake huwa ni za juu ukilinganisha na aina nyingine za Hosting.

Virtual private Server (VPS)

Aina hii, haina utofauti sana na Dedicated Hosting, kimsingi, VPS hutokea baada ya Server moja kugawanywa (partitioned) kwa kutumia software na kuwa server zisizo bayana (Virtual) zaidi ya moja zinazojitegemea kimfumo. Hivyo, hardware zitakazotumika ni zilezile isipokuwa kwenye software, kila VPS itakuwa inajitegemea kabisa. Hivyo, VPS kuna sehemu inakuwa kama Dedicated Hosting ila kuwa sehemu inakuwa siyo.

Faida kuu ya VPS ni kuwa, ina sifa nyingi za Dedicated ikiwa kama matumizi binafsi ya hazina (dedicated resources) na hata usalama (ingawa kuna mazingira hatarishi huweza kuathiri VPS kutokea kwenye VPS nyingine iliyopo kwenye server moja).

Mfano halisi wa VPS, ni sawa na ndani ya ghorofa moja, litakatwa wings, na kila wing ikawa inajitegemea kila kitu, hivyo kwa watu wa wing ile, wanajiona kama wapo kwenye ghorofa lao wenyewe.

VPS, huwafaa sana watu wenye website zenye kutembelewa na watu wengi (high traffic), mfano, website ya habari/blogs au zile zenye mahitaji maalumu, mfano kwa website zinahitaji kipachiko (extensions) nyingi kuliko zinazopatikana katika mazingira ya kawaida. Pia, aina hii ya Website hosting inawafaa sana watu wenye kuhitaji kuanzisha huduma ya Website Hosting ila hawana mtaji mkubwa kuweza kumiliki Dedicated server, au wale wenye mahitaji maalumu ambapo hawapendelei kuchanganyika na wengine.

VPS, pia inakupa uwezo mkubwa wa kujibrand, hii ikijumuisha kutumia IP na Name Server zako mwenyewe (Dedicated IP). Na pia, unakuwa na uwezo wa kuinstall program nyingi. Ingawa kuna baadhi ya program, hauwezi kuinstall kwenye VPs kama, VPN (Virtual Private network) Server.

Tofauti ya VPS na Dedicated server huwa kwenye utendaji kazi na hata ukuaji, mfano, ukiwa na Dedicated server na ujazo (storage/space) ikawa imejaa, ni rahisi kuongeza ujazo bila kuhama, kitu ambacho si rahisi kwa VPS za kukodisha.

Shared Hosting

Shared hosting ni aina ya Hosting ambayo ndani ya server moja, huhost website zaidi ya moja na website hizi hugawana hazina (resources) zilizomo. Kwa, shared Hosting nyingi, kila website inayo uwezo wa kutumia resources zozote zilizomo mpaka zitakapokwisha, hivyo ufanyaji wake kazi hutegemeana sana na jinsi resources hizi zinavyotumika. Na ndiyo maana, kama kuna Website moja inatumia sana resources, huweza kufanya nyingine kuathirika kwa kuwa na spidi ndogo au zisipatikane kabisa.

Shared hosting, unaweza kuifananisha na nyumba ya kupanga ambapo ndani ya nyumba moja, kuna vyumba vingi ambavyo kila kimoja kina mpangaji wake. Hivyo, kama mpangaji mmoja atafungulia redio kwa sauti ya juu, basi wapangaji wengine wote watasikia makelele.

Shared hosting ni kundi ambalo watu wengi huangukia, ni kundi ambalo halihitaji utaalamu mwingi kuweza kulitumia, na hata upatikanaji wake huwa kwa bei nafuu sana. Mfano, Duhosting tunatoa huduma hii kwa kuanzia Tsh5000/= kwa mwezi.

Shared hosting huwafaa sana wale wenye website ndogo au walio na bajeti ndogo ya kuanzia. Ni chaguo la haraka kama ndiyo unataka kuanza safari yako online. Mara nyingi, gharama halisi ya shared hosting hutofautishwa kwa kiwango cha ujazo (Storage/space), mfano 1GB, 2GB nk huku watoa huduma wengi huwa hawaweki ukomo wa mafaili yanayoweza kupita (bandwidth).

Shared hosting ina faida nyingi, kama gharama zake kuwa chini, urahisi wake kwenye matumizi, na pia haihitaji uelewa sana wa uchungaji wa server. Ila, ina hasara zake, kama kutokuwa na uhakika wa resources utakazopewa, spidi kuwa ndogo na hata usalama wake.

Ukiangalia kwa umakini, iwe Dedicated server, VPS au Shared Hosting, matumizi yake na faida hutegemeana na sababu na aina ya website yako. Shared hoting imekuwa ni kimbilio la wengi wakati Dedicated server ni kwa ajili ya wale wanaohitaji hazina ya kutosha. Katika makala zijazo, tutaangalia aina nyingine ya Hosting ambayo leo hatujaigusia, nayo ni Cloud Hosting.

Call us now