Siku ya Jumatano, Februari 24, 2015, timu ya Dudumizi ikiwa kama mmoja wa wana kikundi, ilipata nafasi kuhudhuria ufunguzi rasmi wa kikundi cha wafanyabiashara (BNI - Business Networkng and Referrals) tawi la Amani. Ufunguzi  ulianza saa kumi na mbili na nusu hadi saa tatu asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Ramada.

 Uzinduzi huo, ulienda sambamba na utambulisho wa makampuni kutoka kwa wana Amani pamoja na mafundisho ya kibiashara yaliyowezeshwa na Mr Vishal kutoka BNI Dubai.

BNI inasimama katika falsafa ya Givers Gain, ikijikita katika kupena nafasi kibishara (Referrals). Ndani ya BNI, kila biashara hupata nafasi ya kunadi biashara pia kuomba nafasi ya kuunganishwa na watu husika. Hii inamaana, wana BNI husaidiana kibiashara, kama wewe ni mfanya biashara, huwezi ikosa nafasi hii adimu. Washiriki wa BNI hukutana mara moja kwa wiki kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi hadi saa mbili asubuhi, huu ni wakati mahsusi kupanga mikakati ya kibiashara.

 Kwa Tanzania, kuna matawi mawili ya BNI, moja ni Hodari na lingine ni Amani ambayo yote yapo Dar es Salaam. Hivyo kama wewe ni mfanya biashara na ungependa kujiunga na kikundi cha wafanyabiashara kupitia BNI, fanya haraka kabla nafasi haijachukuliwa kwa sababu, kwa BNI, ni biashara moja tuu inayokubaliwa kwa kila kundi.

Wafanyabiashara wakibadilishana taarifa kabla ya kuanza kwa kikao (Business Networking)

Washiriki wakifuatilia utambulisho wa wana BNI wa Amani

Wafanyabishara wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Ramada

Uchukuaji wa picha ukiendelea kabla ya kuanza kwa tukio la awamu ya pili

Sehemu ya washiriki wa tukio

Nguzo kubwa ya ushirikiano wa kibiashara huanza na uelewa thabiti wa biashara ya mwenzako. Wana BNI wakibadilishana mawazo.

Logo ya Dudumizi ndani ya BNI

 

Call us now