Kwenye nchi nyingi, wanafunzi wa chuo ni moja kati ya makundi yaliyo active katika kufanya kazi, na mapinduzi mengi ya uchumi hutegemea kundi hili, kwani wana nguvu na uwezo mpana. Kazi nyingi za vipindi (part time) huwa zinafanywa na kundi hili. Hii siyo tu inawasaidia kuongeza kipato, bali inawafanya wawe na ubongo ulio active haswa kwenye sehemu ya pili ya maisha, maisha halisi.

Kinyume na hiki, tunakuwa tunatengeneza kundi kubwa la vijana wasomi lakini wanakuwa wamedumaa kwenye kujishugulisha. Na, ni moja ya sababu bumu linapochelewa, inakuwa shida kubwa na maandamano yasiyoisha.

Hali hii, huwa inaathiri sana sekta binafsi pale unapomuajiri mwanachuo moja kwa moja kutoka chuoni, kwani kunakuwa na kazi mbili kwa pamoja, kumbabidili kutoka mwanafunzi kuwa mfanyakazi (huku ukipambana na uhalisia vs ndoto) and kumfundisha kazi kitu ambacho kwenye Uchumi wa viwanda italeta shida, na ni moja ya sababu waajiri wengi hukimbilia kuajiri raia wa kigeni kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa.

Kuna sababu nyingi kwenye hili na kila upande anaongea lake, Upande wa wanachuo wanasema, Wakufunzi wanabana sana hivyo unashindwa hata muda wa kusoma, na upande wa wakufunzi wanajitete kuwa wanafunzi ni goigoi wanapenda mambo rahisi hivyo hawajishugulishi kutwa kuchinda kwenye mitandao jamii, ukiwaachia huru utavuna mabua.

Read more ...

Katika ulimwengu wa IT, kuna usemi unaosema, IT doesnt matter, usemi huu unamaanisha, kwenye kila matumizi ya IT, jambo la msingi si teknolojia (IT), bali ni matokeo yake, na jinsi gani yanavyoweza kuendana na matakwa ya biashara (IT Governance)

Tukiwa kama Website Design Company, Dudumizi tumefanya kazi nyingi za Website, Systems na Applications. Nyingi ya kazi hizi zimekuwa na muingiliano mkubwa, huku kukiwa na upekee wake kwenye kila project.

Katika kuhakikisha tunawasaidia wateja wapya ambao bado wanatafakari ni jinsi gani na wao wataweza kufikia ndoto zao za kuwa na Website, tunakuletea mfululizo wa Case Studies, ambao tutakuwa tunafafanua kila kazi tuliyoifanya, na kuweza kuona uhalisia wake.

Jina la Mteja: Elite Bookstore

Mahali: Mbezi Beach, Dar es Salaam

Kundi: Book seller, Book Publisher, Writer

Aina ya Website: Online Shopping Website (e-Commence)

Muda: Siku 35 

Wazo Kuu: 

Tulipokea maombi ya kuiboresha Website ya Elite toka Website yao ya sasa, leo kuu la Elite ni kuwawezesha kuuza vitabu, Games, stationaries na vingine vingi online kwa urahisi zaidi. Mbali na uuzaji wa vitabu, Elite walikuwa na Challenges zifuatazo;

1. Kwakuwa Elite wana maduka Dar es Salaam (maeneo mengi) na Kilimanjaro, hivyo wakawa wanataka kuwa na njia rahisi ya kujua stock iliyopo, hii ni kwa sababu, vitabu sasa vitauzwa Online na kwenye maduka yote, hivyo Website mpya ni lazima iweze kuwa updated kutoka kwenye maduka.

2. Elite wamekuwa wakipokea maombi ya vitabu ambavyo havipo dukani, na mara nyingi kuwekuwa na ugumu kwenye kufuatilia maombi haya kwakuwa kila duka hukusanya kivyao na kutuma makao makuu, lakini ugumu unakuja, unakiri huu hutegemea sana mtu aliyepokea maombi,hivyo wakahtaji kuwa na uwezo wa kurecord maombi haya yote online, mteja anaweza kutuma maombi moja kwa moja online, pia mamanger wa maduka, wanaweza  pia kutuma maombi haya kupitia  akaunti zao kwenye website

 Pia, Elite walitaka wawe na uwezo wa kuwataarifu wateja pale kitabu kitakapoletwa. 

Kwa kuwa na uwezo wa kujua idadi ya maombi, Elite watakuwa na uwezo wa kukadiria matwakwa (Demand) ya vitabu na mawasiliano yaliyoboreshwa kwakuwa email zote zinatakiwa zitumwe kupitia Website.

3. Wakiwa kama duka lenye miaka kadhaa, Elite wana idadi kubwa ya vitabu offline, hivyo walitaka wawe na uwezo wa kuhamishia maelfu ya vitabu online bila kupoteza taarifa muhimu kama waandishi, publishers, isbn na vingine vingi.

4. Muonekano wa kulidhisha utakaowawezesha watumiaji wa simu na komputa kutembelea Website bila utata wowote.

Read more ...

Dudumizi imekuwa ikiendelea kuboresha huduma zake siku hadi siku. Hii ni kwa sababu, mahitaji ya wateja yanabadilika na ni jukumu letu kuhakikisha tunakupatia mteja wetu huduma zilizo bora, iwe za Website Design, ziwe na App Design au Website Hosting.

Kwa muda wa miaka miwili tangu tuingie kwenye soko la Tanzania, Dudumizi imeweza kuwa kati ya makampuni kumi bora Tanzania yanayotoa huduma za Website Hosting na Domain Registration

Kuanzia mwaka 2017, Dudumizi itafanya mabadiliko makubwa ili kuwezesha huduma na bidhaa zake kusimama imara zaidi. Ukiachia huduma za kutengeneza Website na Application za simu, Dudumizi ina bidhaa zake kama Michongo (kwa ajili ya kuuza na kununua bidhaa zilizo kwenye punguzo), DuLaw (Application inayowawezesha Law firms au Legal Department kujiongoza kwa ufanisi zaidi), Kipanga (Social Business and Governance Platform) na DuHosting (Web Hosting and Domain Registration Playform).

Hivyo, ili kuboresha huduma ya Hosting, kuanzia sasa huduma hii itasimama ikijitegemea na itapatikana kwenye anuani yake pekee. Pia, utaweza kupata huduma zilizoboreshwa kwa ajili yako na mengi zaidi.

Maana ya Logo: 

Rangi: nyekundu na Njano ya dhahabu: Ikimaanisha uharaka, umakini na ubora

Dragon: Ikimaanisha ubora na upekee kwenye tasnia hii.

 

Dudumizi Team

Ni kitu cha kawaida kwa wafanya biashara wengi kutumia email zao binafsi kwa matumiziya kiofisi. Kwa Tanzania, si kitu cha ajabu ukaona tangazo kwenye mitandao halafu mtu akaandika wasiliana nami kwa kutumia This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

Wengi wao hawafahamu ni jinsi gani matumizi ya email binafsi zinavyowapunguzi uaminifu kwao. Je unataka kujua kwanini matumizi ya email ni kitu cha msingi na jinsi gani unaweza kuongeza uaminifu kwenye biashara yako? Endelea kusoma makala hii.


Ni zaidi ya Email

Ni kitu kigumu sana kumshawishi mteja anunua bidhaa au huduma yako, ukizingatia katika hali ya uchumi wa sasa wa kubana matumizi, kila mtu anajitahidi asifanye makosa kwenye manunuzi, hivyo kuaminika ni kitu muhimu. Uaminifu huu hujengwa na vitu vingi, kama taswira uliyoijenga sokoni, mitazamo ya wateja, jinsi unavyowasiliana nao na pia njia za mawasiliano na wateja, email ikiwemo moja wapo.

Watena wana njia mbalimbali za kujenga uaminifu na taswira bora ya kampuni. Email ya kampuni ni moja ya nyenzo za ujenzi wa taswira bora.

Read more ...

Tunayofuraha kuwataarifu wana Dudumizi na jamii kwa ujumla kuwa, baada ya kukaa jikoni kwa muda mrefu, tunatarajia kuzindua programu yetu ya mauzo, inayojulikana kama Michongo App.  Application hii ya Michongo inakuwezesha kuuza na kununua bidhaa mbalimbali zilizopo kwenye punguzo.

 Michongo inajitofautisha na programu nyingi za mauzo ya online kwa sababu kuu zifuatao;

1. Michongo inauza bidhaakwa bei ambayo hauwezi kuipata sokoni. Inamaana, Michongo imeshabageni bei kwa ajili yako.

2. Michongo inatumia programu rafiki ya Affiliate kuwezesha watu kuingiza kipato kwa kila linki wanayosambaza kwa marafiki zao na rafiki akanunua bidhaa. Hii inamaanisha, Michongo ni agent wa timu ya sales itakayokufanyia kazi. Kwa mtindo huu, unaweza kupunguza gharama za kutangaza biashara yako hadi nusu kwa sababu hakuna gharama yoyote kwa kutangaza kwenye Michongo, pia kuna mamilioni ya watu watakuwa busy kusambaza link za bidhaa yako. Hii itawawezesha wajasiriamali wadogo wengi kuingia sokoni na kutengeneza ajira zaidi na zaidi, kama malengo ya Rais wetu (kuongeza ajira).

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

  • Website Hosting

  • 80000Tsh

  • /Year
    • 1Gb Web Space
    • Unlimited Email Accounts
    • Free Website Builder
  • Subscribe
Call us now