Umuhimu wa kumiliki na jinsi ya kusajili domain za .tz

Matumizi ya domain za .tz yamezidi kupamba moto. Ukuaji huu uamechangiwa sana na umuhimu wa .tz, kwa mfano, kwa kutumia .tz, kunakutambulisha mmoja kwa moja uhalisia wako au biashara yako, pia inasaidia kupata majina mazuri uyatakayo, kwa mfano leo hii ni ngumu kupata jina kama john.com au khadija.com lakini kupata jina la john.co.tz au lile la khadija.co.tz ni kitu cha kawaida.

Moja ya vitu au mazoea ambayo wengi wetu tunatakiwa kuyajenga ni kuwa, siyo lazima uwe na biashara au matumizi kwa wakati huo ndiyo uanze kufikiria kusajili jina la website. Kumbuka kuwa, jina la website linaweza kusajiliwa na mtu mmoja tu, na likishasajiliwa, hauna uwezo tena wa kusajili jina hilo labda ulinunue kwa aliyelisajili ambapo mara nyingi huwa ni kwa gharama kubwa.Na dunia tuyaokwenda nayo, jina la website litakuwa ni moja ya vitu muhimu kwa kila mmoja wetu.

 Kuna umuhimu wa kusajili jina la website hata kabla haujaanzisha kampuni, ukiwa kwenye hatua za mawazo kabisa. Kwa mfano, binafsi nilisajili jina la Dudumizi.com mwaka 2010 na tukaanza kulitumia mwaka 2011. Pia, ingawa kuna watu wengi wanadhani kwakuwa na domain ya .com basi hawahitaji .tz, hii si kweli, unaweza kusajili majina yote ya .com na .tz halafu ukaamua kutumia moja na nyingine kulipeleka (redirect) kwa unalolotaka.

Mfano, sisi tunamiliki dudumizi.com na Dudumizi.co.tz, ila mtu akiandika Dudumizi.co.tz inampeleka Dudumizi.com na hii ni kwa sababu tuna wateja kwenye nchi mbalimbali, laiti ingekuwa ni Tanzania pekee, basi tungetumia .co.tz pekee.

Ila kipindi unasajili domain, epuka kusajili domain za watu zilizo na haki miliki, kwa mfano, kwakuwa umeona ippmedia.co.tz haijasajiliwa, wewe ukaenda na kuisajili kwa malengo ya kuja kuwauzia wakihitaji, hilo linaweza kuwa ni kosa kama kisheria linavyojulikana Cybersquatting au domain squatting, pia kuna baadhi ya wasajili hucheza na muda wa kuisha kwa domain na kama muhusika hajasajili wao husajili kwa lengo la kuja kumuuzia kwa bei kubwa, hilo nalo linaweza kuwa kosa Renewal Snatching. Hivyo sajili jina kwa malengo mazuri (Good Faith).

Moja ya changamoto iliyokuwa inakabiri au kupunguza ukuaji wa majina ya .tz ni mlolongo au ugumu wake wa usajili. Usajili wa majina ya .tz haukuwa rahisi. Lakini sasa Dudumizi Technologies imekuja na njia rahisi inayokuwezesha kusajili majina ya .tz kwa urahisi hata kama upo nje ya nchi.

Sasa unaweza kulipia kwa kutumia MPesa, Tigopesa, Airtelmoney, Cash, Cheque au hata Bank transfer, na kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kununua kwa kutumia Visa, Mastercard, Paypal na njia nyingine nyingi.Unachotakiwa kufanya ni kwenda Dudumizi.net na kutafuta jina lako na website itakuongoza kwenye kila hatua.

Kumbuka, si lazima uwe na hosting ili ununue jina la website, unaweza kununua jina la website kwa kulihifadhi tu. Ukiwa na swali tuandikie info at dudumizi.com

 Kwa makala kama hizi, fuatilia blog yetu https://www.dudumizi.com/blog.html   au kurasa yetu https://www.facebook.com/dudumizi 

Kumbuka, .tz ni utambulishi wako kama Mtanzania.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now