Kabla ya kuanza utengenezaji wa Website, Logo au zana vitakavyotumika kwa ajili ya biashara, ni muhimu ukaelewa na kuchagua rangi zenye kufafanua unachokifanya. Hakikisha rangi hizo zinafikisha ujumbe wa biashara yako kiufasaha na pia zinaendana na mila na desturi ya walengwa.

 Katiba biashara, rangi ni moja ya vitu muhimu kabisa katika kufikisha ujumbe kwa wateja. Iwe ni rangi kwa ajili ya Website, logo, brochure nk.  Wataalamu wa mambo ya ubongo wanasema, ubongo wa binadamau hutoa mrejesho tofauti pale anapoangalia rangi, mrejesho huu unaweza kuwa wa uzuri, furaha, kupenda nk. Pia mrejesho huo hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

 

Jinsi ya kuchagua Rangi

Ni ngumu kuelezea moja kwa moja unatakiwa kutumia rangi ya aina gani kwa sababu matumizi ya rangi huendana na aina ya biashara huku pia ikichangiwa na mapenzi binafsi kwa kiasi Fulani. Mfano Logo ya Dudumizi ina nyekundu ambayo ni mapenzi ya mmoja wa waanzilishi wake.

Kwa kutumia chati ya rangi ya Pantone unaweza kuona aina za rangi tofauti na kuchagua rangi inayokuvutia. Kumbuka kwa kuchanganya rangi zaidi ya moja unaweza kupata rangi nyingine nyingi zaidi zenye kuleta maana tofauti.

Maana za rangi:

Red: exciting, stimulating, daring, dynamic, bold & sexy.

Blue: comfort, loyalty, security, stable, serenity & peace.

Yellow: caution, bright, cheerful, energetic, mellow, hope & happy.

Green: money, health, food, nature, fresh, healing, soothing & prestigious.

Brown: nature, aged, eccentric, earth, substance, durability & security.

Orange: warm, excitement, friendly, vital, inviting, energetic & playful.

Pink: soft, healthy, childlike, energy & feminine

Purple: royal, religion, elegant, sensuality, spirituality & creativity.

Black: dramatic, serious, strong, mysterious, elegant & powerful.

Grey: business, cold & distinctive.

White: clean, pure & simple.

Hivyo basi, chagua rangi inayoendana na aina ya biashara unayotaka kufanya.

Call us now