Mtumiaji wa website huwa anatumia dakika zisizozidi tano katika kutafuta kilichomplekea kwenye Website, hivyo ukiwa kama Website Designer unatakiwa kuhakikisha unatumia muda huo ipasavyo kuwafanya watembeleaji kuendelea kubakia kwenye Website yako. Siku hizi tumeshaachana na ule mtindo wa kuwa na mlundikano wa vitu kwenye kurasa za mbele za website, vinapokuwa vichache zaidi basi ndiyo ubora wake.

Katika kuhakikisha tunaongeza mvuto huku tukiwarahisishia wateja kupata picha na vitu vyote wavitakavyo kwenye kurasa moja, Dudumizi tumefanya maboresho ya kimuonekano na mfumo kwenye website yetui. Katika maboresho haya, mambo yafuatayo yameboreshwa;

  • Kutumiwa kwa Video badala ya picha, kwa ushurikiano na partners wetu, tumeweza kupata Video yenye kuendana na matakwa ya Dudumizi
  • Kutumiwa kwa icons badaya ya maneno ili kujenga mazoea kwa watumiaji
  • Matumizi  ya mitandao ya uhifadhi ili kuboresha speed
  • Muonekano wa kazi umeboreshwa na kuondoa kazi zilizopitwa na wakati
  • Muonekano wa kwenye simu nao umeboreshwa

Munonekano wa huduma za Dudumizi kwenye simu

 

Muonekano wa mbele wa Dudumizi

 

Call us now