Kwenye nchi nyingi, wanafunzi wa chuo ni moja kati ya makundi yaliyo active katika kufanya kazi, na mapinduzi mengi ya uchumi hutegemea kundi hili, kwani wana nguvu na uwezo mpana. Kazi nyingi za vipindi (part time) huwa zinafanywa na kundi hili. Hii siyo tu inawasaidia kuongeza kipato, bali inawafanya wawe na ubongo ulio active haswa kwenye sehemu ya pili ya maisha, maisha halisi.

Kinyume na hiki, tunakuwa tunatengeneza kundi kubwa la vijana wasomi lakini wanakuwa wamedumaa kwenye kujishugulisha. Na, ni moja ya sababu bumu linapochelewa, inakuwa shida kubwa na maandamano yasiyoisha.

Hali hii, huwa inaathiri sana sekta binafsi pale unapomuajiri mwanachuo moja kwa moja kutoka chuoni, kwani kunakuwa na kazi mbili kwa pamoja, kumbabidili kutoka mwanafunzi kuwa mfanyakazi (huku ukipambana na uhalisia vs ndoto) and kumfundisha kazi kitu ambacho kwenye Uchumi wa viwanda italeta shida, na ni moja ya sababu waajiri wengi hukimbilia kuajiri raia wa kigeni kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.

Kuna sababu nyingi kwenye hili na kila upande anaongea lake, Upande wa wanachuo wanasema, Wakufunzi wanabana sana hivyo unashindwa hata muda wa kusoma, na upande wa wakufunzi wanajitete kuwa wanafunzi ni goigoi wanapenda mambo rahisi hivyo hawajishugulishi kutwa kuchinda kwenye mitandao jamii, ukiwaachia huru utavuna mabua.

Binafsi, ninaona matatizo sekta zote, Na huu si muda wa kumtafuta mchawi kwani athari yake ni athari ya Taifa letu sote haswa wakati huu tunapoendea uchumi wa kati na wa viwanda. Lets just fix it, it has broken!

1. Mitaala iwekwe kwenye mtindo ambao mwanafunzi atakuwa na muda wa kufanya mambo mengine huku akipata ujuzi.

Nakumbuka kipindi nasoma degree ya kwanza, kuna semester tulikuwa hadi na kozi 14 ukijumlisha michezo (Sports) na masomo ya kuchagua (Optional courses), ila ratiba zilikuwa very flexible na kozi zilipishana vyema huku kukiwa na mpangilio mzuri wa kuziendea hivyo nilipata muda mwingi wa kujifunza mambo mengi na huku tukijishughulisha na kazi nje ya chuo.

Wakati ninasoma shahada ya pili, tulisoma miaka mitatu badala ya miwili (utaratibu wa China isipokuwa kwa wanaosoma kingereza) ili kila mwanafunzi atumie mwaka mzima kwenye kuongoza project, ama za chuo, ama ukaajiliwe ama ukajitolee, na matokeo ya hili ndiyo yatakayokuwezesha kuanza kuandika Masters Thesis, na moja ya matokeo ya hili ni kuzaliwa rasmi kwa Dudumizi. Nilikuja na idea ya kuanzisha kampuni ili nitumie muda wa kujifunza kwenye kampuni iliyo chini yangu.

2. Waajiri wengi huajiri kwa tabia (Attitude) na si utendaji kazi pekee.

Wanafunzi wajue, waajiri wengi wanapenda watu wenye uwezo wa kitaaluma na upeo mkubwa wa maisha aka mtaani.com, na wanapenda kuona kwa kupitia chuo, umebadilishwa kutoka mwanafunzi na sasa ni mwanachuo aliye tayari kuwa mfanyakazi, hivyo kubakia kwenye uanafunzi ni mzigo kwako.

Tunaenda kwenye uchumi wa viwanda, na wanachuo ndiyo tegemezi kubwa ili tusimuangushe Rais wetu, tufanye kazi. Nchi kama China imefanikiwa sana kwa kuwatumia vijana wa vyuo hivyo kufanya soko lao kuwa lenye kuvutia.

Katika kuhakikisha nasi tunafanya kivitendo, ili tusiwe waongeaji bali tuisaidie nchi kivitendo, kabla hatujafika hatua kubwa ya kubadilisha mitaala na mengineyo, tumeona tuje na program itkayowasaidia wanafunzi kuanza kujifunza juu ya ushiriki kwenye biashara na kazi. Programu hii tunaiita Michongo Affiliate.

Michongo Affiliate ni program inayokuwezesha kupata kipato kwa kila mauzo yaliyotokana na wewe. Unachotakiwa ni kuwa na uwezo wa kutafuta wateja watakaonunua kupitia program au website ya Michongo na wewe utalipwa commission.

Application au Website inakuwezesha kuona maendeleo ya link ulizoshare, kiasi cha commission ulichopata na pia kuomba malipo moja kwa moja.

Ili kujua mengi kuhusu Michongo Affiliate inavyofanya kazi Download Michongo App kwenye Google Play Michongo App au unaweza kutembelea  Michongo Affiliate

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now