Katika kuhakikisha tunawashirikisha bloggers wa Tanzania kutumia website zao kutengeneza kipato, timu ya Dudumizi, inakuletea DuHosting Affiliate program, ni program ambayo inakuwezesha kuingiza kipato kwa kuweka banners za Dudumizi kwenye blog yako.

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili halafu utaactivate Affiliate program na kuanza kuweka banners zinazoendana na blog yako, basi System zetu zitaweza kukutambua,na kama kuna mtu ananunua huduma yoyote kupitia blog yako, basi utaweza kupata kipato.  Hii pia inajumuisha hata kwa mitandao jamii.

Video ya jinsi ya kujiunga na Affiliate inavyofanya kazi.

Katika kuongeza hamasa ya matumizi ya domain names, haswa kikoa cha .tz, rasiji ya .tz (.tz domain registry), imeandaa wiki ya .tz. Wiki huu huazimishwa kwa semina pia kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya jinsi gani ya kuhakikisha WaTanzania wanaifahamu na kutumia domain za .tz.

Mwaka huu, mawakala wa .tz ambao ni Dudumizi Technlogies LTD pamoja na Extreme Web Technology, wamechagualiwa kuwakilisha mawakala wengine katika kutoa mada juu ya .tz.

Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuliwa na washika dau mbalimbali wa .tz wakiwemo, wafanya biashara, taasisi binafsi na za uma, mawakala na wengine wengi. Maadhimisho hayo yamefunguliwa leo tarehe 12/6/2017 jijini dar es Salaam katika hoteli ya New Africa na yataendelea hadi siku ya ijumaa tarehe 15/6/2016 ambapo itakuwa ni kilele chake na kuzinduliwa kwa karibu poral. Kilele hicho kitakamilishwa kwa uzinduzi wa Website kwa ajili ya huduma za Domain na Hosting ambapo itazinduliwa na Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kasim majaliwa huku ikienda sambamba na majadiliano pamoja na mada zitakazofanyika katika ukumbi wa msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Dudumizi akiwa pamoja na Afisa Huduma kwa Wateja walihudhulia na kuiwakilisha vyema Dudumizi. Fuatilia kwenye picha.

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua mambo ya kuzingatia kwenye usalama wa tovuti

Wawakilihi wa Mawakala wa .tz walifuatilia maswali toka kwa washiriki

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi mendaji wa rajisi ya .tz

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi mendaji wa rajisi ya .tz

Mtaalamu wa masuala ya Domain na huduma kwa wateja kutoka Dudumizi, bi Lucy Vicent mbele ya bana ya Dudumizi

Mtaalamu wa masuala ya Domain na huduma kwa wateja kutoka Dudumizi, bi Lucy Vicent mbele ya bana ya Dudumizi

Washiriki wa siku ya .tz wakifuatilia mada kwa umakini

Washiriki wa siku ya .tz wakifuatilia mada kwa umakini

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua historia ya Domain na Website

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua historia ya Domain na Website

 Mr Nyoni akifafanua umuhimu wa matumizi ya domain name za kikao cha .tz kwa afya ya uchumi

Mr Nyoni akifafanua umuhimu wa matumizi ya domain name za  kikao cha .tz kwa afya ya uchumi

 

 Makamilisho ya utoaji mada kutoka kwa kampuni ya Dudumizi

Katika siku za karibuni, tumefanya maboresho ya kimfumo na kimuonekano katika Website ya Dudumizi Hosting (DuHosting). Muonekano huu ni muhimu katika kuendana na falsafa ya ubunifu na pia, kuendelea kutoa support kwa matumizi ya kikoa cha .tz. Website yako ya Hosting sasa itapatikana kwa www.duhosting.co.tz badala ya dudumizi.net ingawa watembeleaji wa Dudumizi.net watapelekwa kwenye website mpya moja kwa moja.

Katika mabadiliko haya , pia, tumemleta kwenu Dugon, Dragon aliyebeba umbo na maana nzima ya DuHosting. Lengo kuu ni kuweza kutumia myama huyu kufikisha ujumbe ikiwemo spidi, usalama, uhakika, upendo nk.

Katika maboresho haya, sehemu zifuatazo zimeboreshwa

1. Muonekano wa kurasa ya kwanza umeboreshwa, haswa kwa watumiaji wa simu, sasa utaweza kuweka order moja kwa moja
2. Kuongezwa kwa jukwaa la support ambapo unaweza kuuliza swali na kujibiwa na watu wengine akaweza kufuatilia

Muonekano wa Website Design and Hosting Support

Muonekano wa jukwaa la Support kwa wateja


3. Kuboreshwa kwa kurasa za ndani, mfano kuongezwa kwa kurasa za historia ya DuHosting

History for Website Hosting Company in Tanzania


4. Maboresho ya muonekano wa order kutoka kurasa wa kwanza kabisa

Cheap Website Design and Hosting Tanzania
Plan za Website Hosting, Serengeti sasa ipo kurasa ya mbele

5. Maboresho mengine mengi ya kimfumo

Ni mategemeo yetu sasa utafurahia matumizi ya tovuti yako pendwa.

Katika dunia ya mawasiliano ya leo, kama ilivyo kwenye Website, Hosting au hata Application za simu, karibu kila mtumiaji wa mtandao ni vigumu kuepuka kutumia email. Wengi tumekuwa tukitumia njia tofauti katika usomajiwa email, kuna wanaosoma moja kwa moja kwa kutumia browser na kuna wanaotumia application za simu au computer kama outlook kusoma na kutuma email. Kwa sasa, kuna njia kuu kubwa mbili zinazotumika kupokelea email, kutoka kwa aliyekutumia mpaka unapoipata, nazo ni POP na IMAP, njia hizi zinakuwezesha kupokea email muda na kimfumo utakao.

Kabla haujaanza kufanya setting kwenye application yako na kuharibu mambo, hakikisha unaangalia kama setting za awali (Default setting) kama hatitoshilezi kufanya kazi  unayotaka kwa sababu, mara nyingi setting hizi za awalu huwa zinakidhi mahitaji na mabadiliko yoyote yanaweza kukusababishia usumbufu. Makampuni mengi yanayotoa huduma ya Website na email Hosting (Dudumizi ikiwemo mojawapo), wamekuwa wakikuwezesha kutumia njia mbalimbali kupokea email. Hivyo chaguo la ipi ya kutumia ni lako mwenyewe.

Matumizi ya POP3

Kama jina lake linavyojieleza (Post Ofice Protocol), ni njia inayokuwezesha kupokea email kama posta inavyofanya kazi, email zinakuwa zinapita kwenye seva (posta) na kwenda moja kwa moja kwa mteja bila kuacha nakala kwenye seva (kama unavyochukua barua yako kutoka posta, hivyo posta ni sehemu ya kupitishia na kukaa kwa muda tuu). Hivyo, unaweza kutumia simu au computer kusoma email ambazo zimepakuliwa na zitaendelea kubakia kwenye kifaa chako na siyo kwenye seva, hii ni kwa sababu, kwa mara nyingi (siyo zote), email hufutwa punde tuu baada ya kupakuliwa na kufikishwa kwenye kifaa cha kusomea hivyo, hakuna email inayobakia kwenye seva.

Pia, pindi unapotuma email, email zilizotumwa (Sent items) hubakia kwenye kifaa na si kwenye seva hivyo kama ukibadilisha kifaa bila ya kufanya backup, unaweza kupoteza taarifa zote za awali. Kuna setting unaweza kuzifanya kubakisha email kwenye seva kwa kutumia POP3, lakini hii si chaguo la awali (Default) na mara nyingi halijulikani kwa wengi.

Faida:

 • Si lazima uwe na Internet kusoma email zilizopakulia
 • Urafagha zaidi kwa wenye hofu kubwa ya privacy
 • Haraka kusoma email kwa sababu hakuna kupakua tena

Hasara:

 • Uwezekano wa kupoteza email zote pindi kifaa kinapoibiwa
 • Gharama huongezeka kwa sababu uhifadhi (storage) ya vifaa ni ghali kuliko ya seva
 • Ni ngumu kutumia kwa vifaa zaidi ya kimoja
 • Uwezekano wa kupoteza taarifa ni mkubwa

Matumizi ya IMAP

IMAP inasimama badala ya Internet Message Access Protocol, ambapo ilianza kutumia rasmi mwaka 2013, IMAP ikiwa tofauti na POP3, inayo uwezo wa kukuwezesha kusoma email kwenye vifaa zaidi ya kimoja. Email zote zinazotumwa na kupokelewa hubakia kwenye seva,vifaa (simu, lapop nk) hutumika tu kwa ajili ya kusomea emails.

Kwakuwa email zinakuwa kwenye seva, pale unapotaka kuzisoma, vifaa hivyo hupakua email na kuhifadhi kwa muda kwenye simu, na unapomaliza kusoma huzifuta kutoka kwenye simu yako baada ya muda fulani, mara nyingi ni wiki moja au mbili ingawa huhifadhi vichwa vya emails (header) na siyo vipachiko (attachments)

IMAP inawafaa sana wale wanaofanya kazi mazingira yenye Internet ya uhakika, pia wana mawasiliano ya mara kwa mara ya email.

Faida

 • Ni ngumu kupoteza email
 • Gharama inakuwa chini kwa sababu kuhifadhi kwenye seva ni nafuu
 • Uwezekano wa kupoteza ni mgumu kwakuwa email seva huwa zina ulinzi mzuri

Hasara

 • Lazima uwe na Internet ili kusoma na kutuma email
 • Kama ukihost kwa watoa huduma wasio waaminifu, ni rahisi email zako kudukuliwa

POP3 Au IMAP?

Chaguo lipi ni sahihi kwako, linategemeana sana na jinsi gani unavyotumia emails na mazingira yako ya kazi. Kama unatumiwa sana email kubwa ambazo zinavipachiko na ungependa kuzitumia popote ulipo hata kama hauna Internet, basi POP ni chaguo sahihi kwa sababu utatumia email kama kifaa cha kuhifadhia (storage) na kusizoma popote ulipo hata kama hauna Internet.

Ila kama unatumia email mara kwa mara na email zenye taarifa za kawaida au unatumia kifaa zaidi ya kimoja kusoma email (simu na computer), basi IMAP ni chaguo thabiti.

 

Katika siku za karibuni, tumesikia habari kuhusu tishio la usalama wa watumiaji wa kompyuta za Windows. Tishio hili limekuja kutokana na kusambaa kwa minyoo inayobeba udukuzi wa ransomware. Udukuzi huu umeshambulia sehemu nyingi duniani (Tanzania, haswa dar es Salaam ni mojawapo), ila nchi zilizoathirika sana ni zile nchi zilizoendelea kwakuwa wao wamekuwa wakitegemea sana matumizi ya kompyuta kwenye kila shughuli. Kama ilivyo ada yetu, tukiwa kampuni inayoongoza kwa Website design na Website Hosting Tanzania, ambapo zote zinahusika na matumizi ya kompyuta, tunakuletea ufafanuzi wa kina utakaokuwezesha kufahamu kiundani udukuzi huu na jinsi ya kujikinga.

Idara zaidi ya 48 huko Uingereza, kampuni za FedEX, Telefonica, renault na Nissan ni mojawapo ya zilizoathirika na udukuzi huu, pia inasemekana Idara za serikali za Urusi na ATM nyingi China nazo zimekuwa wahanga wa shambulio hili, kiufupi kompyuta na seva zaidi ya 200,000 duniani kote zimeathiriwa hata kuppelekea baadhi ya nchi kama Uingereza kusitisha baadhi ya huduma za Afya kutokana na kompyuta kushambuliwa zaidi.

Ushambulizi huu umesababishwa na mfumo wa kuvamia kwa watumiaji wa kompyuta unaojulikana kama Ransomware. Ransomeware ni suhambulizi wa kompyuta kwa kumzuia mtumiaji kutumia kompyuta mpaka atakapofanya tukio linaloamrishwa na mvamizi Utekaji wa kompyuta(Compyuta kidnaping).

Wadukuzi wa The Shadow Brokers wameiiba programu hii kutoka Shirika la Usalama wa Marekani (NSA)  ambalo moja ya kazi zake ni kufuatilia na kuchunga usalama wa kimtandao. NSA hutumia programu hizi kudukua na kupata umiliki wa kompyuta za magaidi, lakini mwezi April programu hiyo iliibiwa. Wadukuzi hao waliamua kuiweka kwenye mtandao bure kwa lengo la kuonesha kutokukubaliana na raisi Dornald Trump. Wadukuzi wakaitumia program hiyo yenye kuweza kushambulia kompyuta zenye Windows, ushambulizi (exploit) ambao ulipewa jina la EternalBlue na kampuni ya Microsoft. Ushambulizi huu, hutumia minyoo (worms) na kutengeneza aina ya Ransomware inayojulikana kama WanaCrypt0r 2.0, Wanacry au Wanacrypt au Wcry ambao husambaza ransomware kwa njia ya email zenye mtego /kugushi (phishing) ambapo huonekana zinatoka kwa mtu mwenye nyadhifa (kama bosi wako)  kumbe sivyo.

Kama ilivyo matoleo mengine ya ransomware, Wannacry ransomware inatumia udhaifu uliopo kwenye kompyuta nyingi zinazotumia Windows. Shambulio hili jipya, limepelekea kampuni ya Microsoft inayotengeneza mitambo endeshi ya kopyuta (Operating Systems) aina ya Window kutoa kiraka (pacth) kwa ajili ya matoleo hata yale ya zamani (kama Window XP, Windows 7, Windows Server 2003 na mengine), hivyo kama bado haujaupdate Windows yako, wakati ni sasa kuziba kiraka.

Kiufupi, Wannacrypt husambazwa kwa njia ya Minyoo (Worm) kutoka kwenye kompyuta iliyoshambuliwa kwenda kwenye kompyuta nyingine yao yenyewe (automatically), kusambaa na udukuzi huu huwezeshwa kupitia udhaifu (Vulnerability) uliopo kwenye sehemu ya operating system ya windows (SMB file Sharing). Ingawa udhaifu huu ulishapatiwa kiraka na kutatuliwa kwenye kiraka kilichotolewa Mwezi wa tatu, lakini kuna watu wengi bado hawakuupdate, haswa wale wanaotumia Windows zisizo halali au zile za zamani kama XP, Windows 7 na nyinginezo.

Baada ya kushambuliwa, programu hii huzuia muhusika huambiwa mafaili yake yamefungwa (encryted) na hupewa siku ambapo unatakiwa kulipia la sivyo basi mafaili yatafutwa. Malipo hayo yanatakiwa kufanyika kwa njia ya pesa ya kidigitali (Bitcoin), muhusika hupewa utaratibu wa jinsi ya kukamilisha malipo ikiwemo anuani ya malipo.Kwa wasiofahamu, Biticoin ni aina ya pesa kwa njia ya dijitali ambayo huwezesha kutuma na kupokea pesa bila kujulikana (Annonymously).


Ransomware hufanya nini

Ransomware hutofautiana, lakini zote zinafanana kwenye kitu kimoja, humzuia mtumiaji kutumia kompyuta, Ransomware hukutaka kufanya kitu fulani kabla ya kukuacha kutumia kompyuta. Shambulio hili huathiri aina zote za PC za Windows zenye udhaifu (Vulrnerable), iwe ni kwa ajili ya binafsi, iwe seva nk.

udukuzi wa ramsomware huweza kufanya yafuatayo;

 • Kukuzuai kutumia kompyuta mpaka ufanye malipo (Na Wannacrypt imejikita hapa)
 • Kuencrypt mafaili na kuyafanya yasitumike tena
 • Kuzuai baadhi ya application kutofanya kazi (mfano ni browser ya kompyuta nk)

Ransomware hukutaka kulipa kiasi fulani cha pesa, haswa kwa njia ya mtandao ili kukuwezesha kutumia kompyuta yako, ingawa hakuna uhakika kama baada ya kulipa utaweza kutumia kompyuta yako kama ilivyokuwa awali.

Jinsi Ushambulizi unavyotokea

Kama tulivyoona hapo juu, udukuzi huu wa Wannacry ransomware hutumia minyoo kusambaa kutoka kwenye kompyuta iliyoatthirika kwenda kwenye kompyuta nyingine zilizounganishwa na network. Sifa kuu ya minyoo ya kompyuta ni uwezo wake wa kusambaa kwenye Network, tofauti na Virusi, Minyoo husambaa bila kubonyezwa (clicked), hivyo inahitaji mtu mmoja tu kwenye network awe ameathirika, basi minyoo itasambaa kwa watu wengine wote.

Kompyuta huweza huathirika na ransomware kwa moja kati ya njia zifuatazo;

 • Kutembelea Website zisizo salama, zenye walakini au zisizo za kweli
 • Kufungua vipachiko au email kutoka kwa watu usiowajua au usiowategemea (mfano risiti ya malipo, picha za warembo nk)
 • Kufungua linki zisizo salama kwenye email,Facebook, Twitter na mitandaomingine ya kijamii au programu za mawasiliano kama Skype.

Nini Cha kufanya

Kimsingi, ni kazi ngumu sana kurudisha kompyuta iliyoshambuliwa na ransomware, haijalishi ni aina gani ya Ransomware, iwe Wannacry au nyinginezo. Hivyo, njia bora kabisa ni kujikinga na udukuzi na kuhakikisha unakuwa makini pindi unapotumia mtandao.

Hakikisha unazingatia;


 • Kuhifadhi (backup) ya mafaili yako kwenye sehemu tofauti isiyo na muunganiko na kopyuta yako ya sasa. Hii itakusaidia kurudisha mafaili punde unapovamiwa
 • Usibonyeze (click) link yoyote kwenye Website au email mpaka uwe na uhakika wa hiyo linki na muhusika unamjua
 • Kama una mashaka na linki yoyote, usibonyeze
 • Kama Website ina mambo mengi muhimu au inahitaji taarifa fulani, hakikisha Website ina alama ya https, mfano https://dudumizi.com au https://dudumizi.net
  Usifungue email zisizo rasmi, mara nyingi emails zisizo rasim huwa na majina yasiyoeleweka au yaliyokosewa au yaliyoongezwa, mfano This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. (hapa wameacha i kwenye zi)
 • Hakikisha unatumia antivirus na ipo updated
 • Hakikisha unakuwa makini kwenye kufungua kipachiko inayotoka kwa mtu unayemfahamu, kwakuwa wavamizi huweza kutumia ulaghai wa email (phishing email) na kuonesha inatoka kwa bosi wako kumbe siyo
 • Hakikisha kompyuta yako imepachika viraka (patches) vyote muhimu kutoka Microsoft
 • Jengwa utaratibu wa kuandika link kwenye browser badala ya kubonyeza zilizopo kwenye emails
 • Jaribu kurepy email ili uone kama inaenda kwenye email iliyojia, kama sivyo basi kuna walakini

Je udukuzi wa Wannacry umezuiliwa?

Kwa bahati nzuri, mtaalamu wa masuala ya usalama wa Uk aligundua uwepo wa swichi ya kuzima kutapakaa kwa udukuzi wa Wannacry ndani yake. Swichi hii imeunganishwa na jina la Website (iuqerfsodp9ifjaposdfjhgosurijfaewrwergwea.com) ambalo hufanya programu kuacha kusambaa pindi inapoona jina hilo la website lipo hai (active). Baada ya kusajiliwa kwa jina hilo (domain name), ransomware iliitambua na kuacha kusambaa.

Jina hili la website limeunganishwa kwenda kwenye seva maalumu ya majina (DNS) iliyopo marekani, seva hii ni maalumu kwa ajili ya kutoa majibu hewa kwa lengo la kuzuga wahusika (sinkhole). Tayari IP za seva hii zipo kwenye uchunguzi wa FBI na seva kivuli imeshatengezwa kwa ajili ya kupokea taarifa ili zitumike kutambua walioathirika na kuwataarifu kama itahitajika.

Ingawa kuna taarifa zinazokinzana juu ya uwepo wa swichi kwenye Wannacry ambapo mmoja wa hackers wanaotambulika sana  kuja na uwepo wa swichi tofauti na mashambulio mapya, hivyo hali bado haijatengemaa kama inavyosemekana ingawa imepungua.

 

 

Nini tutegemee

Kama tulivyoeleza hapo juu, kilichofanyika ni kuzuia kuendelea kwa kusajili Domain, hivyo tutegemee muda wowote kuanzia leo Jumatatu kulipuka upya kwa aina nyingine ya ushambulizi baada ya wahusika kubadili swichi ya kuifunga programu na kuanza kutapakaa tena. Hivyo hakikisha unafuata hatua bora za utumiaji kama tulivyoainisha hapo juu.

Microsoft wanajiandaa kuja na Aptch kwa matoleo yote ya awali hata yale waliyositisha kuyapa support, hii ni kwa sababu, inaonekana idara nyingi, haswa za serikali na Afya bado wanatumia matoleo hao. Hii ni kwa sababu ya muingiliano wa programu na taratibu za kuhamia matoleo mapya.

Kwa watumiaji wetu wa Dudumizi, seva zetu bado zipo salama na tutaendelea kuwataarifu pindi kutakapojitokeza tishio lolote la kiusalama. Pia, tunawashauri wamiliki wa Website kutumia https kwenye Website zao. Dudumizi.net inatoa huduma hii kama kipachiko kwenye Website Hosting. Tafadhali wasiliana nasi kwa maelezo zaidi. 

Kusoma zaidi:

Dudumizi imekukusanyia linki zenye uhusiano zaidi juu ya makala hii ambapo utapata uelewa wa kutosha.

http://www.bbc.com/news/health-39904851

https://blog.comae.io/wannacry-new-variants-detected-b8908fefea7e

https://twitter.com/msuiche

https://www.theregister.co.uk/2017/05/14/microsoft_to_spooks_wannacrypt_was_inevitable_quit_hoarding/

http://www.telegraph.co.uk/news/2017/05/12/russian-linked-cyber-gang-shadow-brokers-blamed-nhs-computer/

http://www.bbc.com/news/technology-39920269

 

Kama wewe ni muathirika au una mchango, tafadhali changia makala hii ili kuwashauri wengine.

 

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe
Call us now