APE Network, ni kampuni ya Kitanzania inayojihusisha na Uchapishaji wa vitabu pamoja na kazi mbalimbali zenye malengo ya kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Katika moja ya hatua zake, kampuni hiyo ilitengeneza Application ya simu kwa watumiaji wa Android. Application hii ilikuwa inawawezesha watumiaji kujifunza na kusoma kazi mbalimbali za kiswahili kama Misemo, methali, nahau na Vitendawili ambayo inajulikana kama Swahili Sayings (Misemo ya Kiswahili)

Application hii imepokea muitikio mzuri kutoka katika jamii ya watumiaji wa Kiswahili kwenye mtandao,  watumiaji wengi wamekuwa wakitoa maoni chanya juu ya kazi hii. Ingawa Application hii ilikua na vitu vingi vizuri, lakini pia ilikuwa inahitaji maboresho zaidi ili kuifanya iendane na mahitaji na mabadiliko ya tabio za watumiaji, haswa kimuonekano (User Interface), muingiliano na mtumiaji (user engagement) na machaguo ya mtumiaji (user selection) na pia kuongeza mvuto wa kwa mtumiaji ili aendelee kuitumia tena na tena.

Ili kuboresha hili, timu ya APE Network, iliitafuta Dudumizi Technologies LTD, ili kuangalia ni jinsi gani inaweza kuboresha Mobile Application yake na kuifanya iwe bora zaidi. Kama ilivyo kawaida yetu, tulitumia muda mwingi kuisoma na kuielewa, ili kuja na features zenye kutatua tatizo lililopo.

Timu ya Dudumizi kwa kushirikiana na Mkurugenz wa APE Network (mr Hermes Salla) tumeweza kukamilisha Application bora kabisa ya Kiswahili Duniani ambayo sasa inapatikana kwenye Playstore 

Features:

 • Kusoma Misemo, Methali, Nahau na Vitendawili
 • Kusikiliza Misemo, Nahau, Methali na Vitendawili kwa sauti
 • Uwezo wa kutuma maoni (comment) 
 • Uwezo kugawana (share) na wengiine
 • Uwezo wa kushiriki kwenye mijadala
 • Uwezo wa kuhifadhi taarifa uzipendazo
 • Uwezo wa kuona picha kulingana na aina ya taarifa

Tulichokifanya (what we have done)

 Muonekano wa App kwa picha

Muonekano wa mbele wa Application ya Swahili Sayings

Jinsi taarifa zinavyoonekana, sauti, picha na hata maoni

 

Unaweza kutuma maoni na ukafuailia ya wengine

Baadhi ya features kwenye menu ya Swahili sayings

Na mengine mengi yanapatikana kwenye Swahili sayings, Pakua App hii kutoka Playstore, pia kwa mahitaji ya App Development Tanzania, tuandikia kwa ajili ya kukutumia Free Quotation hapa

 

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now