Katika makala zilizopita tumeangalia umuhimu wa kuwa na Website. Pia tumeangalani hatua muhimu za kupitia mpaka unakuwa na website. Lengo la website ni kufanya kazi na siku ya mwisho wewe kama mmiliki ni lazima uone matokeo ya kazi iliyofanywa na website.

Ingawa kumekuwa na mijadala sana kwenye uwanja wa IT juu ya upimaji wa matokeo ya IT, wengi wakisema, ni ngumu kupima matokeo yanayosababishwa na IT pale ambapo IT inakuwa ni  muwezeshaji, na website ikiwa ni sehemu moja wapo. Ukweli ni kuwa, kwa sasa IT si muwezeshaji tena, bali ni sehemu ya kazi. Hivyo, inatakiwa itoe matokeo tena yanayopimika, na website ni sehemu mojawapo. Na lazima ijumuishwe kwenye malengo ya kampuni / shirika.

Kitendo cha upimaji wa Website hutegemea na sababu ya kuanzishwa kwake, leo hii kuna mamia ya website kwenye kila idara, kuanzia blogu za habari hadi zile website za serikali. Hivyo hakuna njia moja kupima mafanikio hayo. Kwakuwa kila website ina malengo tofauti, lakini kuna kitu ambacho website zote zinahusika, nacho ni; zote zinamlenga mtumiaji na mmiliki.

 Uhumuhimu wa kupima mafanikio ya Website.

Mafanikio kama inavyotafsiriwa kwenye kamusi ni ktendo cha kufikisha malengo. Hivyo, katika upimaji huu, wewe kama mpimaji kitu ambacho utakuwa unaangalia ni je umefanikiwa kufikia yale malengo uliyojiwekea katika hatua za awali? Malengo haya huambatana sana na dhumuni la kuanzishwa kwa website, je website yako ilianzishwa kwa ajili ya kutoa habari, kwa ajili ya kuuza bidhaa, kwa ajili ya kuwa kwenye orodha ya wanaomiliki website nk. Hivyo basi, lazima uwe na malengo ili kuweza kupima mafanikio ya Website. Leo hii kuna website nyingi sana zinaanzishwa tu kwakuwa mmiliki naye anataka kuwa na website.


Tukirudi kwenye mashirika au idara nyingi za serikali, unakuta malengo ya idara ya IT (wanaohusika na Website) hayaendani na malengo ya kampuni, kwa mtindo huu IT na Website haiwezi kuchangia kwenye kueleta thamni (Value) ya kampuni. Mfano, unakuta kampuni ya habari inayomiliki gazeti, inasema lengo letu ni kuuza nakala elfu ishirini kwa siku, na wale wa IT malengo yao yanasema kuhakikisha Website inakuwa hewani muda wote na ina muonekano mzuri. Ingawa malengo haya ya IT ni mazuri, lakini je yamegusia vipi kwenye kuongeza thamani (Value) ya kampuni?

Malengo yakiwa ni hatua muhimu itakayokuwezesha kupima mafanikio ya utendaji wa Website, ni lazima yawe na sifa zifuatazo

 

S (Mahususi / Specific): Malengo lazima yawe mahususi. Usiwe na malengo yanayoelea hewani. Kuna maswali mengi unatakiwa ujiulize hapa kama Jinsi gani, muda gani, namna gani nk. Kwa mfano, wewe ni mmiliki wa Website, malengo yaliyo mahususi ni kama, ndani mwaka mmoja tuongeze memba hadi 10000, muda wanaotumia kwenye website uwe dakika 5 na uwiano wa wanaotimika uwe chini ya 40% na tutafanikisha hili kwa kujitangaza zaidi, kuwa na makala zinazowagusa wahusika nk. 

Malengo yasiyo mahususi ni kama, "Kuongeza ubora wa matumizi ya website kwa wateja wetu". Malengo kama haya si mahususi kwani hayatoi picha ni jinsi gani utakavyoweza kufanikisha. Malengo mahususi ni yale yanayogusa sehemu husika kwa vigezo husika , muda husika na jinsi ya kuyafanikisha.

M (Yanapimika / Measurable): Kama nilivyokwisha fafanua hapo juu, malengo ya kuwa na Website lazima yaweze kupimika. Bila kipimo, hutoweza kujua ufanisi wake. Kwenye kupimika ni lazima uhakikishe unaweza kujitambua kwenye kila hatua na kukupa matokeo (majibu) ya maswali yafuatayo. Unataka kufika wapi? Sasa hivi upo wapi? Utafikaje unapotaka? Utajuaje kama umeshafika? Utafanya nini kuhakikisha unaendelea kuwepo ulipo? Hivyo, vipimo vitakusaidia kujitathmini kila hatua katika safari yako ya mafanikio.

A(Yanafikika / Attainable): Epuka kuweka malengo ambayo yapo juu ya uwezo wako kwa wakati husika, ingawa watu wengi wanasema hakuna kisichowezekana, lakini hata unapokata mti, inabidi uende hatua kwa hatua na hivyo ndivyo malengo yanavyotakiwa kuwa. Kuwa na malengo makubwa si kosa, ila kuwa na malengo makubwa zaidi ya uwezo wako ni kosa.

Jaribu kuweka malengo yanayofikika kulingana na hazina / Assets (Resources & Capabilities) ulizonazo kwa wakati huo halafu utakuwa unaongeza hatua kwa hatua. Kwa njia nyingine tunaweza kusema, lazima uwe na malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu. Ya muda mfupi ndiyo yatakuwezesha kufikia yale ya muda mrefu, hivyo utakuwa unapima yale ya muda mfupi, kama umefikia malengo, basi unasonga hatua ya mbele. Kwa mfano, wewe ni mmiliki wa Blog, malengo ya muda mfupi ni kama kuwezesha watumiaji wa simu kusoma makala bila shida, na yale ya muda
mtefu ni kama "Ndani ya miaka mitano, kuhakikisha kila Mtanzania anayeetumia intaneti anaweza kutuma habari aliyoiona pale alipo (Mobile News) na atalipwa kwa kila habari anayotuma kwenye Blogu yangu."

R( Yana matiki / Relevant) : Usiweke malengo ambayo hatuwezi kusema hayana maana, ila hayaingii akilini. Lengo la malengo ni kwa ajili ya kufanikisha kitendo fulani ambacho kitakuwa na manufaa. Kwa mfano, wewe ni mmiliki wa website inayotumia Blogspot, na unataka kuwa na website kamili. Inawezekana lengo lako ni kuwawezesha watumiaji ambao wanaishi nchi ambazo Blogspot haipatikaniki kama China kuweza kuipata Website yako. Lakini, swali la msingi, je katika
watembeleaji / walengwa wako je China ni moja wapo? Kama siyo, bali hayo malengo hayana mantiki kwani hayana msaada mkubwa kwenye biashara / huduma yako.

T(Yenye kikomo / Time Bouund) Chukulia mfano wanafunzi, haijalishi ni wa chuo au sekondari, ingawa muhula una miezi mingi, lakini watu huwa hawajishughulishi kwa sana mpaka pale inapifika imebaki wiki moja kabla ya mitihani kila mtu anashinda maktaba na madarasani. Hivyo hakikisha malengo yako yamegawika kwenye muda fulani. Usiweke malengo yasiyo na kikomo. Kuwa na malengo kwa wakati, kuwa na malengo yasiyo na kikomo, siyo tu hautoweza kujitathmini, bali pia utashindwa kujipa nguvu ya ziada kwenye kuyafanikisha.

Baada ya kuona vitu muhimu vya kuzingatia unapoweka malengo, sehemu ya pili tutaangalia ni vizio gani vya upimaji ni muhimu kama uunataka kupima mafanikio ya Website yako.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now