Tayari umeshamaliza kusajili kampuni Brela na sasa unajiandaa kukamilisha taratibu za kupata TIN kutoka TRA na hatimaye leseni ya biashara ili kuanza rasmi biashara yako. Umeshikwa na shauku kubwa kusubiria siku kuu ambayo utakata keki kuashiria ufunguaji rasmi wa biashara yako. Lakini, Dudumizi inapenda kukukumbusha kuna kitu umekisahau kwenye orodha ya shughuli za kufanya, nacho ni usajili wa .co.tz domain.
Kumbuka, si lazima uwe na Website ndiyo usajili Domain, usajili wa domain unatakiwa kufanyika mapema ili kulinda jina lako hata kama haujaanza kulitumia. Sajili domain hapa.
Historia ya majina ya Website:
Kabla ya mwaka 1984 ambayo University of Wisconsin technicians walitengeneza seva za majina ya website(Name Server), hakukuwa na majina ya Website, watu walitumia namba tu, mfano, kama unataka kutembelea Website ya Dudumizi, ulitakiwa kuandika https://198.207.55.196. Hebu fikiria tungekwa tunaiandikaje kwenye Business card?
Mwaka 1985, majina ya Website kwa kutumia .com, .net na .org yalianza kutumika na watu kuanza kuachana na namba. Kwa kulitambua hilo, kwa tanzania, mchakato ulianza mwaka 1995 na hatimaye, TCRA iliuna tzNIC kama msimamizi mkuu wa .tz domaiin, na hatimaye, mwaka 2009, tzNIC ilianza rasmi kumanage majina ya .tz domain kupitia kwa mawakala wake, Dudumizi ikiwa mmoja wao.