Kwa siku nyingi nimekuwa nikitaka kuandika makala inayohusiana na mambo muhimu ya kuzingatia unapotafuta mtu au kampunni ya Hosting kwa Website hapa Tanzania. Ila, kitu kikubwa kilinichonisukuma kuandika makala hii, ni jana nilipokea simu kutoka kwa mtu wangu wa karibu akinilalamikia kuwa kijana waliomtumia kuhost website yao ameshindwa kuendelea kulipia huko alipokuwa anahost na hivyo kupelekea kufungiwa huduma na website zote zilizopo chini yake kufungwa. Alikuwa amechanganykiwa sana, ila sikuwa na jambo la kumsaidia zaidi ya kumpa pole na kumkumbuka kusiwepo na next time.

Unapochagua sehemu ya hosting ya website au wapi kwa kununua jina la webste (Domain name) unatakiwa uwe makini sana, kwa sababu, tatizo lolote linaweza kukusababisha upotee kwenye mtandao na usipatikane tena. Unapotafakari wapi kwa kuhost Website, kuna mambo mengi ya kuzingatia, ni zaidi ya gharama, wengi wamekuwa wahanga kwakuwa wanafikiria gharama pekee na kuacha mambo mengine hivyo huwapelekea kujuta siku za usoni.

Kwa wengi wetu, unapofanya Website Hosting, ndipo kutakapokuwa na email zako, na ni emal hizo ndizo chombo rasmi za mawasiliano, hivyo, kutokuwa online, kuna maumivu makubwa kwenye biashara yako.

Sasa, ili kuwasaidia wanajamii wa Kitanzania ambao wameonesha ari ya matumizi ya mtandao, hebu tuangalie vitu vya msingi vya kuzingatia unapochagua Website Hosting.

1. Zingatia upatikanaji na utengamaaji wa huduma (Availability & Stabiliy)

Linapokuja suala la Website, email au application yoyote, upatikanaji ndiyo kila kitu. Kabla haujaamua wapi kwa kuhost Website yako, kitu cha kwanza kabisa, hakikisha unaijaribu Website ya wahusika je wanapatikana kwa spidi nzuri na muda wote ipo imetengemaa. Hakuna watu wasio na uvumilivu kama watumiaji wa mtandao, wengi hawapendi kusubiri, hivyo zingatia kuwa sehemu unayohost ipo imara na wana spidi nzuri.

Waulize wakupatie website portfolio, angalau tano wanaozihost za aina tofauti na kwa wakati tofauti uzijaribu, wakati wa kazi, wakati wa usiku mnene na wakati wa weekend. Hii itakupa picha halisi ya mazingira ambayo website yako itakuwa ikiishi.

2. Tabia ya huduma ya mtoa huduma ni kitu muhimu

Kuhost website, kwa wengi ni kama nyumba ya kupanga, je ushawahi kuishi kwenye nyumba ambapo mitaro ikiziba baba mwenye nyumba hapatikani hadi baada ya wiki? Hili ni sawa na kwenye Website Hosting, hakikisha unajiridhisha na tabia ya mtoa huduma kwa wateja. Pata uwiano wa wateja anaowahost na muda anakaa nao (Retention rate).

Kwakuwa inawezekana kukawa na vitu muhimu kwenye Website yako, hivyo hakikisha unapata profile ya wateeja wake ili kupata muelekeo au jamii unayoingia kwa sababu na wewe utakuwa ni miongoni mwao. Pia, jiridhishe ni kwa jinsi gani wanawasaidia na kuwawezesha wateja pindi wanapokuwa na matatizo. Unaweza jaribu kuwaandikia email ili ujue ni kwa muda gani wanachukua hadi wakujibu. Tanzania tuna tatizo kubwa kwenye idara ya huduma kwa wateja, hivyo safiri na watu makini.

Service Desk Manager was Dudumizi akiwa kazini

3. Uhai wa kampuni kwenye biashara

Kama nilivyodokeza hapo juu, hosting ni kama nyumba, inashauriwa sana ukafanya biashara na mtu au kampuni ambayo ipo kwenye biashara kwa miaka kadhaa. Hii itakuhakikisshia uzoefu walio nao kwenye kuhudumia wateja na kukabiliana na matatizo. Pia, itakuonesha stability ya kampuni au mtu. Watu wengi wamekuwa wakiingia kwenye bashara kimajaribio, hivyo, na wewe usingependa uwe sehemu ya majaribio. Maana baada ya majaribio kufeli utakuwa nje ya mtandao.

4. Hakikisha unachunguza muenendo wa kampuni

Linapokuja suala la kutoa huduma, si kampuni zote zitakuwa na huduma sawa, ila pendelea kuhost Website na kampuni bora zaidi, tena iliyojipatia sifa nzuri kwenye industry hiyo, Google inaweza kukusaidia kwenye hili. Jaribu kufanya google search, kama Website Hosting Companies in Tanzania, au kuandika jina la kampuni kwenye Google mfano Dudumizi na ukapata kujua muenendo wao na jinsi gani watu wanavyowaongelea. Pia, hakikisha unapitia mitandao jamii ya kampuni ili kujua tabia na muenendo wao, mitandao jamii itakuwezesha pia kujua ni kwa jinsi gani wapo active kwenye biashara.

Makampuni yote makini ya mtandao ni lazima yawe active kwenye mitandao jamii, kwa sababu hayo ndiyo maisha yao, hivyo ni lazima waamini na waishi kwenye wanachokiamini.

5. Kampuni ni bora kuliko mtu, na kama utaamua mtu, basi epuka kabisa mtu anayefanya kama part time

Kama utaniuliza je kati ya kampunni nisiyo ifahamu na rafiki yangu anayefanya hosting kipi ni bora, nitakuambia kampuni ni bora. Kadri uwezavyo hakikisha unafanya kazi na kampuni kuliko mtu, na epuka kampuni zinazofanya kazi kama mtu.

Kati ya wateja wengi sana wanaokuja kwetu Dudumizi ili kupata msaada juu ya kupoteza Website zao kutokana na kupotea kwa wahusika, angalau 70% wamefanya kazi na watu, 20% wamefanya kazi na makampuni yanayoendashwa na mtu na 10% ndiyo makampuni rasmi. Hivyo siku zote pendelea sana kufanya kazi na kampuni, faida ni nyingi ikiwemo ubora wa huduma, na usalama wa taarifa zao kwa sababu unapofanya kazi na mtu, risk zote amebeba mtu, akiumwa Website yako imeumwa, akifariki Website yako nayo imefariki na akifirisika Website yako nayo imefirisika. Risk hizi ni ndogo kunapokuja kampuni inayofanya kazi kama kampuni.

Pia, wakati unachagua kampuni, hakikisha Hosting ni moja kati ya huduma zake kuu. Siku zote, kama ni huduma kuu, basi watawekeza kwenye huduma hii na kukufanya upata huduma bora.

Orodha ya makampuni kumi bora kwenye kusajili Domain (.tz Domain name registrars)

6. Hakikisha kuna nafasi ya kuhama

Unapofanya Hosting, mwanzoni kuna uwezekano usiwe na vitu vingi ila vikakua jinsi siku zinavyosonga, je plan yako inakuwezesha kuhama bila kufanya setup nyingine zozote, na ni jinsi gani taratibu za malipo. Chukulia mfano umehost kwa miezi miwili halafu space imejaa, je utahitaji kulipia gharama upya au unaweza kubeba kiasi kilichobaki.

7. Jua utofauti kati ya Bandwidth na Disk space na vikomo vyake

Kabla haujaamua kuhost, hakikisha unajua vikomo vya Bandwidth na Disk space. Bandwidth ni kiasi cha ujazo wa taarifa zinazoweza kupita wakati disk space ni ujazo wa taarifa zinazoweza kukaa. Bandwidth mara nyingi huwa kubwa, kwa mfano kurasa ya mbele (homepage) ya website yako ina ujazo wa 3MB, na kila mwezi inatembelewa na watu 500, hivyo kwa mwezi utatumia bandwidth ya 500 X 1 = 1500MB, bandwidth inakokotolewa kwa kila kurasa anayotembelea. Ingawa kwa matumizi ya kawaida na kama Website yako haijavamiwa, ni ngumu sana kupitiliza.

8. Usalama ni kila kitu.

Usalama wa mtandao ni moja kitu cha lazima kukizingatia. Usalama wowote wa mtandao huanzia kwenye miundombonu, application na mengineyo. Hivyo hakikisha unafanya hosting kwenye kampuni ambayo haina historia ya kuvamiwa.

Moja ya makampuni yanayofanya hosting Tanzania na yaliyo kwenye orodha chafu

Kabla ya kuhost, hakikisha website yao ipo safi kwa kwenda https://mxtoolbox.com/blacklists.aspx kwa kuweka domain ya kampuni, hapa utaweza kupata taarifa juu ya usafi wa Domain au IP kama inavyoonekana huko nje. Kama Website yako ikiwa imeoorodheshwa, basi kuna uwezekano mkubwa kuwa Hosting ina matatizo na hii itakuathiri sana haswaa upatikanaji wa email.

Ni mara ngapi watu wamekuwa wakilalamika kutokupata email kutoka kwako, au ni mara ngapi email unazotuma zimekuwa hazifiki kwa wahusika? Basi, tatizo kuu ni hili, IP ya sehemu unayohost imeorodheshwa kwenye orodha ya mitandao isiyo misafi. Hivyo, mitandao mingine mingi itakuwa inazuia kupokea email kutoka kwako.


Kama unahitaji msada au ushauri kwenye huduma za hosting tuandikie info at dudumizi.com au tupigie 0768 816728 au Tembelea www.dudumizi.net

Call us now