Katika siku za karibuni, tumesikia habari kuhusu tishio la usalama wa watumiaji wa kompyuta za Windows. Tishio hili limekuja kutokana na kusambaa kwa minyoo inayobeba udukuzi wa ransomware. Udukuzi huu umeshambulia sehemu nyingi duniani (Tanzania, haswa dar es Salaam ni mojawapo), ila nchi zilizoathirika sana ni zile nchi zilizoendelea kwakuwa wao wamekuwa wakitegemea sana matumizi ya kompyuta kwenye kila shughuli. Kama ilivyo ada yetu, tukiwa kampuni inayoongoza kwa Website design na Website Hosting Tanzania, ambapo zote zinahusika na matumizi ya kompyuta, tunakuletea ufafanuzi wa kina utakaokuwezesha kufahamu kiundani udukuzi huu na jinsi ya kujikinga.

Idara zaidi ya 48 huko Uingereza, kampuni za FedEX, Telefonica, renault na Nissan ni mojawapo ya zilizoathirika na udukuzi huu, pia inasemekana Idara za serikali za Urusi na ATM nyingi China nazo zimekuwa wahanga wa shambulio hili, kiufupi kompyuta na seva zaidi ya 200,000 duniani kote zimeathiriwa hata kuppelekea baadhi ya nchi kama Uingereza kusitisha baadhi ya huduma za Afya kutokana na kompyuta kushambuliwa zaidi.

Ushambulizi huu umesababishwa na mfumo wa kuvamia kwa watumiaji wa kompyuta unaojulikana kama Ransomware. Ransomeware ni suhambulizi wa kompyuta kwa kumzuia mtumiaji kutumia kompyuta mpaka atakapofanya tukio linaloamrishwa na mvamizi Utekaji wa kompyuta(Compyuta kidnaping).

Wadukuzi wa The Shadow Brokers wameiiba programu hii kutoka Shirika la Usalama wa Marekani (NSA)  ambalo moja ya kazi zake ni kufuatilia na kuchunga usalama wa kimtandao. NSA hutumia programu hizi kudukua na kupata umiliki wa kompyuta za magaidi, lakini mwezi April programu hiyo iliibiwa. Wadukuzi hao waliamua kuiweka kwenye mtandao bure kwa lengo la kuonesha kutokukubaliana na raisi Dornald Trump. Wadukuzi wakaitumia program hiyo yenye kuweza kushambulia kompyuta zenye Windows, ushambulizi (exploit) ambao ulipewa jina la EternalBlue na kampuni ya Microsoft. Ushambulizi huu, hutumia minyoo (worms) na kutengeneza aina ya Ransomware inayojulikana kama WanaCrypt0r 2.0, Wanacry au Wanacrypt au Wcry ambao husambaza ransomware kwa njia ya email zenye mtego /kugushi (phishing) ambapo huonekana zinatoka kwa mtu mwenye nyadhifa (kama bosi wako)  kumbe sivyo.

Kama ilivyo matoleo mengine ya ransomware, Wannacry ransomware inatumia udhaifu uliopo kwenye kompyuta nyingi zinazotumia Windows. Shambulio hili jipya, limepelekea kampuni ya Microsoft inayotengeneza mitambo endeshi ya kopyuta (Operating Systems) aina ya Window kutoa kiraka (pacth) kwa ajili ya matoleo hata yale ya zamani (kama Window XP, Windows 7, Windows Server 2003 na mengine), hivyo kama bado haujaupdate Windows yako, wakati ni sasa kuziba kiraka.

Kiufupi, Wannacrypt husambazwa kwa njia ya Minyoo (Worm) kutoka kwenye kompyuta iliyoshambuliwa kwenda kwenye kompyuta nyingine yao yenyewe (automatically), kusambaa na udukuzi huu huwezeshwa kupitia udhaifu (Vulnerability) uliopo kwenye sehemu ya operating system ya windows (SMB file Sharing). Ingawa udhaifu huu ulishapatiwa kiraka na kutatuliwa kwenye kiraka kilichotolewa Mwezi wa tatu, lakini kuna watu wengi bado hawakuupdate, haswa wale wanaotumia Windows zisizo halali au zile za zamani kama XP, Windows 7 na nyinginezo.

Baada ya kushambuliwa, programu hii huzuia muhusika huambiwa mafaili yake yamefungwa (encryted) na hupewa siku ambapo unatakiwa kulipia la sivyo basi mafaili yatafutwa. Malipo hayo yanatakiwa kufanyika kwa njia ya pesa ya kidigitali (Bitcoin), muhusika hupewa utaratibu wa jinsi ya kukamilisha malipo ikiwemo anuani ya malipo.Kwa wasiofahamu, Biticoin ni aina ya pesa kwa njia ya dijitali ambayo huwezesha kutuma na kupokea pesa bila kujulikana (Annonymously).


Ransomware hufanya nini

Ransomware hutofautiana, lakini zote zinafanana kwenye kitu kimoja, humzuia mtumiaji kutumia kompyuta, Ransomware hukutaka kufanya kitu fulani kabla ya kukuacha kutumia kompyuta. Shambulio hili huathiri aina zote za PC za Windows zenye udhaifu (Vulrnerable), iwe ni kwa ajili ya binafsi, iwe seva nk.

udukuzi wa ramsomware huweza kufanya yafuatayo;

 • Kukuzuai kutumia kompyuta mpaka ufanye malipo (Na Wannacrypt imejikita hapa)
 • Kuencrypt mafaili na kuyafanya yasitumike tena
 • Kuzuai baadhi ya application kutofanya kazi (mfano ni browser ya kompyuta nk)

Ransomware hukutaka kulipa kiasi fulani cha pesa, haswa kwa njia ya mtandao ili kukuwezesha kutumia kompyuta yako, ingawa hakuna uhakika kama baada ya kulipa utaweza kutumia kompyuta yako kama ilivyokuwa awali.

Jinsi Ushambulizi unavyotokea

Kama tulivyoona hapo juu, udukuzi huu wa Wannacry ransomware hutumia minyoo kusambaa kutoka kwenye kompyuta iliyoatthirika kwenda kwenye kompyuta nyingine zilizounganishwa na network. Sifa kuu ya minyoo ya kompyuta ni uwezo wake wa kusambaa kwenye Network, tofauti na Virusi, Minyoo husambaa bila kubonyezwa (clicked), hivyo inahitaji mtu mmoja tu kwenye network awe ameathirika, basi minyoo itasambaa kwa watu wengine wote.

Kompyuta huweza huathirika na ransomware kwa moja kati ya njia zifuatazo;

 • Kutembelea Website zisizo salama, zenye walakini au zisizo za kweli
 • Kufungua vipachiko au email kutoka kwa watu usiowajua au usiowategemea (mfano risiti ya malipo, picha za warembo nk)
 • Kufungua linki zisizo salama kwenye email,Facebook, Twitter na mitandaomingine ya kijamii au programu za mawasiliano kama Skype.

Nini Cha kufanya

Kimsingi, ni kazi ngumu sana kurudisha kompyuta iliyoshambuliwa na ransomware, haijalishi ni aina gani ya Ransomware, iwe Wannacry au nyinginezo. Hivyo, njia bora kabisa ni kujikinga na udukuzi na kuhakikisha unakuwa makini pindi unapotumia mtandao.

Hakikisha unazingatia;


 • Kuhifadhi (backup) ya mafaili yako kwenye sehemu tofauti isiyo na muunganiko na kopyuta yako ya sasa. Hii itakusaidia kurudisha mafaili punde unapovamiwa
 • Usibonyeze (click) link yoyote kwenye Website au email mpaka uwe na uhakika wa hiyo linki na muhusika unamjua
 • Kama una mashaka na linki yoyote, usibonyeze
 • Kama Website ina mambo mengi muhimu au inahitaji taarifa fulani, hakikisha Website ina alama ya https, mfano https://dudumizi.com au https://dudumizi.net
  Usifungue email zisizo rasmi, mara nyingi emails zisizo rasim huwa na majina yasiyoeleweka au yaliyokosewa au yaliyoongezwa, mfano This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. (hapa wameacha i kwenye zi)
 • Hakikisha unatumia antivirus na ipo updated
 • Hakikisha unakuwa makini kwenye kufungua kipachiko inayotoka kwa mtu unayemfahamu, kwakuwa wavamizi huweza kutumia ulaghai wa email (phishing email) na kuonesha inatoka kwa bosi wako kumbe siyo
 • Hakikisha kompyuta yako imepachika viraka (patches) vyote muhimu kutoka Microsoft
 • Jengwa utaratibu wa kuandika link kwenye browser badala ya kubonyeza zilizopo kwenye emails
 • Jaribu kurepy email ili uone kama inaenda kwenye email iliyojia, kama sivyo basi kuna walakini

Je udukuzi wa Wannacry umezuiliwa?

Kwa bahati nzuri, mtaalamu wa masuala ya usalama wa Uk aligundua uwepo wa swichi ya kuzima kutapakaa kwa udukuzi wa Wannacry ndani yake. Swichi hii imeunganishwa na jina la Website (iuqerfsodp9ifjaposdfjhgosurijfaewrwergwea.com) ambalo hufanya programu kuacha kusambaa pindi inapoona jina hilo la website lipo hai (active). Baada ya kusajiliwa kwa jina hilo (domain name), ransomware iliitambua na kuacha kusambaa.

Jina hili la website limeunganishwa kwenda kwenye seva maalumu ya majina (DNS) iliyopo marekani, seva hii ni maalumu kwa ajili ya kutoa majibu hewa kwa lengo la kuzuga wahusika (sinkhole). Tayari IP za seva hii zipo kwenye uchunguzi wa FBI na seva kivuli imeshatengezwa kwa ajili ya kupokea taarifa ili zitumike kutambua walioathirika na kuwataarifu kama itahitajika.

Ingawa kuna taarifa zinazokinzana juu ya uwepo wa swichi kwenye Wannacry ambapo mmoja wa hackers wanaotambulika sana  kuja na uwepo wa swichi tofauti na mashambulio mapya, hivyo hali bado haijatengemaa kama inavyosemekana ingawa imepungua.

 

 

Nini tutegemee

Kama tulivyoeleza hapo juu, kilichofanyika ni kuzuia kuendelea kwa kusajili Domain, hivyo tutegemee muda wowote kuanzia leo Jumatatu kulipuka upya kwa aina nyingine ya ushambulizi baada ya wahusika kubadili swichi ya kuifunga programu na kuanza kutapakaa tena. Hivyo hakikisha unafuata hatua bora za utumiaji kama tulivyoainisha hapo juu.

Microsoft wanajiandaa kuja na Aptch kwa matoleo yote ya awali hata yale waliyositisha kuyapa support, hii ni kwa sababu, inaonekana idara nyingi, haswa za serikali na Afya bado wanatumia matoleo hao. Hii ni kwa sababu ya muingiliano wa programu na taratibu za kuhamia matoleo mapya.

Kwa watumiaji wetu wa Dudumizi, seva zetu bado zipo salama na tutaendelea kuwataarifu pindi kutakapojitokeza tishio lolote la kiusalama. Pia, tunawashauri wamiliki wa Website kutumia https kwenye Website zao. Dudumizi.net inatoa huduma hii kama kipachiko kwenye Website Hosting. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi. 

Kusoma zaidi:

Dudumizi imekukusanyia linki zenye uhusiano zaidi juu ya makala hii ambapo utapata uelewa wa kutosha.

http://www.bbc.com/news/health-39904851

https://blog.comae.io/wannacry-new-variants-detected-b8908fefea7e

https://twitter.com/msuiche

https://www.theregister.co.uk/2017/05/14/microsoft_to_spooks_wannacrypt_was_inevitable_quit_hoarding/

http://www.telegraph.co.uk/news/2017/05/12/russian-linked-cyber-gang-shadow-brokers-blamed-nhs-computer/

http://www.bbc.com/news/technology-39920269

 

Kama wewe ni muathirika au una mchango, tafadhali changia makala hii ili kuwashauri wengine.

 

Unapomaliza kusajili na Jina la Website (Domain Name),kuna vitu vingi unaweza kufanya, wengi hudhani baada ya hapo kinachofuata ni kuanza Website Design. Kati ya vitu vinavyohusiana na domain, Domain Transfer na kubadili name Server ni moja kati ya vitu vinavyowachanganya wengi. Hata hapa Dudumizi tumekuwa tukipokea simu nyingi sana juu ya kupata ufafanuzi. Hivyo, kama kawaida yetu Dudumizi tunakurahisishia maisha ya kuwa mmiliki wa Domain Name.

Katika makala hii tutaangalia utofauti kati ya kuhamisha domain kwenda kwa msajili (registrar) mwingine (Domain Transfer) na kubadilisha namer Servers.

Msajili ni nani

Unaposajili Domain name, unatakiwa kuchagua msajili ambaye atakusajilia domain. Usajili huu huendana na mkataba wa umiliki wa domain. Ninapoongelea mkataba, ni mkataba wa muda wa umiliki, ingawa ni msajili ndiye anayekusajilia hii domain, lakini wewe ndiye utakuwa mmiliki halali wa hii domain kwa kipindi mulichokubaliana, mara nyingi huwa ni mwaka mmoja au zaidi. Na kila mwaka utatakiwa kurenew mkataba huu. Punde unapoacha kurenew basi umiliki wa domain yako utakuwa umeisha.

Kwa mfano, wasajli wa domain hapa Tanzania ni kama Dudumizi Technologies, Extreme Technologies, Web Technologies, ASYX Group na wegine wengi ambao unaweza kuwapata. Na kama unatafuta registrar wa nje ya nchi basi kuna Domain.com, Go Daddy, Hostgator na wengine wengi.

Gharama za kusajili domain hutofautiana kutoka registrar mmoja hadi mwingine, pia hutegemeana na kikoo cha domain, kwa mfano, kwa .tz hapa Dudumizi tunasajili kwa 20,000TZS wakati za .com tunasajili kwa 30,000TZS.

Kumbuka, si lazima kufanya Website Hosting na kununua Domain kwa mtu mmoja, kama unataka kufanya kwa makampuni tofauti, utahitajika kubadili name servers, makala hii inakufafanulia.

Sababu za ku transfer Domain

 • Unataka kumanage dmain na website hosting mahala pamoja
 • Umenunua domain ambayo ilikuwa kwa msajili mwingine tofauti na yule uliyemzoea
 • Umeuza Domain na mmiliki anataka kuhamisha kwa msajili wake
 • Kampuni iliyokusajilia domain inaelekea kufa au uwepo wake hauna uhakika

Mambo ya kuzingatia kabla haujaanza mchakato wa kuhamisha domain

Kabla haujaanza mchankato wa kuhamisha domain, unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo;

 • Kama domain name ni ya .com, basi inatakiwa iwe imeshafikisha siku 60 tangu iliposajili
 • Unatakaiwa kufahamu kama name servers nazo zitatakiwa kubadilika baada ya kuhamisha domain
 • Hakikisha domain yako haijapita muda wake (expired)
 • Unatakiwa uwe na uwezo wa kupata funguo za uhamishaji (transfer keys)

Utaratibu wa kuhamisha Domain (Domain name transfer)

Utaratibu huu unafanana sana, iwe ni .com au .tz, awali ya yote, unatakiwa kuwasiliana na msajili wako wa sasa, nao wataanzisha mchakato kwa kukutumia namba ya siri. Utaratibu huu hutofautiana kutoka msajili mmoja hadi mwingine.

Baada ya kupata funguo, basi utawasiliana na msajili wako mpya na kuanzisha mchakato wa kuhamia kwake. Mchakato huu hutumia siku chache, hadi siku tano kulingana na msajili. Kumbuka kuwa, utatakiwa kupitisha maombi ya uhamaji, uhakiki huu hutakiwa kufanywa na mmiliki wa sasa wa domain.

Name Servers

Name server ni seva zinazotumika kufanya utafsiri wa makazi ya Website yako. Name server inawezesha kutambua makazi ya website au email.

Kubadili Name Server
Ni kitendo cha kubadili name server kwenda mahali ambapo utapenda kumanage domain yako. mara nyingi name servers zinaonekana kwenye mtindo kama;

ns1.dudumizi.net

ns2.dudumizi.net

Kubadili Name severs, unatakiwa ama kufanya mwenyewe kupitia upande wa mtumiaji au kuwasiliana na msajili.Kumbuka, unapobadili name sever, mara nyingi hutumia muda mpaka ianze kufanya kazi kwenda kwenye name server mpya.

 

Ukomo wa mkataba wa Domain

Kulingana na sheria na kanuni za umiliki wa domain kama ilivyoanishwa na Taasisi ya Majina ya Website Duniani (Internet Assigned Numbers Authority) endapo baada ya mwaka kuisha mmiliki wa Domain Name atakuwa hajarenew mkataba wa umiliki wa domain, basi domain yako itaingia katika mchakati wa kufutwa. Mchakato huu hupitia hatua zifuatazo;

 • Ndani ya mwezi wa kwanza, domain huondolewa kabisa katika orodha ya muunganisho wa domain (NS Records).

Kama utataka kurenew domain katika kipindi hiki, basi utalipia gharama za kawaida z domain na domain yako itarudi kama kawaida.

 • Baada ya mwezi kupita, domain inaingia katika kipindi cha kufutwa

Domain ikishaingia katika kipindi hiki, gharama ya kuirudisha huwa ghali kwa sababu huambatana na gharama ya kuiondoa kwenye kufutwa. Gharama hutofautiana kutoka kwa msajili mmoja hadi mwingine ila mara nyingi ni mara mbili ya gharama halisi ya domain.

 • Baada ya miezi miwili kupita, Domain hufutwa na mtu yoyoe anayeza kuisajili

Hadi hapa, unakuwa umeshapoteza umiliki wa domain yako. Ingawa mtu yoyote anaweza kuisajili, ila uzoefu unaonesha, inakuwa ngumu sana kuipata tena domain haswa kama ilikuwa na traffic nzui. Hii ni kwa sababu kuna watu wengi wametengeneza mitambo yenye kazi ya kutafuta domain kama hizi (zilizofutwa ila zila watembeleaji wengi) na kuzisajili kwa majina yao hivyo kupata watembeleaji wako watakaopotelea huko.

Athari yake ni kubwa kibiashara, hivyo hata kama umeamua kusimamisha biashara, inashauriwa ukaendelea kushikiria domain name yako mpaka siku utakaporudi tena.

Ni matumaini makala hii itakuwa imekusaidi kujua utofauti kati ya name server na domain, n,a ni muda gani unatakiwa kuhamisha domain. Pia tumeona umuhimu wa kuendelea kushikilia umiliki wa domain hata kama umesitisha biashara. Kama unataka kuendelea kushikilia Domain yako, usisite kuwasiliana nasi.

Katika Dunia ya sasa, kuwa na Website si jambo a kujiuliza mara mbili, mfanya biashara yoyote aliye makini na biashara yake ni lazima awe na Website. Kuwa na Website siyo tu kutakufanya kuwafikia watu wengi zaidi ya walio kwenye uzio wako, bali pia huongeza thamani ya biashara , kwani mtazamo wa watu huwa chanya zaidi pindi unapokuwa na Webste au Email, huonekana upo makini na unachokifanya.

Tumekuwa tukipokea maombi mengi ya kutaka kutengenezewa Website (Website Design), na baada ya uchunguzi tumeona kuna kundi ambalo inawezekana liliachwa kutokana na gharama kuwa nje ya uwezo wao. Hivyo, Dudumizi tukiwa kampuni inayoongoza kwenye Website design in Tanzania, tunakuletea ofa kabambe kwa ajili ya Website Design, Webste Hosting, Domain Registration na huduma nyingine. Ofa hii ni kwa ajili ya makampuni madogo na ya kati kuweza yaliyo Tanzania na itaisha mei 5.

Pata Webiste kwa bei ya 600,000TZS tu huku ikijumuisha;

 • Full Responsive Website
 • Unlimited Business email
 • CMS to manage your website
 • IT Business Consultation
 • Search Engine Optimization (SEO)
 • 1 Year Web maintenance
 • 2GB website & email Hosting
 • Full Cpanel Acces
 • Web Analytic
 • Website & Email backup

Ofa hii ni kwa ajili ya muda maalumu wa sikukuu ya Wafanyakazi ambapo itaisha mei 5. 

Kama upo Interested, tuandikie This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au Tembelea Dudumizi.com

 

Katika nchi nyingi za zinazoendelea haswa zilizo chini ya jangwa la sahara, Tanzania ikiwamo, tumekuwa tukikabiliwa sana na matatizo ya Afya bora. Na moja ya sababu kubwa ni kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya njia thabiti za kuishi kwa kufuata taratibu sahihi za afya.

Kuna usemi wa kiswahili unaosema, "Kinga ni bora kuliko Tiba", hii ina maana, kama utafuata njia thabiti za kujikinga na tatizo, ni bora zaidi kuliko kusubiri kuja kupata matibabu. Na hii ndiyo sababu tumekuwa tukiona harakati nyingi za kusambaza elimu ya Afya bora na kuhakikisha watu wanajikinga na maradhi mbalimbali. Na hata wale waliota maradhi, jinsi gani ya kuishi ukiwa mgonjwa.

Hakuna nchi inayoweza kuwa na maendeleo kama watu wake hawana Afya njema, au muda wote wapo wagonjwa, kwani unapoumwa, nguvu kazi na utendaji kazi hupungua. Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano kuhusu Tanzania ya Viwanda, ni lazima tuhakikishe wanajamii wanakuwa na Afya bora itakayowawezesha kushiriki kwenye kutekeleza majukumu yao, timu ya Dudumizi technologies, kwa kushirikiana na timu ya madaktari (Specialists) na wataalamu wengine wa Afya, imezindua mtandao utakaokuletea makala, taarifa, habari na Majibu juu ya maswalii mbalimbali ya Afya. Unaweza kutembelea Website https://tanzmed.co.tz iwe kwa simu, laptop au kifaa chochote. Application ya tanzmed.co.tz itazinduliwa siku si nyingi.

TanzMEd inakuletea taarifa zote muhimu za afya kiganjani mwako, kwa kutumia TanzMED unaweza kupata taarifa za Afya, kujua hospitali ipi ipo karibu nawe, kuuliza maswali moja kwa mmoja kwa madaktari na mengine mnengi kuhakikisha unapata Afya Bora.

Read more ...

Kwa wengi wanaoanza kwenye ulimwengu wa Website, kuna misamiati mingi sana utakuwa unakutana nayo. Na kwa mazingira ya Tanzania, kupata taarifa hizi kwa lugha rahisi kwani hata wengi wanaoandika, huandika makala nzito kwa watu wenye uelewa tayari na kuwasahau wanaoanza.

Ingawa si lazima ujue misamiati yote ya Website na Website Design, ila ni vyema ukawa na uelewa wa baadhi yake. Habari njema ni kuwa, Dudumizi kama Website Design Company hapa Tanzania tunakuletea makala mbalimbali zitakazokujengea ufahamu wa masuala ya Website.

Website ni nini

Website ni mjumuiko wa mafaili kwenye mtandao (World wide Web) , kwa wengi wanavyoujua kama Internet. Chukulia mfano wa vitabu kwenye shelfu. Vile vitabu ndiyo vinaitwa Website, kwani kwenye kila kitabu kutakuwa na taarifa nyingi nyingi kwa kila kurasa (Hii inafananishwa na kurasa za Website, Web Pages). Ili uweze kuwa na Website iliyokamilika, lazima uwe na vitu vingine kama Web Hosting na Domain Name, hii ni sawa na Shelfu la vitabu na jina la kitabu.

Kwenye Website, taarifa huandikwa na lugha nyingi za Web, mara nyingi lugha zinazotumika ni kama HTML, CSS na Javascript. Lugha hizi hutoa maelekezo kwa browser (Google Chrome, Mozila Firefox, Internet Explorer nk) ni jinsi gani hiyo Website ionekane na ifanyeje kazi. Muandishi atatumia lugha hizo kuwakilisha vitu tofauti, kama ilivyo kwenye vitabu tunavyotumia. mwandishi wa kitabu cha Ngoswe ni tofauti wa kile cha Kuli.

Domain Name

Watu wengi wamekuwa wakichanganya Domain Name na Website, hivi ni vitu viwili tofauti. Ili mtu aweze kufungua Website yako, anahitajika kuandika jina la Website kwenye browser (Domain Name). Hapo awali kabla ya matumizi ya Domain Name kuanza, hakukuwa na majina ya Website, bali watu walitumia namba za utambulishi wa kifaa kwenye Internet (IP), mfano ukitaka kufungua website ya Dudumizi.com ulitakiwa uandike 123.456.789.101. Sasa, baada ya kuona ni ngumu kukariri hizi namba ndipo walipoamua kuja na majina ya Website.

Kwa kawaida, huwa ina sehemu mbili, sehemu ya kwanzani TLD na sehemu ya pili ni Jina halisi, TLD (Top Level Domain) ni kama .co.tz, .com, .or.tz nk, wakati jina lenyewe ni kama Dudumizi, Michongo nk, hivyo ukichanganya ndiyo unapata dudumizi.com michongo.co.tz nk kutegemeana umechangua TLD ipi. Hiz TLD hutofautiana kulingana na matumizi na pia wapi zimetolewa. Unaweza kupata maarifa zaidi ya Domain kwenye hii makala Mazingatio 10 Juu Ya Majina Ya Website

Web Hosting

Website Hosting ni kama vile nafasi uliyokodi kwa ajili ya biashara. Mfano unapokodisha nafasi mara nyingi unakuta hakuna kitu, hakuna shelfu wala viti. Ni sawa na Hosting, unaponunua Website Hosting usitegemee kuwa tayari ina Website iliyokamilika. Utahitajika ama utengeneze mwenyewe ama ukubaliane na aliyekuuzia nafasi akutengenezee, sawasawa na maisha ya nje ya Website.

Bila Website Hosting, hakuna kitakachoendelea na hautoweza kufanya lolote kwakuwa mafaili yako hayatokuwa na sehemu ya kukaa na watu waweze kuyaona.

Neno la kumalizia;

Kwa maelezo ya juu, utaona kuwa, Website, Domain Name na Website Hosting ni vitu vinayoshirikiana. Unavihitaji vyote ili Website yakoiwe hewani na kuonekana na watu wote Tanzania na Dunia kwa ujumla (Internet). Domain Name litaiita Website ambayo ina makazi kwenye Website Hosting. Na pale mtu anapobonyeza www.dudumizi.com basi mafaili yaliyo kwenye Website yatafunguliwa kulingana na jinsi ilivyotengenezwa.

Ukiwa na swali lolote kuhusu Website Deisign, Website Hosting na Domain Name Registration ikijumuisha .tz domain name, usisite kuwasiliana nasi Dudumizi.com

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe

HAPPY CUSTOMERS & PARTNERS FROM SMEs TO ENTERPRISES

 

We do not just build software, we help companies in their digital transformation challenges.

Call us now