Website Hosting Companies Tanzania

Website ni moja ya nyenzo muhimu sana na pengine ni ya lazima katika biashara. Kuwa na website siyo tu kunakuwezesha kuwafikia watu wengi nje ya mipaka, bali pia kunakupa njia ya kufikisha huduma zako karibu Zaidi na wateja.

Moja ya changamoto zinazowakabili wengi wenye Website, ni kuhakikisha Website inakuwa na hali ya ubora hata baada ya kuitengeneza. Makampuni mengi yanayotengeneza Website (Website Design Companies) huishia kwenye website na kumuacha mteja aendelee mwenyewe, hii inakuwa ni sawa na kumuacha mtoto anayesimama dede peke yake.

Website nyingi zimekuwa zikipoteza mvuto na ubora punde tuu baada ya kutengenezwa na kuachwa kwa mteja, pia kuna wateja wengi wamekuwa wakihofia kuwa na Website kwa kuhofia hadha ya kuiboresha na kuimanage.

Ili kuhakikisha wateja wetu wanatumia muda wao kwenye biashara huku Dudumizi ikichunga na kuziongoza Website zao, Dudumizi tunakuletea huduma mpya kabisa, Website maintenance. Kwa kutumia huduma hii, Dudumizi tutamanage Website kwa ajili yako. Kwa taarifa Zaidi, tembelea Website Maintenance Page na endapo utakuwa na maoni au ushauri tafadhali wasiliana nasi.

Matumizi ya email za kampuni (Corporate Business Email Address) ni moja ya njia rahisi kabisa ya kutangaza biashara yako kwa wateja. Mfano, miaka sita iliyopita nilinunua mashine ya kutotolesha vifaranga kutoka China na mawasiliano mengi tulifanya kwa kutumia email. Juzi mmoja wa watu wangu wa karibu alitaka kununua machine, alitumiwa quotation nyingi tu, aliponionesha,kulikuwa na emails 13. Kati ya hizo, 3 zilikuwa zenye domain za kampuni 2 Yahoo 5 Gamil 3 QQ. Kupitia email hizo,niiliweza kubaini moja wapo ya hizi email zilizotumia domain za kampuni (Corporate Business Email Address) ni wale walionuzia mashine ambayo inatumika hadi leo. Hivyo, ilikuwa rahisi kwangu kuwabaini na kupelekea kumshauri afanye nao kazi.

 Kitu ambacho nilikuwa ninajiuliza sana, inawezekana vipi mtu akatuma taarifa za kampuni kwa kutumia email za gmail? Utamuhakikishia vipi mteja kama anadili na kampuni na si mtu binafsi (mfanyakazi wa ndani ya kampuni aliyeamua kuifanya hiyo kazi mwenyewe)?

 Matumizi ya emails za bure siyo tu yanakuondolea uthamani (Value), bali kunaweza kukukimbizia wateja wengi. Pia, kumbuka kuwa, si lazima uwe na website ili uwe na email ya kampuni. Unachotakiwa ni kuwa na jina la website na ukanunua bando la email. Dudumizi tunayo huduma ya email kwa kampuni (Business Emails).Huduma hizi zote zinapatikana kwenye website yetu ya Hosting https://Duhosting.co.tz

Read more ...

Tayari umeshamaliza kusajili kampuni Brela na sasa unajiandaa kukamilisha taratibu za kupata TIN kutoka TRA na hatimaye leseni ya biashara ili kuanza rasmi biashara yako. Umeshikwa na shauku kubwa kusubiria siku kuu ambayo utakata keki kuashiria ufunguaji rasmi wa biashara yako. Lakini, Dudumizi inapenda kukukumbusha kuna kitu umekisahau kwenye orodha ya shughuli za kufanya, nacho ni usajili wa .co.tz domain.

Kumbuka, si lazima uwe na Website ndiyo usajili Domain, usajili wa domain unatakiwa kufanyika mapema ili kulinda jina lako hata kama haujaanza kulitumia. Sajili domain hapa.

Historia ya majina ya Website:

Kabla ya mwaka 1984 ambayo University of Wisconsin technicians walitengeneza seva za majina ya website(Name Server), hakukuwa na majina ya Website, watu walitumia namba tu, mfano, kama unataka kutembelea Website ya Dudumizi, ulitakiwa kuandika https://198.207.55.196. Hebu fikiria tungekwa tunaiandikaje kwenye Business card?

Mwaka 1985, majina ya Website kwa kutumia .com, .net na .org yalianza kutumika na watu kuanza kuachana na namba. Kwa kulitambua hilo, kwa tanzania, mchakato ulianza mwaka 1995 na hatimaye, TCRA iliuna tzNIC kama msimamizi mkuu wa .tz domaiin, na hatimaye, mwaka 2009, tzNIC ilianza rasmi kumanage majina ya .tz domain kupitia kwa mawakala wake, Dudumizi ikiwa mmoja wao.

Read more ...

Katika siku za karibuni, kumekuwa na matukio mengi sana ya kukosewa kwa taarifa mbalimbali za Tanzania. Ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Matukio haya yalipelekea kuwa na mijadala mingi sana kwenye mitandao jamii hado kupelekea baadhi ya wahusika kuomba samahani.  Mfano wa mijadala hii ni kama, Mbwana Sammatta alisemwa anatokea Congo, mara Kenya, ikaja Olduvai ipo Kenya, mara Kilimanjaro ipo Kenya na mengine mengi sana.

 Matokeo ya mijadala hii minngi ilikuwa ni suluhisho la muda mfupi, kama kuziba kilaka na si suluhisho la muda mrefu ambalo ni kuboresha taarifa za nchi na vinavyopatikana kwenye mitandao. Kwa upande mmoja, tunaweza kuona majirani zetu ni wachokozi, lakini kwa upande wa uhalisia, mimi ninawaona majirani zetu ni watu wanaojua kutumia fursa ipasavyo. Kenya wamefnikiwa sana kutumia Tehama katika kujitangaza na kutangaza nchi yao na vilivyomo.

Ukweli usiopingina ni kuwa, leo hii, kwenye nchi zote zilizoendelea, watu wanategemea sanasana mitandao kupata taarifa, na si kwenye TV, mabango wala radio kama ilivyokuwa zamani. Hivyo lazima kuwe na kampeni mahususi ya kujitangaza na kuboresha taarifa za Mama Tanzania.

Read more ...

Siku ya Jumatano, Februari 24, 2015, timu ya Dudumizi ikiwa kama mmoja wa wana kikundi, ilipata nafasi kuhudhuria ufunguzi rasmi wa kikundi cha wafanyabiashara (BNI - Business Networkng and Referrals) tawi la Amani. Ufunguzi  ulianza saa kumi na mbili na nusu hadi saa tatu asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Ramada.

 Uzinduzi huo, ulienda sambamba na utambulisho wa makampuni kutoka kwa wana Amani pamoja na mafundisho ya kibiashara yaliyowezeshwa na Mr Vishal kutoka BNI Dubai.

BNI inasimama katika falsafa ya Givers Gain, ikijikita katika kupena nafasi kibishara (Referrals). Ndani ya BNI, kila biashara hupata nafasi ya kunadi biashara pia kuomba nafasi ya kuunganishwa na watu husika. Hii inamaana, wana BNI husaidiana kibiashara, kama wewe ni mfanya biashara, huwezi ikosa nafasi hii adimu. Washiriki wa BNI hukutana mara moja kwa wiki kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi hadi saa mbili asubuhi, huu ni wakati mahsusi kupanga mikakati ya kibiashara.

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now