SSL Certificate ni cheti cha kieletroniki chenye taarifa muhimu zinazohusiana na Kampuni au mtu. Pindi funguo zenye taarifa ya cheti hiki zinapofungwa kwenye seva, basi husababisha browser kuonesha alama ya kufuri likimaanisha kuwa mawasiliano yote kati ya seva na browser yatapita kwenye njia salama. Mara nyingi, mtindo huu hutumika sana kulinda taarifa muhimu kama kwenye mabenki, manunuzi ya online na sehemu yoyote online inayopokea taarifa muhimu za mtumiaji.

Kwa siku za karibuni, tumeona ongezeko la matumizi ya SSL Certificates hata kwenye websites za kawaida ambazo hazipokei taarifa za watumiaji. Hii ni kwa sababu, mtandao wa utafutaji wa taarifa za mtandaoni (Google Search Engine) wameweka SSl certificate kama moja ya vigezo vyake katika upangaji wa utafutaji wa taarifa, hivyo watu wengi wameamua kutumia fursa ili kujiweka katika nafasi nzuri ya upatikanaji kwenye mitandao (online visibility).

Je SSL Certificate inatambulisha nini;

Kwenye kila SSl Certificate, kuna mambo vitu viwili

 • Jina la website na seva iliyopo
 • Taarifa za mmiliki (eg jina, aina ya biashara, anuani nk)

Kabla ya kuanza kutumia SSL Certificate, unahitajika kuinstall SSL Certificate kwenye seva. Mara unapomaliza, mawasiliano yote kati ya seva na watumiaji yatapita kwenye njia salama. Moja ya ishara kuwa mawasiliano yanapita kwenye makubaliano yaliyo salama, utaona ile alama ya HTTP imebadilika na kuwa HTTPs, na pia kuna kufuri la kijani kabla ya anuani kuanza. Kuna aina nyingine za SSl Certificate huifanya sehemu yote ya anuani (address bar) kuwa ya kijani na jina la kampuni huanza kutokea kabla ya kuanza kwa anuani.

Muundo wa SSL Certificate;

SSl hutumia kitu kinachoitwa Public key cryptography. Hii ni moja ya cryptography inayotumia namba mbili zinazounda kutokana na msururu wa namba zilizochanganywa changanywa, kwa lugha ya kitaalamu faili hili huitwa funguo(key) kwa sababu ndilo hutumika kufunga na kufungua taarifa kwa mpokeaji. Funguo hizi zimegawanyika katika makundi mawili, moja huitwa funguo ya nje(public key) wakati nyingine huitwa funguo ya ndani (private key). Kimsingi, taarifa hufungwa kwa funguo ya nje, na hufunguliwa na funguo ya ndani, hivyo kama hauna funguo ya ndani, basi hautokuwa na uwezo wa kufungua na kuona ulichotumiwa.

Funguo ya nje hujulikana na server yako ila hutolewa kwa mtu yoyote anayetumia web,na hii ndiyo hutumika kufunga taarifa kabla haitajumwa. Na ile private key hujulikana ndani tuu n, kumbuka, private key hutengenezwa pale unapoanza mchakato wa kutengeneza SSL Certificate. SSL Certificate huanza kutengeneza kwa kukusanya taarifa za umiliki utakaotumika kwenye kutengeneza cheti. Taarifa hizi hujumuishwa kwenye taarifa inayoitwa Maombi ya usainishaji (Certificate Signing Request, CRS). maombi haya hutumika na kujumuishwa kwenye utengenezaji wa SSL Certificate.

Jinsi SSL inavyofanya kazi;

Mfano, Juma anamtumia Yohana ujumbe, basi kwakuwa ufunguo wa nje wa seva itakayopokea taarifa za Yohana unajulikana, basi Juma atafunga taarifa kwa kutumia ufunguo wa nje (public key) wa Yohana na kuituma taarifa. Njia pekee ambayo Yohana atatakiwa kuitumia ili kuiona hii taarifa ni kwa kuifungua kwa kutumia funguo ya ndani (Private key). Kwakuwa ni Yohana pekee ndiye mwenye huu ufunguo wa ndani (private key) basi, ni yeye pekee ndiye atakuwa na uwezo wa kufungua hii taarifa.

Endapo katikati kukatokea hacker ambaye atavamiwa mawasiliano haya na kuiba taarifa kabla hazijafunguliwa na Yohani, hatoweza kuelewa kitu maana atakutana na taarifa iliyofungwa (cryptographic code).

Tukirudi kwenye ulimwengu wa Website, mawasiliano yote hutokea kati ya Website na seva, hapa kwetu, Juma na Yohana ndiyo website na seva zetu.

Kwanini unahitaji SSL Certificate kwa Website ya biashara yako

Ukiacha sababu za kuongeza daraja la website kwenye mitandao ya utafutaji, SSl Certificate ikakusaidia;

 • Kuongeza usalama wa taarifa kati ya mtumiaji na seva
 • Kuongeza uaminifu kwa wateja
 • Kuboresha biashara kwa kuvutia wateja zaidi

Jinsi ya kununua SSL Cerificate (Where to buy SSl Certificate in Tanzania)

Unaweza kununua SSLcertificate kutoka kwa makampuni mengi yanayotoa huduma za Website Hosting na kuinstall kwenye seva yako. Ila, kama ilivyo ada, kununua kutoka kwa makampuni ya karibu hukurahisishia pindi unapokutana na changamoto, pia ni rahisi kwenye njia za malipo maana unaweza kununua hata kwa kutumia malipo ya simu kama Mpesa na Tigo pesa, au hata cash.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua SSL Certificate

Kuna vitu vya msingi unatakiwa kuzingatia kabla ya kununua SSl Certificate navyo ni;

 • Hosting wako anaruhusu matumizi ya SSl kutoka njia

Kwa wale wanaotumia blogger, hauna uwezo wa kuinstall SSl Certificate iliyonunuliwa nje ya blogger kwa sasa, hivyo ni vyema ukainunua kutoka kwao. Hii pia hutokea kutoka kwa mitandao mingine inayotoa huduma ya free hosting.


 • Aina ya SSL unayohitaji

Kuna aina nyingi za SSl, hivyo ni bora ukajua ni aina gani unahitaji, aina kuu zinazotumiaka na wateja wengi ni kama;

 • SSL Certificate kwa ajili ya Website moja (www na isiyokuwa na www)
 • SSL Certificate kwa ajili ya Website na sub domain zake zote
 • SSL Certificate kwa ajili ya domain zaidi ya moja
 • SSL Certificate yenye mkanda wa kijani (EV)

Pia, ni vyema ukanunua SSL Certificate kutoka kwa makampuni yenye kuaminika. Kwa sasa Dudumizi tunatoa hii huduma, na unaweza kununua SSL Certificate Hapa.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now