Kufanya Update ya Website ni kitu cha muhimu kwa website Designer au mmiliki yoyote. Siku hizi, utengenezaji wa Website umerahisishwa sana. Wengi wanapendelea kutumia Content management System (CMS) kama Joomla, Woordpress au Drupal kutengenezea Website.

Uzuri wa kutumia CMS ni kuwa, kuna wachangiaji wengi ambao huangalia utendaji na uboreshaji wa kimfumo na kiutendaji. Hii hupelekea kuhitajika kwa update za mara kwa mara. Updates hizi huwa ni za kiusalama (Security fix), kiuboreshaji (Optimization) au kurekebisha tatizo (bug fix) linaloweza kupunguza utendaji wa Website. Hakikisha unajiunga na mlisho wa makala kutoka Joomla ili kupokea taarifa juu ya maboresho haswa yale ya kiusalama.

 Kwa kawaida hapa Dudumizi, tunawataka wateja wote wanaofanya Website Hosting, kuhakikisha Website zao zinatumia version mpya kabisa. Na pia, kama ni mmiliki wa website, hakikisha una mtaalamu wa IT ambaye atakusaidia kuifanyia maboresho ya mara kwa mara.

Video hii, itakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kufanya update kwenye Joomla Website, iwe ni ya Core Joomla au Extensions za Joomla.

Call us now