Moja kati ya changamoto iliyokuwa inawakabili wateja wetu ilikuwa ni jinsi ya kusetup emails za Dudumizi kwenye outlook. Hii ni kwa sababu kwenye server za Dudumizi kuna mabadiliko tumefanya ili kuongeza usalama. Mabadiliko hayo kwa namna moja au nyingine huleta utofauti kwenye jinsi ya kutengeneza email kwenye outlook tofauti na utaratibu wa kawaida.

 Ungana na mkufunzi wetu akikuongoza hatua kwa hatua juu ya jinsi ya kusetup email kwenye outlook.

Read more ...

Kabla ya kuanza utengenezaji wa Website, Logo au zana vitakavyotumika kwa ajili ya biashara, ni muhimu ukaelewa na kuchagua rangi zenye kufafanua unachokifanya. Hakikisha rangi hizo zinafikisha ujumbe wa biashara yako kiufasaha na pia zinaendana na mila na desturi ya walengwa.

 Katiba biashara, rangi ni moja ya vitu muhimu kabisa katika kufikisha ujumbe kwa wateja. Iwe ni rangi kwa ajili ya Website, logo, brochure nk.  Wataalamu wa mambo ya ubongo wanasema, ubongo wa binadamau hutoa mrejesho tofauti pale anapoangalia rangi, mrejesho huu unaweza kuwa wa uzuri, furaha, kupenda nk. Pia mrejesho huo hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Read more ...

Neno Dudumizi si geni katika masikio ya watu wengi. Hapa kwetu Tanzania, Dudumizi inamaanisha ni ndege, ndege huyu mwenye rangi ya ugoro na nyeusi akiwa na macho mekundu ni adimu sana hasa kwa watu wanaoishi mijini, hii inaweza kutokana na uchache wake au mazoea ya ndege huyu. Pia, kwa upande wa pili, neno Dudumizi ni kampuni bora inayojishughulisha na masuala ya huduma za IT kama kutengeneza website, kutengeneza systems za kompyuta na application za simu.

Read more ...

Tanzania inaingia katika kipindi kigumu na cha muhimu sana kwenye historia yake. Ni kipindi ambacho kitasaidia kuamua muelekeo wa nchi kwa miaka mitano inayokuja. Mara nyingi ifikapo wakati wa uchaguzi kuna mambo mengi hubadilika. Biashara huanza kuwa ngumu kutokana na hofu miongoni mwa watu. Pia, ushiriki wa watu kwenye kampeni hufanya muda mwingi kutumika huko hivyo kutoa muda mchache kwenye shughuli kama kazi.

Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka huu tutashuhudia mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya siyo tu aina ya watu wanaoshiriki kwenye kugombea nafasi mbalimbali, bali pia mfumo utakaotumika kwenye kampeni hadi upigaji kura. Mwaka huu tutashuhudia matumizi ya Tehama kwa kiwango kikubwa sana kwenye kampeni za uchaguzi na hata utangazaji na uchungaji wa matokeo ya chaguzi.Tutegemee kupata updates za matokeo ya kura toka kila kituo ndani ya dakika punde tuu wanapomaliza kuhesabu.

Kwa chama chochote kinachotaka kufikia watu na hatimaye kushinda, ni ngumu kufanikisha hilo bila kutumia Tehama. kwa maneno mengine, Tehama ndiyo itakayoongoza uchaguzi wa mwaka huu. Tumeona mfano wa Obama mwaka 2008. Akiongozwa na kauli mbiu yake ya pamoja tunaweza (Yes we can) na matumizi ya mitandao, Obama aliweza kufikisha ujumbe kwa vijana wengi kama ilivyo sasa kwa Tanzania, na hatimaye kushinda uchaguzi wa kihistoria.

Read more ...

Moja kati ya changamoto tunayokutana nayo hapa Dudumizi pindi tunapofanya kazi za wateja wetu ni kuwa, wengi wao wamekuwa wakitaka kukamilisha kazi ya kesho leo. Hii ina maana, mteja anataka website ambayo ina vitu vingi ambayo si lazima vyote vikamilike kwa siku moja.

Kwenye biashara yoyote, kama alivyoandika Simon Sinek's kwenye kitabu chake cha anza na kwanini, "Start with why" kuwa unatakiwa kuanza na sababu ya kuwepo kwa biashara yako, na si nini unatakiwa kufanya. Kwa kujua hili, kutakusaidia kujua na kupanga hatua kwa hatua cha nini kifanyike kwenye muda gani ili kukidhi mahitaji ya wateja.

 Ukiangalia website nyingi maarufu duniani kama Facebook, Twitter, Apple, Google, YouTube, eBay, LinkedIn, Yahoo, na Flickr zimekuwa zikibadilika kuendana na matakwa ya watumiaji na wakati. Hii ni kwa sababu, uwepo wao kwenye biashara unategemeana sana na mambo hayo muhimu. Kumbuka, hazina (muda na pesa) zina kikomo hivyo lazima kuwe na mpango endelevu.

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe
Call us now