Faida kuu 5 za kutumia .tz domain kwenye biashara
Ingawa wapo watu wenye shauku ya kumiliki domain ya .co.tz lakini, kuna maswali au utata unaozunguka kichwani, hivyo, makala hii itasaidia kutatua maswali yanayoweza kujitokeza kuhusu .tz domain.
1. Je nitahitaji .tz pamoja na .com
Jibu la swali hili ni NDIYO au HAPANA, .tz ndiyo mpango mzima. Haijalishi unafanya biashara Tanzania pekee au dunia nzima, .tz itakufikisha huko na inatosha kabisa. Kumbuka, haijalishi unatumia kikoa cha .tz au .com, zote zitapatikanika dunia nzima. Tofauti tu, kwa kutumia .tz mtu anaweza kujua moja kwa moja hii ipo Tanzania bila hata kwenda kwenye mawasiliano.
Kuna woga au dhana ambayo ipo kwa wengi wetu ya kuhofia matumizi ya .co.tz inayopelekea kuamini kama .com ndiyo inayojulikana na watu. Google imeboresha sana upatikanaji wa Website bila kuathiriwa na kikoa.
2. .tz inakuwezesha kurudisha domain iliyopotea
Ni mara ngapi imeshatokea umepoteza mawasiliano na mtu aliyekutengenezea Website au kukusajilia domain (kwa wale wanaotumia watu binafsi), au ni mara ngapi mumeshindwa kufikia maelewano na mtu aliyekukusajilia domain na kupelekea kutaka kuifungia domain hiyo?
Kwakuwa usimamizi wa .tz unafanyika Tanzania moja kwa moja, hivyo, endapo kutatokea tatizo lolote na mtu aliyekusajilia domain mukashindwa kuwa na mawasiliano, kama unatumia .tz domain, taasisi ya tzNIC itakuwezesha kurudisha domain hiyo punde tuu utakapowasilisha taarifu za uhakikiwa umiliki wake.
3. .tz inakuwakilisha Kitanzania Zaidi
Mtembeleaji wa wavuti anapoona kikoo cha .tz, basi moja kwa moja anajua kuna mahusiano na Tanzania. Hivyo, hii hupelekea kuwa na imani na utulivu kwakuwa wateja wengi hupenda kufanya kazi na kampuni zilizo karibu nao.
Kwa mfano, makampuni ya kitalii, hii ni moja ya nyenzo muhimu sana kwenye kujitangaza, kwani watalii wanapenda kufanya kazi na mtu aliye karibu na eneo husika, .tz ni kiashiria tosha.
Ndiyo maana, hata Google wameamua kutumia Google.co.tz ambayo inawalenga watu wa Tanzania.
4. Uwanja mpana wa kuchagua
Ni mara ngapi umeona website imeongezewa tz mbele ya jina, mfano dudumizitz.com au michongotz.com kwakuwa majina ya kwanza yameshachukuliwa na muhusika anapenda tuu kutumia .com. Kwanini usingefikiria kutumia majina kama dudumizi.co.tz badala ya dudumizitz.com?
Kwa, kutumia .tz, unao uwanja mpana wa machaguzi kwakuwa majina mengi sana bado hayajachukuliwa.
5. Uzalendo
Ndiyo, kwa kutumia vikoa vya .tz, tunasaidia kutangaza nchi yetu, watu wanapoona domain za .tz inawasaidia kuikumbuka Tanzania na kufika mbali zaidi.
Unayo kila sababu ya kusajili .tz domain, kumbuka pia kusajili domain kutoka kwa makampuni yenye uhakika ili kuepuka kupoteza uhalali wa umiliki wake. Gharama za kusajili domain za .tz ni 25000 tu. Hivyo, sajili Domain yako Hapa.