Tunayofuraha kuwataarifu wana Dudumizi na jamii kwa ujumla kuwa, baada ya kukaa jikoni kwa muda mrefu, tunatarajia kuzindua programu yetu ya mauzo, inayojulikana kama Michongo App.  Application hii ya Michongo inakuwezesha kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye punguzo.

 Michongo inajitofautisha na programu nyingi za mauzo ya online kwa sababu kuu zifuatao;

1. Michongo inauza bidhaakwa bei ambayo hauwezi kuipata sokoni. Inamaana, Michongo imeshabageni bei kwa ajili yako.

2. Michongo inatumia programu rafiki ya Affiliate kuwezesha watu kuingiza kipato kwa kila linki wanayosambaza kwa marafiki zao na rafiki akanunua bidhaa. Hii inamaanisha, Michongo ni agent wa timu ya sales itakayokufanyia kazi. Kwa mtindo huu, unaweza kupunguza gharama za kutangaza biashara yako hadi nusu kwa sababu hakuna gharama yoyote kwa kutangaza kwenye Michongo, pia kuna mamilioni ya watu watakuwa busy kusambaza link za bidhaa yako. Hii itawawezesha wajasiriamali wadogo wengi kuingia sokoni na kutengeneza ajira zaidi na zaidi, kama malengo ya Rais wetu (kuongeza ajira).

3. Michongo inakuwezesha kupata huduma kwa kutumia namba za kuponi. Hii inamaana, unaepuka kutembea na pesa (usalama) na malipo yote yanaishia kwenye Michongo na kukupa namba ya siri utakayoonesha kwa muuzaji.

4. Michongo inahusisha Bidhaa na Huduma. Programu nyingi zimejikita kwenye bidhaa pekee huku zikisahau Huduma. Michongo tumekufikia.

5. Michongo inakuwezesha kupata bidhaa zilizo karibu nawe zaidi kwa kutumia simu ya mkononi. Chukulia upo katikati ya mji na unataka kutafuta sehemu yenye punguzo la chakula ukapate chakula cha mchana. Utapata kwenye Michongo App. 

Katika uzinduzi huu, Michongo inaandaa tamasha la mauzo ambapo wafanya biashara watapata kuuza moja kwa moja bizaa na wateja kununua. Tamasha hili linaitwa Michongo festival . Michongo festival ni tamasha la aina yake kuwahi kutokea Tanzania ambapo wauzaji wataweza kuuza moja kwa moja, pia watapata nafasi ya kujua zaidi kuhusu michongo, kwakweli si la kukosa. Tamsaha hili litafanyika Oktoba 29, Mlimani City

Idea hii ya Michongo ilianzia nchini China ambapo muanzilishi wa Dudumizi Mr Nyoni aliliwasilisha wazo la Michongo kwenye kongamano la wana electronics Duniani lililohudhuriwa na magwiji kutoka kampuni makubwa ya teknolojia Duniani, kama Intel, IBM, Microsoft na mengine mengi. Katika kongamano hilo Mr Nyoni alialikwa kama mtoa mada mkuu (Keynote Speaker) ambapo aliweza kuliwasilisha wazo la Michongo na jinsi gani litasaidia kukuza biashara kwa nchi zinazoendelea haswaa kwenye dunia ya leo ya mitandao, baada ya miaka mitano, leo hii anatimiza wazo hili.

Wazo kamili la Michongo ni kuweza kufikisha huduma au bidhaa kwa uharaka, kwa watu wengi na bei nafuu, huku ukimsogezea mnunuzi bidhaa karibu na pia zilizo na machaguo yake. Mnunuzi anapata bidhaa zilizomlenga na zinazomfaa (selected) na zilizomzunguka (nearby) huku tukiongeza ushinani kwa watoa huduma. Michongo inalenga kuwapa sauti wanunuzi na kuwapa nafasi ya kuwashawishi wengine zaidi kununua bidhaa/huduma.

Kupakua Application ya Michongo toleo la Android unaweza kutembelea https://play.google.com/store/apps/details?id=com.dudumizi.michongo.user

 

Call us now