Kufanya Update ya Website ni kitu cha muhimu kwa website Designer au mmiliki yoyote. Siku hizi, utengenezaji wa Website umerahisishwa sana. Wengi wanapendelea kutumia Content management System (CMS) kama Joomla, Woordpress au Drupal kutengenezea Website.

Uzuri wa kutumia CMS ni kuwa, kuna wachangiaji wengi ambao huangalia utendaji na uboreshaji wa kimfumo na kiutendaji. Hii hupelekea kuhitajika kwa update za mara kwa mara. Updates hizi huwa ni za kiusalama (Security fix), kiuboreshaji (Optimization) au kurekebisha tatizo (bug fix) linaloweza kupunguza utendaji wa Website. Hakikisha unajiunga na mlisho wa makala kutoka Joomla ili kupokea taarifa juu ya maboresho haswa yale ya kiusalama.

 Kwa kawaida hapa Dudumizi, tunawataka wateja wote wanaofanya Website Hosting, kuhakikisha Website zao zinatumia version mpya kabisa. Na pia, kama ni mmiliki wa website, hakikisha una mtaalamu wa IT ambaye atakusaidia kuifanyia maboresho ya mara kwa mara.

Video hii, itakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kufanya update kwenye Joomla Website, iwe ni ya Core Joomla au Extensions za Joomla.

APE Network, ni kampuni ya Kitanzania inayojihusisha na Uchapishaji wa vitabu pamoja na kazi mbalimbali zenye malengo ya kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Katika moja ya hatua zake, kampuni hiyo ilitengeneza Application ya simu kwa watumiaji wa Android. Application hii ilikuwa inawawezesha watumiaji kujifunza na kusoma kazi mbalimbali za kiswahili kama Misemo, methali, nahau na Vitendawili ambayo inajulikana kama Swahili Sayings (Misemo ya Kiswahili)

Application hii imepokea muitikio mzuri kutoka katika jamii ya watumiaji wa Kiswahili kwenye mtandao,  watumiaji wengi wamekuwa wakitoa maoni chanya juu ya kazi hii. Ingawa Application hii ilikua na vitu vingi vizuri, lakini pia ilikuwa inahitaji maboresho zaidi ili kuifanya iendane na mahitaji na mabadiliko ya tabio za watumiaji, haswa kimuonekano (User Interface), muingiliano na mtumiaji (user engagement) na machaguo ya mtumiaji (user selection) na pia kuongeza mvuto wa kwa mtumiaji ili aendelee kuitumia tena na tena.

Ili kuboresha hili, timu ya APE Network, iliitafuta Dudumizi Technologies LTD, ili kuangalia ni jinsi gani inaweza kuboresha Mobile Application yake na kuifanya iwe bora zaidi. Kama ilivyo kawaida yetu, tulitumia muda mwingi kuisoma na kuielewa, ili kuja na features zenye kutatua tatizo lililopo.

Timu ya Dudumizi kwa kushirikiana na Mkurugenz wa APE Network (mr Hermes Salla) tumeweza kukamilisha Application bora kabisa ya Kiswahili Duniani ambayo sasa inapatikana kwenye Playstore 

Features:

 • Kusoma Misemo, Methali, Nahau na Vitendawili
 • Kusikiliza Misemo, Nahau, Methali na Vitendawili kwa sauti
 • Uwezo wa kutuma maoni (comment) 
 • Uwezo kugawana (share) na wengiine
 • Uwezo wa kushiriki kwenye mijadala
 • Uwezo wa kuhifadhi taarifa uzipendazo
 • Uwezo wa kuona picha kulingana na aina ya taarifa

Tulichokifanya (what we have done)

 Muonekano wa App kwa picha

Muonekano wa mbele wa Application ya Swahili Sayings

Jinsi taarifa zinavyoonekana, sauti, picha na hata maoni

 

Unaweza kutuma maoni na ukafuailia ya wengine

Baadhi ya features kwenye menu ya Swahili sayings

Na mengine mengi yanapatikana kwenye Swahili sayings, Pakua App hii kutoka Playstore, pia kwa mahitaji ya App Development Tanzania, tuandikia kwa ajili ya kukutumia Free Quotation hapa

 

Katika siku za awali, timu ya Dudumizi tukiwa moja ya .tz Domain Registrar chini ya tzNIC, tulitengeneza video iliyokuwa inaelezea jinsi ya kutumia command kusajili Domain ya .tz ka maregistrar. Video hii ilikuwa na msaada mkubwa kwa registrars wengi kwa kuwawezesha kuhamisha maarifa kwa wafanyakazi wapya. Tumekuwa tukipokea maoni na pongezi nyingi kutoka kwao.

Katika kuhakikisha tunaongeza matumizi ya .tz domain kwa Watanzania wengi zaidi huku tukiwasaidia ma registrar ambao hawana uwezo wa kufanya automation, timu nzima ya Dudumizi tumedevelop module kwa ajili ya WHMCS (System inayotumika kwa ajili ya Hosting).

Module hii inakuwezesha kufanya mambo mengi kama kusajili domain, kurenew domain, kuhamisha domain, kubadili name server na mengine mengi.

Je unaipataje DuConnect?

Kumbuka, DuConnect ni kwa ajili ya maregistrar pekee, hivyo kabla ya kuitumia hii ni lazima uwe umehakikiwa na tzNIC, unatakiwa uwe na akaunti pamoja na SSL Certificate.

Grama za DuConnect

Setup fees 250,000TZS

Gharama ya kila mwaka 50,000TZS

Gharama hizi zinakuja na Support pamoja na Updates kwenye Module zote mbili.

Auangalia video ya jinsi gani DuConnect inavyofanya kazi

 

Are you ready to take next step with DuConnect Get it now

 

Mtumiaji wa website huwa anatumia dakika zisizozidi tano katika kutafuta kilichomplekea kwenye Website, hivyo ukiwa kama Website Designer unatakiwa kuhakikisha unatumia muda huo ipasavyo kuwafanya watembeleaji kuendelea kubakia kwenye Website yako. Siku hizi tumeshaachana na ule mtindo wa kuwa na mlundikano wa vitu kwenye kurasa za mbele za website, vinapokuwa vichache zaidi basi ndiyo ubora wake.

Katika kuhakikisha tunaongeza mvuto huku tukiwarahisishia wateja kupata picha na vitu vyote wavitakavyo kwenye kurasa moja, Dudumizi tumefanya maboresho ya kimuonekano na mfumo kwenye website yetui. Katika maboresho haya, mambo yafuatayo yameboreshwa;

 • Kutumiwa kwa Video badala ya picha, kwa ushurikiano na partners wetu, tumeweza kupata Video yenye kuendana na matakwa ya Dudumizi
 • Kutumiwa kwa icons badaya ya maneno ili kujenga mazoea kwa watumiaji
 • Matumizi  ya mitandao ya uhifadhi ili kuboresha speed
 • Muonekano wa kazi umeboreshwa na kuondoa kazi zilizopitwa na wakati
 • Muonekano wa kwenye simu nao umeboreshwa

Munonekano wa huduma za Dudumizi kwenye simu

 

Muonekano wa mbele wa Dudumizi

 

Siku za karibuni, Dudumizi tulipokea maombi kutoka kwa kampuni ya 4 Bell inayoandaa matembezi ya Bagamoyo Historical Marathon wakiwa na kusudio la kutengeneza Website kwa ajili ya tukio hilo la Marathon (Marathon Website Design), na moja ya matakwa yao ni kuwawezesha watumiaji kujisajili na kufanya malipo online haswaa kwa kutumia njia za simu kama mpesa na Tigopesa. Muda ulikuwa mfupi, huku kukiwa na hitaji la integration ya payment jambo ambalo linahitaji umakini na kutokukosea.

Kama ilivyo ada yetu, timu nzima ya Dudumizi ilihakikisha inafanya kazi kwa kutumia maarifa yote mpaka Website inakuwa hewani. Na mnamo, Julai 27, tulikamilisha kazi na sasa Website ip hewani kwenye link https://bagamoyomarathon.co.tz

Features:

 • Online Marathon registration
 • Pesapal Payment Integration
 • Registrants Management
 • Registrants Export
 • Marathon Gallery
 • News/Blog

What we did:

Read more ...

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe
Call us now