Ni kitu cha kawaida kwa wafanya biashara wengi kutumia email zao binafsi kwa matumiziya kiofisi. Kwa Tanzania, si kitu cha ajabu ukaona tangazo kwenye mitandao halafu mtu akaandika wasiliana nami kwa kutumia This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..
Wengi wao hawafahamu ni jinsi gani matumizi ya email binafsi zinavyowapunguzi uaminifu kwao. Je unataka kujua kwanini matumizi ya email ni kitu cha msingi na jinsi gani unaweza kuongeza uaminifu kwenye biashara yako? Endelea kusoma makala hii.
Ni zaidi ya Email
Ni kitu kigumu sana kumshawishi mteja anunua bidhaa au huduma yako, ukizingatia katika hali ya uchumi wa sasa wa kubana matumizi, kila mtu anajitahidi asifanye makosa kwenye manunuzi, hivyo kuaminika ni kitu muhimu. Uaminifu huu hujengwa na vitu vingi, kama taswira uliyoijenga sokoni, mitazamo ya wateja, jinsi unavyowasiliana nao na pia njia za mawasiliano na wateja, email ikiwemo moja wapo.
Watena wana njia mbalimbali za kujenga uaminifu na taswira bora ya kampuni. Email ya kampuni ni moja ya nyenzo za ujenzi wa taswira bora.