Katika ulimwengu wa sasa, hakuna kitu muhimu kama kuwa karibu na wateja wako. Siku hizi, wateja wamekuwa na sauti kubwa Ukaribu huu siyo tu unakufanya uweze kupata maoni juu ya huduma au bidhaa unazoziuza, bali pia ni njia muhimu ya kufikisha taarifa kwa wateja kwa haraka zaidi. 

 Siku hizi mitandao jamii imerahisisha sana, si kitu cha ajabu kuona kampuni ikitumia mitandao jamii kufikisha taarifa muhimu. Tumeona mfano mzuri, kwenye uchaguzi wa mgombea uraisi kupitia chama cha CCM, matokeo yalikuwa yanatolewa kwanza kabisa kwenye mitandao jamii kabla hata kutangazwa ukumbuni. Mitandao hii ni kama Facebook, Twitter, Instagram na mingine mingi.

 Katika kipindi chote, Dudumizi tulikuwa tunatumia sana mtandao wa facebook, ukifuatiwa na Twitter kama mitandao jamii. Kwakuwa, Dudumizi tunajihusisha na utengenezaji wa Website (Website Design) na Systems, vitu ambavyo vinatumika kwenye sehemu kubwa ya maisha ya binadamu wa sasa, hivyohatuna budi kuwa karibu zaidi ili pale wateja wetu wanapopata matatizo, tuwe karibu nao, sasa tumefungua akaunti rasmi ya Instagram itakayojulikana kwa Dudumizitech.

Kurasa hii itatumika kama kurasa rasmi ya Dudumizi kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wetu, kwa offer, matangazo, habari mbalimbali nk, hivyo usikose kutufollow.

#Dudumiziteam

Call us now