Ni kitu cha kawaida kwa wafanya biashara wengi kutumia email zao binafsi kwa matumiziya kiofisi. Kwa Tanzania, si kitu cha ajabu ukaona tangazo kwenye mitandao halafu mtu akaandika wasiliana nami kwa kutumia This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

Wengi wao hawafahamu ni jinsi gani matumizi ya email binafsi zinavyowapunguzi uaminifu kwao. Je unataka kujua kwanini matumizi ya email ni kitu cha msingi na jinsi gani unaweza kuongeza uaminifu kwenye biashara yako? Endelea kusoma makala hii.


Ni zaidi ya Email

Ni kitu kigumu sana kumshawishi mteja anunua bidhaa au huduma yako, ukizingatia katika hali ya uchumi wa sasa wa kubana matumizi, kila mtu anajitahidi asifanye makosa kwenye manunuzi, hivyo kuaminika ni kitu muhimu. Uaminifu huu hujengwa na vitu vingi, kama taswira uliyoijenga sokoni, mitazamo ya wateja, jinsi unavyowasiliana nao na pia njia za mawasiliano na wateja, email ikiwemo moja wapo.

Watena wana njia mbalimbali za kujenga uaminifu na taswira bora ya kampuni. Email ya kampuni ni moja ya nyenzo za ujenzi wa taswira bora.

Email ni njia mojawapo ya kukutangaza

Kwa kutumia Email ya biashara, ni dhahiri utaweza kuwafikia watu wengi zaidi, mfano, mtu anapoona email kama This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it., ni dhahiri atataka kujua ni nini Dudumizi.com. Hivyo atakwenda kutembelea Website na pengine atakuwa mteja wako ajaye.

Mitazamo ya watu kulingana na Email unayotumia

Hata kama utaamua kuwa na Email yenye jina zuri kabisa, baadhi ya watu wanaweza kukuweka katika kundi lisilo kulingana na historia ya hizo email. Kwa mfano, tumeona siku za karibuni, yahoo wakivamiwa na akaunti nyingi kuwekwa hadharani. Hivyo, kwakutumia akaunti ya Yahoo, unaweza kumkimbiza mteja akaona kuwa hayupo salama.

Nini cha kufanya?

Watu wengi bado wanadhani hauwezi kuwa na email kama hauna Website. Hili si la kweli, unaweza kuwa na email ya kampuni hata kama hauna Website. Kwa mfano Dudumizi tunayo Package ya Email za Biashara (Business Emails) ambayo inakuwezesha kupata Email kwa 60,000TZS na Domain ya bure kwa mwaka mzima. Hii inawawezesha wafanya biashara kumiliki hadi email kumi kwa gharama nafuu kabisa.

Eemail za biashara hukuwezesha kuongeza uaminifu kwa wateja, pia kukupa njia rahisi ya kujitangaza zaidi na zaidi. Hivyo anza kuzitumia ipasavyo

Call us now