Moja ya vitu ambayo wengi wetu tumekuwa tukidhani ni kuwa, Website ikishatengenezwa, basi itaishi milele bila kufanyiwa mabadiliko yoyote ya kimfumo. Katika dunia ya leo, Website ni moja kati ya nyenzo thabiti kwa biashara. Hivyo, taarifa, muundo na hata sababu ya kuwa na Website inatakiwa iwe inaangaliwa na kuboreshwa kwa wakati.

Kwa mfano, kwa miaka ya hivi karibuni, tumeona jinsi matumizi ya simu za mkononi yalivyoongezeka, hivyo ni lazima ujiulize kama Website yako inao uwezo wa kuwahudumia wateja hawa wanaotumia simu kutembelea Website. Website ni lazima iende sambamba na mabadiliko hayo. Kitu cha kuzingatia ni kuwa, si lazima ubadili muonekano wa Website ili iweze kuendana na matakwa hayo.

 

Hebu tuangalie kwanini Website ni muhimu kwa biashara yako;

 1. Asilimia kubwa ya manunuzi huanzia Online.

Hebu jiulize, mara zote unapohitaji huduma yoyote, ni nini kitu cha kwanza kufanya? kumpigia simu rafiki au kwenda online, iwe facebook, Instagram au Google na kutafuta huduma? Ingawa ni kweli mitandao Jamii inaweza kuwa ni chanzo cha kukufikia, ila Wateja wengi huhitaji taarifa zaidi kabla ya kuamua kununua bidhaa yako. Website, ina uwezo mkubwa wa kufikisha taarifa hizi. Kama bado hauna Website, basi tambua unapoteza wateja wengi makini kila siku.

2. Wateja wengi wanatumia simu online kuliko Kompyuta

Kama ulikuwa bado haufahamu, ukweli ni kuwa, ongezeko la watumiaji wa internet kupitia simu limeongezeka kwa 400% kuanzia mwaka 2013, na namba zimekuwa kubwa zaidi miaka ya karibuni. Je, website yako ipo rafiki na simu (responsive website)? Kama haipo, basi jua wazi kuwa unapoteza wateja wengi sana siku hadi siku. Hivyo unatakiwa kufikiria kuiboresha Website.

3. Wateja wana nguvu sasa

Je umewahi kujiuliza jinsi wateja wanavyotumia mitandao jamii kupata taarifa za biashara yako kabla ya kuamua kujiunga? Je unatumia mitandao jamii kwa ajili ya biashara? Na ni moja ya mpango mkakati wa watumizi ya mitandao kwa biashara yako? Kama bado, basi unatakiwa kuanza kulifanyia kazi leo.

4. Wateja wanaiamini Google

Je umewahi kujiuliza pindi unapotafuta huduma yoyote Google, kitu gani kinakuzuia usiende page ya pili? Jibu ni moja, unaiamini Google na umeipa nafasi ya kukuchagulia nani bora hivyo huishia kurasa ya kwanza.

Matokeo ya utafutaji, Dudumizi ipo namba 1


Kitendo cha kuboresha Website yako ili iwe na matokeo ora kwenye mitambo ya utafutaji (Search Engine) kinaitwa Search Engine Optimization (SEO), hivyo hakikisha Website yako ni rafiki wa Google. Kuliacha hili ni sawa na kufanya biashara bila kuwa na anuani wala njia rahisi ya kufikika na wateja.

6. Watu wanahitaji muongozo

Watembeleaji wanapokuja kwenye Website yako, haimaanishi watakuwa wateja. Unahitaji kuwaongoza na kuwapa sababu ya kuwa wateja. Mfano, Website lazima iwe na njia rahisi za kuwasiliana nawe, njia rahisi ya kupata quotation, njia rahisi ya kuona kazi zilizopita na maono ya wateja wako wa sasa. Mfano, katika moja ya maboresho katika Website yetu ya Dudumizi ni kuhakikisha mteja anayetumia simu ana uwezo wa kutupigia simu moja kwa moja kwenye simu yake kutokea kwenye Website.

muonekano mpya wa Dudumizi kwenye simu za mkononi

Kwa kuwa na taarifa hizi, kutakusaidia kuwapa mvuto wa kuwa wateja bila hofu yoyote. Kumbuka wateja hawataji usumbufu kwakuwa wao ni wafalme wako.

6. Website ni mfanyakazi bora, anafanya kazi 24/7/365

Je umeshawaji kujiuliza ni jinsi gani Website inavyokuletea Wateja? Hata wakati ambao wafanyakazi wengine wote wamelala, Website ipo hewani inafanya kazi, dha, kweli huyu mfanyakazi bora.

Wengi wetu tumekuwa na mipango mingi sana juu ya namna ya kuboresha na kuongeza ufanisi wa wafanyakazi. Je umeshawahi kujiuliza ni kiasi gani umewekeza kwa mfanyakazi Website? Huyu ni mfanyakazi bora asiyechoka, hivyo anahitaji uwekezaji bila kusita.

Hakikisha mfanyakazi Website ana kiwango na ubora wa juu kabisa kwakuwa huyu ndiye mfana kazi bora.

7. Website ni taarifa

Wateja wanapokuja kwenye Website yako, hawaji kuona picha zenu, wala hawaji kuona matukio muliyofanya au uongozi wa kampuni yako. Wanakuja kupata taarifa. Hivyo basi, hakikisha Website yako ina taarifa zote muhimu ambazo zitamsaidia mteja kufanya maamuzi.

Taarifa siyo tu itamsaidia mteja, pia, zitasaidia kuifanya Website yako iwe na nafasi ya juu kwenye mitambo ya utafutaji (SEO). Kumbuka, taarifa ni mfalme wa Website (Content is King)

8. Website haikuhusu, ni ya Wateja

Unaweza anza kutishika inakuwaje isinihusu? Unapotengeneza Website, kumbuka kuwa, hakuna mteja atakayekusifia kwakuwa Website ina mambo au imetenegnezwa kwa kutumia Teknolojia ya juu. Bali, watakusifia kama Website ina taarifa wanazozitaka kukamilisha mahitaji ya biashara yao. Sisi huwa tunasema, IT haijalishi (IT Doesnt Matter), kinachojalisha ni jinsi gani itaweza enda sambamba na mahitaji husika.

Tengeneza Website kwa ajili ya Wateja, si kwa ajili yako.

Hivyo basi, hakikisha Website ni sehemu ya biashara. Website ni mfanyakazi bora ambaye hana mgomo wala kuchelewa kazini kama utamuwezesha. kwenye kazi zetu, Dudumizi husema, tunakutengenezea biashara, siyo Website.

Kama unahitaji kutengenezewa Website au ushauri juu ya namna ya kuboresha Website yako, wasiliana nasi kwa kwenda Hapa.

 

Call us now