Tangu kuanza kuchanganya kwa maendeleo ya Teknolojia Tanzania, tumeona makampuni mengi yakizaliwa siku hadi siku, kila moja likiwa na lundo la huduma wanazotoa kwa wateja wao. Iwe kwa yale ya simu, yale ya kibenki, yale ya kutengeneza programu na hata yale ya kuuza majina ya website (Domain names), wote hawa wamejikitia kuhakikisha mteja anapata anachokitaka.

Kitu ambacho mengi ya makampuni haya yemeshindwa kufahamu ni kuwa, je huyu mteja ANATAKA NINI? mteja hanunui huduma ama bidhaa kama bidhaa, bali ni faida/thamani (Value) inayokuja na ile huduma au bidhaa. Chukulia mfano, wewe ni Bank na unatoa huduma ya kibenki kwa mtandao (Online banking), mteja anayeamua kutumia huduma hii ya kibenki toka kwako, siyo kwa sababu anataka kuwa na akaunti ya bank au kutuma pesa tu, bali nini kinakuja na hii huduma.

Read more ...

Kupata makala zaidi za IT, like kurasa yetu: https://www.facebook.com/dudumizi

Kama wewe ni mfanyabiashara wa kati au juu, basi kuwa na Website ni moja ya vitu vya lazima kwa dunia ya sasa. Takwimu zinaonesha, kuna Watanzania milioni tano wapo online kila siku. Hapa hawajajumlishwa wale walio nje ya nchi.

Kuwa na Website ya kampuni kunafungua milango zaidi kwa biashara yako, kila kona ya dunia inayofikika kwa intaneti, basi website yako inaweza kufika. Kwa kutumia mitambo ya utafutaji (searh engines) kama Google, Yahoo, Bing nk, watu ni
rahisi sana kutafuta wanachokitaka online. Hivyo usipoteze nafasi hii ya kipekee kabisa.

Katika makala za awali, tumeandika sana umuhimu wa website, mambo ya kuzingatia nk, leo hii tutaangalia hatua muhimu za kupitia hadi kumiliki website. Hivyo twende kazi...

1.Andaa bajeti

Bajeti ni kitu cha awali kabisa kwenye kuendea kuwa na website. Siku hizi teknolojia imerahisishwa, unaweza kuwa na website inayoendana na bajeti yako. Siyo lazima uwe na mamilioni ili uwe na website, hakikisha unajieleza ipasavyo pindi unapowasiliana na watengeneza website ili kuwafahamisha ukomo wa bajeti yako na wao wataweza kukupa website iliyo ndani ya kikomo chako.

Kwa mfano, kuhost website ya kawaida haizidi laki moja ya Kitanzania kwa mwaka,na kutengeneza website ya kawaida pia huanzia laki tatu za Kitanzania kwa kampuni ya kawaida,ingawa wapo wanaochaji chini au zaidi ya hapo. Kwa wamiliki wa makampuni makubwa kama Facebook au Google yanatumia mabilioni kuhakikisha website zao zinakuwa hewani bila tatizo.

Hivyo, bajeti haziwezi kuwa sawa, usiogope kujadiliana na mtengeneza Website yako, kama ukipata kampuni iliyo makini, watakusaidia kufikia malengo.

Read more ...

Kuna usemi wa kiswahili unaosema, "mali bila daftari, hupotea bila habari". Maana ya msemo huu sio kwamba kwenye daftari ndio utahifadhi mali zako, la hasha, bali kwa kuwa na kumbukumbu za matumizi ya mali zako, basi utaweza kufuatilia mwenendo wake. Hili ni sawa na kwenye Website, kuwa na website bila kuwa na maandalizi ni sawa na kujenga nyumba bila msingi, ndio maana siku ya mwisho utaona Website ni mzigo usio na maana.

Kuna wakati niliwahi kufanya kazi na mmoja wa wanablog maarufu Tanzania ambaye hadi leo hii amekuwa akiogopa mabadiliko baada ya kufeli kwenye badiliko moja alilotaka kufanya kwenye blog yake.Baada ya kukutana na mimi aliniambia, Nyoni, nimewahi kujaribu, ila tulifeli vibaya, nikamuambia, mulifeli kwakuwa mulikuwa munajaribu na sio muliamua. Kwani kama mungeamua, basi mungekuwa na maandalizi na mipango ya awali kabla ya kuanza maboresho ya blog yako, hivyo mulifeli kupanga, ndio maana mukaja kufeli kutekeleza.

Read more ...

Kwa mara kadhaa nimekuwa nikiongea na watu wengi juu ya suala la kuwa na wavuti ya biashara zao. Wengi wakisema kuna umuhimu gani kwani hata sina uhakika kama kuna mtu atatembelea. Pia wengi wa wafanyabiashara hawa wana mambo mengi sana hivyo kwa wao hakuna muda wa kwa ajili ya wavuti, kwa wao husema wavuti ni kitu cha ziada. 

Kulingana na matokeo ya tafiti kutoka internetworldstats zinaonesha kuwa, kwa mwaka 2012, watumiaji wa internet kwa Tanzania walikuwa 11% ya Watanzania wote, hii inamaanisha kwa katika kila Watanzania 10, angalau mmoja anatumia internet.Huu ni muongezeko wa mkubwa ukilinganisha na watumiaji 1.6% mwaka 2005. Matokeo haya yanaashiria ongezeko kubwa la watumiaji siku hadi siku.

Siku za karibuni tumeshuhudia kwa wafanyabiashara wachache waliopata muamko kuanza kutumia blogs kama njia mojawapo za kuingia online. Hii inawezekana na sababu ya urahisi wake au kukosa motisha na nguvu ya kuwafanya wawe na tovuti kamili. Lakini, swali la kujiuliza, ni kwanini wengi wa hawa wafanyabiashara wamekuwa wagumu kutumia wavuto kamali kama sehemu ya biashara zao? Leo hii haishangazi kuona mmiliki wa hoteli kubwa anakupa kadi yake ina email ya This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Je ni kwa sababu hawafanamu umuhimu wa kuwa na tovuti kamili au kuna vikwazo vinavyowafanya wakate tamaa juu ya malengo ya kuwa na tovuti?

Hebu tuangalie faida zitokanazo na kuwa na wavuti ya kampuni;

Read more ...

Baada ya kukamilisha mafundisho ya Joomla, nimekuwa nikipokea barua pepe nyingi sana toka kwa watu ambao wamekuwa wakiniuliza juu ya template gani bora, kiendelezo gani bora na mengineyo.

Ingawa hakuna jibu la moja kwa moja juu ya ubora, ila kuna jibu la moja kwa moja juu ya nini kinashauriwa. Hapa ninamaanisha, siwezi kusema kiendelezo hiki ni ndio bora au sio bora kuliko kingine kwani kuna njia na mambo mengi ya kuzingatia pindi unapochagua viendelezo vya Joomla. Ila ninaweza kusema kinedelezo kipi kinaweza kukusaidia vipi. 

Leo hii nitagusia viendelezo vitano ambavyo kwenye kila wavuti kumi za Joomla, angalau tisa zitakuwa na moja ya viendelezo hivi.Kama haujawahi kutumia moja ya viendelezo hivi, basi huu ndio muda wa kuvitambua na kuangalia jinsi gani vinaweka kukusaidia kwenye ujenzi wa watuvi zako.

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe
Call us now