Mitandao jamii imekuwa moja ya nyenzo imara kabisa ya kujitangaza na kuwafikia walengwa wengi kwa uharaka na mapana zaidi kwa njia ya mtandao. Jiulize swali dogo tuu, je kwa siku za karibuni umekuwa ukitumia njia gani kufahamu juu ya bidhaa au huduma fulani.
Je kwa kutumia tangazo la kwenye TV au Radio ambapo hauna uhakika hata saa ngapi wataonesha tangazo unalohitaji? Au kwa kupitia gazeti ambapo wengi wetu sasa inapita hata mwezi bila kusoma gazeti lililochapishwa? Au ni mara ngapi umetumia muda wako kusoma lundo la emails kwenye sanduku la email za matangazo (Junk emails)?
Siku hizi watu wamebadilika sana, wateja hupendelea kutafuta huduma toka mahali ambapo wanapata taarifa zote kwa upamoja tena pindi wanapohitaji, baadhi ya njia watumiazo kwa sana ni kama; kwa kutumia mitambo ya utafutaji (search engines) au toka kwa marafiki zao walio kwenye mitandao jamii (Social networks). Na huko ndiko kunakoshibisha njaa ya huduma na kujibu maswali yao yote.