Umuhimu wa kushikilia umiliki wa domain hata baada ya kufunga biashara

Unapomaliza kusajili na Jina la Website (Domain Name),kuna vitu vingi unaweza kufanya, wengi hudhani baada ya hapo kinachofuata ni kuanza Website Design. Kati ya vitu vinavyohusiana na domain, Domain Transfer na kubadili name Server ni moja kati ya vitu vinavyowachanganya wengi. Hata hapa Dudumizi tumekuwa tukipokea simu nyingi sana juu ya kupata ufafanuzi. Hivyo, kama kawaida yetu Dudumizi tunakurahisishia maisha ya kuwa mmiliki wa Domain Name.

Katika makala hii tutaangalia utofauti kati ya kuhamisha domain kwenda kwa msajili (registrar) mwingine (Domain Transfer) na kubadilisha namer Servers.

Msajili ni nani

Unaposajili Domain name, unatakiwa kuchagua msajili ambaye atakusajilia domain. Usajili huu huendana na mkataba wa umiliki wa domain. Ninapoongelea mkataba, ni mkataba wa muda wa umiliki, ingawa ni msajili ndiye anayekusajilia hii domain, lakini wewe ndiye utakuwa mmiliki halali wa hii domain kwa kipindi mulichokubaliana, mara nyingi huwa ni mwaka mmoja au zaidi. Na kila mwaka utatakiwa kurenew mkataba huu. Punde unapoacha kurenew basi umiliki wa domain yako utakuwa umeisha.

Kwa mfano, wasajli wa domain hapa Tanzania ni kama Dudumizi Technologies, Extreme Technologies, Web Technologies, ASYX Group na wegine wengi ambao unaweza kuwapata. Na kama unatafuta registrar wa nje ya nchi basi kuna Domain.com, Go Daddy, Hostgator na wengine wengi.

Gharama za kusajili domain hutofautiana kutoka registrar mmoja hadi mwingine, pia hutegemeana na kikoo cha domain, kwa mfano, kwa .tz hapa Dudumizi tunasajili kwa 20,000TZS wakati za .com tunasajili kwa 30,000TZS.

Kumbuka, si lazima kufanya Website Hosting na kununua Domain kwa mtu mmoja, kama unataka kufanya kwa makampuni tofauti, utahitajika kubadili name servers, makala hii inakufafanulia.

Sababu za ku transfer Domain

 • Unataka kumanage dmain na website hosting mahala pamoja
 • Umenunua domain ambayo ilikuwa kwa msajili mwingine tofauti na yule uliyemzoea
 • Umeuza Domain na mmiliki anataka kuhamisha kwa msajili wake
 • Kampuni iliyokusajilia domain inaelekea kufa au uwepo wake hauna uhakika

Mambo ya kuzingatia kabla haujaanza mchakato wa kuhamisha domain

Kabla haujaanza mchankato wa kuhamisha domain, unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;

 • Kama domain name ni ya .com, basi inatakiwa iwe imeshafikisha siku 60 tangu iliposajili
 • Unatakaiwa kufahamu kama name servers nazo zitatakiwa kubadilika baada ya kuhamisha domain
 • Hakikisha domain yako haijapita muda wake (expired)
 • Unatakiwa uwe na uwezo wa kupata funguo za uhamishaji (transfer keys)

Utaratibu wa kuhamisha Domain (Domain name transfer)

Utaratibu huu unafanana sana, iwe ni .com au .tz, awali ya yote, unatakiwa kuwasiliana na msajili wako wa sasa, nao wataanzisha mchakato kwa kukutumia namba ya siri. Utaratibu huu hutofautiana kutoka msajili mmoja hadi mwingine.

Baada ya kupata funguo, basi utawasiliana na msajili wako mpya na kuanzisha mchakato wa kuhamia kwake. Mchakato huu hutumia siku chache, hadi siku tano kulingana na msajili. Kumbuka kuwa, utatakiwa kupitisha maombi ya uhamaji, uhakiki huu hutakiwa kufanywa na mmiliki wa sasa wa domain.

Name Servers

Name server ni seva zinazotumika kufanya utafsiri wa makazi ya Website yako. Name server inawezesha kutambua makazi ya website au email.

Kubadili Name Server
Ni kitendo cha kubadili name server kwenda mahali ambapo utapenda kumanage domain yako. mara nyingi name servers zinaonekana kwenye mtindo kama;

ns1.dudumizi.net

ns2.dudumizi.net

Kubadili Name severs, unatakiwa ama kufanya mwenyewe kupitia upande wa mtumiaji au kuwasiliana na msajili.Kumbuka, unapobadili name sever, mara nyingi hutumia muda mpaka ianze kufanya kazi kwenda kwenye name server mpya.

 

Ukomo wa mkataba wa Domain

Kulingana na sheria na kanuni za umiliki wa domain kama ilivyoanishwa na Taasisi ya Majina ya Website Duniani (Internet Assigned Numbers Authority) endapo baada ya mwaka kuisha mmiliki wa Domain Name atakuwa hajarenew mkataba wa umiliki wa domain, basi domain yako itaingia katika mchakati wa kufutwa. Mchakato huu hupitia hatua zifuatazo;

 • Ndani ya mwezi wa kwanza, domain huondolewa kabisa katika orodha ya muunganisho wa domain (NS Records).

Kama utataka kurenew domain katika kipindi hiki, basi utalipia gharama za kawaida z domain na domain yako itarudi kama kawaida.

 • Baada ya mwezi kupita, domain inaingia katika kipindi cha kufutwa

Domain ikishaingia katika kipindi hiki, gharama ya kuirudisha huwa ghali kwa sababu huambatana na gharama ya kuiondoa kwenye kufutwa. Gharama hutofautiana kutoka kwa msajili mmoja hadi mwingine ila mara nyingi ni mara mbili ya gharama halisi ya domain.

 • Baada ya miezi miwili kupita, Domain hufutwa na mtu yoyoe anayeza kuisajili

Hadi hapa, unakuwa umeshapoteza umiliki wa domain yako. Ingawa mtu yoyote anaweza kuisajili, ila uzoefu unaonesha, inakuwa ngumu sana kuipata tena domain haswa kama ilikuwa na traffic nzui. Hii ni kwa sababu kuna watu wengi wametengeneza mitambo yenye kazi ya kutafuta domain kama hizi (zilizofutwa ila zila watembeleaji wengi) na kuzisajili kwa majina yao hivyo kupata watembeleaji wako watakaopotelea huko.

Athari yake ni kubwa kibiashara, hivyo hata kama umeamua kusimamisha biashara, inashauriwa ukaendelea kushikiria domain name yako mpaka siku utakaporudi tena.

Ni matumaini makala hii itakuwa imekusaidi kujua utofauti kati ya name server na domain, n,a ni muda gani unatakiwa kuhamisha domain. Pia tumeona umuhimu wa kuendelea kushikilia umiliki wa domain hata kama umesitisha biashara. Kama unataka kuendelea kushikilia Domain yako, usisite kuwasiliana nasi.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now