Katika kuhakikisha tunapata muda wa kuwa pamoja na wana Dudumizi, timu nzima ya Dudumizi Technologies LTD inatarajia kuandaa siku ya Dudumizi, yaani Dudumizi Day. Siku hii itakuwa ni wakati pekee wa wana Dudumizi kujuana na jamii, pia wanajamii kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na Dudumizi.

 Katika kuelekea siku hii, tunatarajia kuandaa vifaa vitakavyotumika siku hiyo, hivyo, kwakuwa Dudumizi inahudumia wana jamii, na kwakuwa wana jamii ndiyo wanaoijua vyema Dudumizi. Tunapenda kupata mawazo yao, ni jinsi gani Dudumizi day itaonekana.

 Kwenye kulitambua hilo, tumeandaa mashindano ya kudesign mchoro (artwork) itakayotumika kwenye siku ya Dudumizi, mshindi atachaguliwa na wanajamii wenyewe na kujinyakulia 50,000Tsh pamoja na Wireless Router Mercury MW 302R Mpya and Genuine kabisa.

Jinsi ya Kushiriki:

Read more ...

Moja ya changamoto kubwa inayoikabili jamii yetu,ni kutotimiza majukumu kama yalivyokubaliwa. Yawe tuliyopewa au tuliyojiwekea sisi wenyewe. Kwa upande wa biashara, iwe ni kubwa ama ndogo, ni dhahiri kuwa kutakuwa na majukumu mengi yanayotakiwa kufanyika kila siku kwa ubora uliokubaliwa.

Swali unalotakiwa kujiuliza, je unatumia mtindo upi kuchunga majukumu na kufuatilia muenendo wake? Pia haujawahi kujiuliza, ni tatizo gani linaweza kusababisha kuchelewa ama kutokukamilika kwa jukumu fulani? Na je, hakuna njia yoyote itakayoweza saidia kwenye kuchunga muenendo wa majukumu?

Read more ...

Ndugu wateja wa Dudumizi, kama tulivyowataarifu kwenye salamu ya ujumbe wa mwaka mpya juu ya kuwepo kwa kusudio la kuhama kwa ofisi za Dudumizi. Tunayo furaha kukutaarifu kuwa, ofisi za Dudumizi zimehama kutoka kwenye eneo la zamani ambapo ilikuwa Gates of Paradise Hotel kuja kwenye ofisi mpya kabisa hapa Shamo Park House, lakini bado tupo hapahapa Mbezi Beach.

Read more ...

Awali ya yote, kwa niaba ya timu nzima ya Dudumizi, tunapenda kuwatakiwa heri na faraja katika mwaka huu wa 2015. Ni mwaka wa mambo makubwa sana hapa Dudumizi. Wengi wetu wanaweza kujiuliza, mbona ni salamu zilizochelewa, kumbuka wahenga walinena, "kimya kingi, kina mshindo mkuu" hivyo tarajia mengi makubwa toka Dudumizi.

Na hii itakuwa ni ada yetu, kwa kila mwaka kuzungumzana wateja wetu ili kuwawezesha kutambua nini tunatarajia kufanya ili kuifanya Dudumizi kuwa kampuni namba moja kwenye kutoa huduma za Web Tanzania.

Kama wengi tunavyojua, Dudumizi ilifungua rasmi huduma zake hapa Tanzania mnamo Aprili 2014, tangu kufunguliwa kwake, Dudumizi imekuwa ni moja ya kampuni za Wazawaambayo ni kimbilio kwa huduma za uhakika kwenye huduma za Web, huduma hizi ni kama kutengeneza Website, kutengeneza Web Systems, kuhost website, uuzaji wa majina ya website (domain names), kutengenezea Logo na huduma nyingne nyingi. Kwa mwaka huu mzima, Dudumizi imehakikisha inafikisha huduma iliyo bora kabisa.

Read more ...

Katika ulimwengu wa kijasirimali, tumekuwa tukishuhudia biashara zinazoanzishwa kila kukicha, na moja ya malengo makuu ya biashara yoyote ni kuhakikisha inafanikiwa na kupokelewa vyema na watumiaji.Na mapokeleo haya ndiyo yatakayokujenga au kukubomoa,na mapokeo hayo ndiyo yanayotengeneza brandi ya huduma au bidhaa yako.

Biashara nyingi huwa na majina kama ni njia mojawapo wa kujitambulisha au kujitofutisha na wengine wanaotoa / uza huduma au bidhaa inayofanana.

Kitu unachotakiwa kufahamu ni kuwa, bidhaa / huduma inapokuwa maarufu, inaweza kutengeneza brandi moja kwa moja, na brandi inaweza kutumika kama jina la bidhaa ila kuna utofauti kati ya brandi na huduma. Mfano, bia ya kilimanjaro (brand), watu wengi wakienda madukani husema nipe kilimanjaro ya baridi (wakimaanisha bia ya kilimanjaro),ili kuondoa mkanganyiko, hebu tuangalie tofauti kati ya bidhaa / huduma na brandi.

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now