Katika sehemu ya kwanza ya jinsi ya kupima mafanikio ya Website, tumeangalia dhumuni la upimaji wa mafanikio, pia tumeangalia vitu muhimu vya kuzingatia. Tumeona umuhimu wa kuwa na malengo yenye sifa kuu tano au kwa kifupi (SMART).

Katika sehemu hii ya pili, tutaangalia vizio muhimu vya upimaji wa mafanikio ya Website.

Kama tunavyojua, dhumuni la kuwa na website ni ili iweze kutumika kwa watu, wawe wateja, wafanyakazi au hata washirika. Kwa kujua takwimu za matumizi ya watu hawa, ni dhahiri utaweza kujua ufanisi wa Website yako. Vizio hivi vya
uchambuzi vitakuwezesha kupata picha kamili ya ni jinsi watu wanafika vipi kwenye website yako, wakifika wanatembelea kurasa gani, wanakaa muda gani nk. Google analytics ni moja ya website ambazo zinaweza kukusaidia kupata takwimu hizi.

Hebu, tuangalie vizio hivi;

 

1. Uwiano wa matumizi (Conversation Rate)

Kizio hiki kinakuwezesha kujua jisni gani watu wanaitumia website yako, kwa haraka tunaweza kusema je website yako inatumika? Kizio hiki hutolewa kwa kulinganisha asilimia ambayo watumiaji waliotembelea website na kutimka na wale waliokuja na kuitumia.

Kwakujua uwiano huu, itasaidia kujua muono wa watembeleaji wa website na kujifanyia tathmini wewe mwenyewe.

2. Kurasa walizoondokea (Exit Page)

Chukulia mfano unaenda kwenye duka linalouza vitu vya watoto, basi baada ya kufanya shopping ya kutwa nzima, watoto watamalizia sehemu ya Ice cream ambayo atanunua na kushika mkononi ambayo atakuwa anakula huku anaenda nyumbani.

Hii ni sawa na kwenye website, kurasa za kutokea inamaanisha, ni kurasa gani ambazo mara nyingi ndizo huwa za mwisho kwa watembeleaji.  Kwa kujua kurasa hizi, itakuwezesha ama kuzitumia kwa kuweka ujumbe unaotaka kuwafikishia wahusika, ama kwa kuweka baadhi ya ofa.

Mfano mzuri ni kwenye supermarket, pale sehemu ya kulipia utaona vitu vidogodogo kama pipi,bazoka nk.

Kwa Tanzania, washika dau wanasema watu ni wavivu kusoma, hivyo wamiliki wengi wa website za habari / blogs wanapenda kuwa na kurasa ndefu yenye kila kitu kwenye kurasa moja. Hivyo, kwa website kama hizi, tegemea kuwa kurasa itakayoongoza ni ile ya kwanza. Na ndiyo maana kila mtu anayetaka kutangaza anataka kuweka matangazo hapo na siku ya mwisho wanajikuta wanajaza matangazo mengi kwenye kurasa hii.

Kwa tafiti tulizozifanya kwenye website ya Mjengwa Blog, ushaidi unaonesha, watu wengi hubonyeza matangazo yaliyo ndani ya makala kuliko yale yaliyo pale juu. Na hii ni kutokana na asili ya website husika. Hivyo, kurasa za walizoondokea hutofautiana kutoka website moja hadi nyingine na ni jukumu lako kama mmiliki kulitambua hilo.


3. Watembeleaji halisi (Unique Visitors)

Kizio hiki kitakuwezesha kujua idadi ya watu waliotembelea website yako kwa siku / muda husika. Watu wengi wamekuwa wakiangalia sana idadi ya kurasa zilizotembelewa. Inawezekana ni mtu mmoja aliyeboreka hivyo akawa anasoma kurasa
nyingi.

Kwa kujua ni watuwangapi wanaotembelea Website yako, itakuwezesha kujipanga. Kwenye hili unaweza pia kujua nchi wanazotoka, vifaa walivyotumia, muda waliokaa kwenye website nk. Pia utaweza kujua wanatoka wapi hadi kufika kwenye website
yako (Referrers). Hivi ni vitumuhimu unavyopaswa kuvitambua kipindi unaandaa mkakati wa kujitanua zaidi.

Chukulia mfano, wewe una website ya habari halafu muda wa watu wanaotumia kwenye website yako ni chini ya dakika mmoja, hii inamaanisha kuwa habari zako hazina mvuto, watu wanaishia kusoma vichwa vya habari na kupotea.

4. Uwiano wa watimkaji (Bounce Rate).

Uwiano wa kutimka inamaanisha watu wanaondoka kupitia kurasa waliojia, yaani mtu baada ya kufungua ile kurasa, anapotea, kwa maneno mengine tunasema kama amepotea njia. Kizio hiki cha uwiano wa kutimka hukuwezesha kupima vitu vingi,siyo
tu utaweza kupima mvuto wa website yako, bali pia unaweza hata kugundua baadhi ya mambo mengine kama ugumu wa ufungukaji wa website.

Kwa kutumia vizio vya watembeleaji halisi, pia utaweza kujua vizio vingine vinavyowahusu kama aina za simu walizotumia, kampuni ya intaneti nk, hivyo kwa kutumia taarifa hizi, unaweza kubaini matatizo ya ufungukaji wa website kwa watu wa sehemu fulani au wanaotumia kifaa fulani. Kwa mfano, inawezekana watembeleaji wa simu wengi wanashindwa kusubiri mpaka website yakoifunguke kwakuwa inatumia muda mwingi hivyo hufunga website yako hata kabla haijamaliza kufunguka. Na hivyo ukahitaji toleo la simu za mononi kwa website yako. Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo unaweza kuyagundua na kutumia kwa msada wa kizio cha uwiano wa watimkaji

5. Vipachiko (Key words)

Kwanini nimeiweka kizio hiki mwisho? kwa sababu, siku za hivi karibuni, Google wamebadilisha sheria na kanuni zao, na wameanza kutoonesha vipachiko, hivyo kama wewe unatumia Google analytics (Moja kati ya mtambo wa uchambuzi wa bure inayotumiwa na wengi zaidi) basi unaweza kujikuta unaishia kuona vitu kama unknown kibao au usione kabisa.

Kwa kujua vipachiko ambavyo watu wanatumia wakati wanatafuta huduma fulani, kwa mfano, wewe ni mtengenezaji wa website kama Dudumizi, hivyo ni lazima uhakikishe unajua watu wanaotaka kutengeneza website Tanzania wakiwa wanahitaji mtu wa kuwatengenezea website huwa wanaandika nini kwenye mitambo ya utatutajii. Kuna watakaoenda Google na kuandika Website design in Tanzania, au kuna atakayeandika website tanzania nk.

Hivyo, kwa kujua hili, unaweza kusaidia kuboresha ama kurasa za kuondokea ama kuingiza kwenye malengo ya uboreshaji wa mitambo ya utafutaji(SEO).


Walenga walisema, kama usipopima, basi hautoweza kuichunga, hivyo basi kwa kuwa na malengo, ukayaweka kwenye namba halafu ukawa unajitathmini ili kujua maendeleo na wapi ulipofikia ni moja ya nyenzo kubwa kwenye kufanikiwa na kuwa na
website yenye kufikia malengo. Na hii itakuwezesha kuchunga maendeleo ya biashara yako huku Website ikiwa kama moja ya sehemu muhimu.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now