Katika dunia ya leo ya mapinduzi ya Internet, website, Application za simu na hata mifumo ya komputa (Systems), vimekuwa ni nyenzo thabiti katika maisha ya binadamu. Wengi wetu tumekuwa tukitumia mifumo hii bila kujua jinsi inavyofanya kazi au ni wapi inapokaa. Ingawa kwa mtumiaji, hiyo si kitu muhimu, muhimu ni kuwa, inapatikana pale anapohitaji. Ila, upatikanaji huu huweza kuathiriwa na wapi mifumo inakaa. Na, kitendo cha kuwezesha mifumo hii kupatikana kutoka pale inapokaa, ndiyo tunayoiita Hosting, ama wengi wanavyoita Webste Hosting. Website Hosing, imegawanyika katika makundi mengi sana, kuna Shared, VPS, Dedicated Server au Cloud Hosting.

Kwa Tanzania, watumiaji wengi hutumia aina ya shared hosting (website zaidi ya moja kuwa sehemu moja), aina hii ya hosting imekuwa na msaada kwa wengi, hii ni kwa sababu ya urahisi wake katika gharama na hata uangalizi wa mazingira ya hosting kwakuwa kama mmiliki wa Website, hauhitajiki kuchunga mazingira hayo bali kwa yule anayetoa huduma (Website Hosting Company), mfano wa watoa huduma ni Duhosting.

Ili kuweza kuelewa, hebu tuangalie aina mbalimbali za Website Hosting.

Dedicated Hosting

Aina hii ya hosting ni ile ambayo, unakuwa na umiliki wa server nzima mwenyewe. Inaweza iwe kwenye sehemu yako (kama maofisi mengi wanavyofanya) au ya kukodisha server online. Aina hii ya hosting huwa tunaifananaisha na mtu kujenga ama kukodisha ghorofa nzima.

Faida ya dedicated server ni kuwa, unakuwa na hazina (resources) za kutosha, pia spidi na usalama unakuwa wa hali ya juu kama utaweza kufanya maboresho ya kiumfumo (optimization) yanayotakiwa.

Aina hii inawafaa sana, makampuni makubwa, watu binafsi wanaotaka kuanza biashara ya Hosting au wale wanaomiliki website zenye mahitaji makubwa ya resources, kama makampuni ya betting.

Hasara zake ni kuwa, unahitaji waangalizi na wataalamu wa kutosha watakaochunga server yako. Pia, gharama zake huwa ni za juu ukilinganisha na aina nyingine za Hosting.

Virtual private Server (VPS)

Aina hii, haina utofauti sana na Dedicated Hosting, kimsingi, VPS hutokea baada ya Server moja kugawanywa (partitioned) kwa kutumia software na kuwa server zisizo bayana (Virtual) zaidi ya moja zinazojitegemea kimfumo. Hivyo, hardware zitakazotumika ni zilezile isipokuwa kwenye software, kila VPS itakuwa inajitegemea kabisa. Hivyo, VPS kuna sehemu inakuwa kama Dedicated Hosting ila kuwa sehemu inakuwa siyo.

Faida kuu ya VPS ni kuwa, ina sifa nyingi za Dedicated ikiwa kama matumizi binafsi ya hazina (dedicated resources) na hata usalama (ingawa kuna mazingira hatarishi huweza kuathiri VPS kutokea kwenye VPS nyingine iliyopo kwenye server moja).

Mfano halisi wa VPS, ni sawa na ndani ya ghorofa moja, litakatwa wings, na kila wing ikawa inajitegemea kila kitu, hivyo kwa watu wa wing ile, wanajiona kama wapo kwenye ghorofa lao wenyewe.

VPS, huwafaa sana watu wenye website zenye kutembelewa na watu wengi (high traffic), mfano, website ya habari/blogs au zile zenye mahitaji maalumu, mfano kwa website zinahitaji kipachiko (extensions) nyingi kuliko zinazopatikana katika mazingira ya kawaida. Pia, aina hii ya Website hosting inawafaa sana watu wenye kuhitaji kuanzisha huduma ya Website Hosting ila hawana mtaji mkubwa kuweza kumiliki Dedicated server, au wale wenye mahitaji maalumu ambapo hawapendelei kuchanganyika na wengine.

VPS, pia inakupa uwezo mkubwa wa kujibrand, hii ikijumuisha kutumia IP na Name Server zako mwenyewe (Dedicated IP). Na pia, unakuwa na uwezo wa kuinstall program nyingi. Ingawa kuna baadhi ya program, hauwezi kuinstall kwenye VPs kama, VPN (Virtual Private network) Server.

Tofauti ya VPS na Dedicated server huwa kwenye utendaji kazi na hata ukuaji, mfano, ukiwa na Dedicated server na ujazo (storage/space) ikawa imejaa, ni rahisi kuongeza ujazo bila kuhama, kitu ambacho si rahisi kwa VPS za kukodisha.

Shared Hosting

Shared hosting ni aina ya Hosting ambayo ndani ya server moja, huhost website zaidi ya moja na website hizi hugawana hazina (resources) zilizomo. Kwa, shared Hosting nyingi, kila website inayo uwezo wa kutumia resources zozote zilizomo mpaka zitakapokwisha, hivyo ufanyaji wake kazi hutegemeana sana na jinsi resources hizi zinavyotumika. Na ndiyo maana, kama kuna Website moja inatumia sana resources, huweza kufanya nyingine kuathirika kwa kuwa na spidi ndogo au zisipatikane kabisa.

Shared hosting, unaweza kuifananisha na nyumba ya kupanga ambapo ndani ya nyumba moja, kuna vyumba vingi ambavyo kila kimoja kina mpangaji wake. Hivyo, kama mpangaji mmoja atafungulia redio kwa sauti ya juu, basi wapangaji wengine wote watasikia makelele.

Shared hosting ni kundi ambalo watu wengi huangukia, ni kundi ambalo halihitaji utaalamu mwingi kuweza kulitumia, na hata upatikanaji wake huwa kwa bei nafuu sana. Mfano, Duhosting tunatoa huduma hii kwa kuanzia Tsh5000/= kwa mwezi.

Shared hosting huwafaa sana wale wenye website ndogo au walio na bajeti ndogo ya kuanzia. Ni chaguo la haraka kama ndiyo unataka kuanza safari yako online. Mara nyingi, gharama halisi ya shared hosting hutofautishwa kwa kiwango cha ujazo (Storage/space), mfano 1GB, 2GB nk huku watoa huduma wengi huwa hawaweki ukomo wa mafaili yanayoweza kupita (bandwidth).

Shared hosting ina faida nyingi, kama gharama zake kuwa chini, urahisi wake kwenye matumizi, na pia haihitaji uelewa sana wa uchungaji wa server. Ila, ina hasara zake, kama kutokuwa na uhakika wa resources utakazopewa, spidi kuwa ndogo na hata usalama wake.

Ukiangalia kwa umakini, iwe Dedicated server, VPS au Shared Hosting, matumizi yake na faida hutegemeana na sababu na aina ya website yako. Shared hoting imekuwa ni kimbilio la wengi wakati Dedicated server ni kwa ajili ya wale wanaohitaji hazina ya kutosha. Katika makala zijazo, tutaangalia aina nyingine ya Hosting ambayo leo hatujaigusia, nayo ni Cloud Hosting.

SSL Certificate ni cheti cha kieletroniki chenye taarifa muhimu zinazohusiana na Kampuni au mtu. Pindi funguo zenye taarifa ya cheti hiki zinapofungwa kwenye seva, basi husababisha browser kuonesha alama ya kufuri likimaanisha kuwa mawasiliano yote kati ya seva na browser yatapita kwenye njia salama. Mara nyingi, mtindo huu hutumika sana kulinda taarifa muhimu kama kwenye mabenki, manunuzi ya online na sehemu yoyote online inayopokea taarifa muhimu za mtumiaji.

Kwa siku za karibuni, tumeona ongezeko la matumizi ya SSL Certificates hata kwenye websites za kawaida ambazo hazipokei taarifa za watumiaji. Hii ni kwa sababu, mtandao wa utafutaji wa taarifa za mtandaoni (Google Search Engine) wameweka SSl certificate kama moja ya vigezo vyake katika upangaji wa utafutaji wa taarifa, hivyo watu wengi wameamua kutumia fursa ili kujiweka katika nafasi nzuri ya upatikanaji kwenye mitandao (online visibility).

Je SSL Certificate inatambulisha nini;

Kwenye kila SSl Certificate, kuna mambo vitu viwili

 • Jina la website na seva iliyopo
 • Taarifa za mmiliki (eg jina, aina ya biashara, anuani nk)

Kabla ya kuanza kutumia SSL Certificate, unahitajika kuinstall SSL Certificate kwenye seva. Mara unapomaliza, mawasiliano yote kati ya seva na watumiaji yatapita kwenye njia salama. Moja ya ishara kuwa mawasiliano yanapita kwenye makubaliano yaliyo salama, utaona ile alama ya HTTP imebadilika na kuwa HTTPs, na pia kuna kufuri la kijani kabla ya anuani kuanza. Kuna aina nyingine za SSl Certificate huifanya sehemu yote ya anuani (address bar) kuwa ya kijani na jina la kampuni huanza kutokea kabla ya kuanza kwa anuani.

Muundo wa SSL Certificate;

SSl hutumia kitu kinachoitwa Public key cryptography. Hii ni moja ya cryptography inayotumia namba mbili zinazounda kutokana na msururu wa namba zilizochanganywa changanywa, kwa lugha ya kitaalamu faili hili huitwa funguo(key) kwa sababu ndilo hutumika kufunga na kufungua taarifa kwa mpokeaji. Funguo hizi zimegawanyika katika makundi mawili, moja huitwa funguo ya nje(public key) wakati nyingine huitwa funguo ya ndani (private key). Kimsingi, taarifa hufungwa kwa funguo ya nje, na hufunguliwa na funguo ya ndani, hivyo kama hauna funguo ya ndani, basi hautokuwa na uwezo wa kufungua na kuona ulichotumiwa.

Funguo ya nje hujulikana na server yako ila hutolewa kwa mtu yoyote anayetumia web,na hii ndiyo hutumika kufunga taarifa kabla haitajumwa. Na ile private key hujulikana ndani tuu n, kumbuka, private key hutengenezwa pale unapoanza mchakato wa kutengeneza SSL Certificate. SSL Certificate huanza kutengeneza kwa kukusanya taarifa za umiliki utakaotumika kwenye kutengeneza cheti. Taarifa hizi hujumuishwa kwenye taarifa inayoitwa Maombi ya usainishaji (Certificate Signing Request, CRS). maombi haya hutumika na kujumuishwa kwenye utengenezaji wa SSL Certificate.

Jinsi SSL inavyofanya kazi;

Mfano, Juma anamtumia Yohana ujumbe, basi kwakuwa ufunguo wa nje wa seva itakayopokea taarifa za Yohana unajulikana, basi Juma atafunga taarifa kwa kutumia ufunguo wa nje (public key) wa Yohana na kuituma taarifa. Njia pekee ambayo Yohana atatakiwa kuitumia ili kuiona hii taarifa ni kwa kuifungua kwa kutumia funguo ya ndani (Private key). Kwakuwa ni Yohana pekee ndiye mwenye huu ufunguo wa ndani (private key) basi, ni yeye pekee ndiye atakuwa na uwezo wa kufungua hii taarifa.

Endapo katikati kukatokea hacker ambaye atavamiwa mawasiliano haya na kuiba taarifa kabla hazijafunguliwa na Yohani, hatoweza kuelewa kitu maana atakutana na taarifa iliyofungwa (cryptographic code).

Tukirudi kwenye ulimwengu wa Website, mawasiliano yote hutokea kati ya Website na seva, hapa kwetu, Juma na Yohana ndiyo website na seva zetu.

Kwanini unahitaji SSL Certificate kwa Website ya biashara yako

Ukiacha sababu za kuongeza daraja la website kwenye mitandao ya utafutaji, SSl Certificate ikakusaidia;

 • Kuongeza usalama wa taarifa kati ya mtumiaji na seva
 • Kuongeza uaminifu kwa wateja
 • Kuboresha biashara kwa kuvutia wateja zaidi

Jinsi ya kununua SSL Cerificate (Where to buy SSl Certificate in Tanzania)

Unaweza kununua SSLcertificate kutoka kwa makampuni mengi yanayotoa huduma za Website Hosting na kuinstall kwenye seva yako. Ila, kama ilivyo ada, kununua kutoka kwa makampuni ya karibu hukurahisishia pindi unapokutana na changamoto, pia ni rahisi kwenye njia za malipo maana unaweza kununua hata kwa kutumia malipo ya simu kama Mpesa na Tigo pesa, au hata cash.

Mambo ya kuzingatia kabla ya kununua SSL Certificate

Kuna vitu vya msingi unatakiwa kuzingatia kabla ya kununua SSl Certificate navyo ni;

 • Hosting wako anaruhusu matumizi ya SSl kutoka njia

Kwa wale wanaotumia blogger, hauna uwezo wa kuinstall SSl Certificate iliyonunuliwa nje ya blogger kwa sasa, hivyo ni vyema ukainunua kutoka kwao. Hii pia hutokea kutoka kwa mitandao mingine inayotoa huduma ya free hosting.


 • Aina ya SSL unayohitaji

Kuna aina nyingi za SSl, hivyo ni bora ukajua ni aina gani unahitaji, aina kuu zinazotumiaka na wateja wengi ni kama;

 • SSL Certificate kwa ajili ya Website moja (www na isiyokuwa na www)
 • SSL Certificate kwa ajili ya Website na sub domain zake zote
 • SSL Certificate kwa ajili ya domain zaidi ya moja
 • SSL Certificate yenye mkanda wa kijani (EV)

Pia, ni vyema ukanunua SSL Certificate kutoka kwa makampuni yenye kuaminika. Kwa sasa Dudumizi tunatoa hii huduma, na unaweza kununua SSL Certificate Hapa.

GMail ni moja ya mitandao maarufu na inayotumika na wengi sana kusomea email, wengi wanatumia emails kama  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. , This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. nk. Lakini, kwa wale wanaomiliki kampuni au kufanya biashara, inashauriwa sana kutumia email zenye jina la kapuni na kuwa na email kama This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Kama tulivyoelezea kwenye makala iliyopita Zijue Faida Za Kutumia Email Ya Kampuni Na Siyo Gmail / Yahoo ambapo tulielezea faida za kutumia email ya kampuni kwa njia za mawasiliano, hivyo watu wengi sasa wanatumia email za makampuni yao.

Moja ya changamoto ambayo baadhi yao wamekuwa wakitueleza ni kuwa, wanapenda kuwa na uwezo wa kusoma na kutuma emails zote kutoka sehemu moja, na pia wengi wamekuwa wakisema wamezoea sana muonekano na features za gmail hivyo inawawia ugumu kuanza kutumia application nyingine kama webmail.

Tukiwa kama Top Website Design and Website Hosting Company in Tanzania, tunapendelea kuwarahisishia wateja wetu juu ya utumiaji wa huduma, iwe Website Design, iwe domain registration na hata Website Hosting. Hivyo ni lazima tuhakikishe tunawawezesha wateja wetu kuwa na njia rahisi za kutumia huduma zetu bila kuhangaika. Hii ndiyo sababu ya kuandaa video hii, katika Video hii, utajifunza jinsi ya kutumia gmail kutuma na kupokea emails ulizozihost Dudumizi. Video hii inawalenga wateja wote, wale wa Business email, Mikumi, Kilimanjaro na Plan nyingine.

Video hii itakufundisha jinsi ya kutumia gmail kutuma na kupokea emails kutoka kwenye akaunti yako huku mtu anayepokea anaona email ya kampuni na siyo gmail. Hii ni sawa tu na wale wanaotumia outlook au waliounganisha kwenye simu. Kama bado haujaunganisha kwenye simu, unaweza kuangalia Video Jinsi Ya Kusetup Dudumizi Email Kwenye Simu Za Android

Kufanya Update ya Website ni kitu cha muhimu kwa website Designer au mmiliki yoyote. Siku hizi, utengenezaji wa Website umerahisishwa sana. Wengi wanapendelea kutumia Content management System (CMS) kama Joomla, Woordpress au Drupal kutengenezea Website.

Uzuri wa kutumia CMS ni kuwa, kuna wachangiaji wengi ambao huangalia utendaji na uboreshaji wa kimfumo na kiutendaji. Hii hupelekea kuhitajika kwa update za mara kwa mara. Updates hizi huwa ni za kiusalama (Security fix), kiuboreshaji (Optimization) au kurekebisha tatizo (bug fix) linaloweza kupunguza utendaji wa Website. Hakikisha unajiunga na mlisho wa makala kutoka Joomla ili kupokea taarifa juu ya maboresho haswa yale ya kiusalama.

 Kwa kawaida hapa Dudumizi, tunawataka wateja wote wanaofanya Website Hosting, kuhakikisha Website zao zinatumia version mpya kabisa. Na pia, kama ni mmiliki wa website, hakikisha una mtaalamu wa IT ambaye atakusaidia kuifanyia maboresho ya mara kwa mara.

Video hii, itakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kufanya update kwenye Joomla Website, iwe ni ya Core Joomla au Extensions za Joomla.

APE Network, ni kampuni ya Kitanzania inayojihusisha na Uchapishaji wa vitabu pamoja na kazi mbalimbali zenye malengo ya kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Katika moja ya hatua zake, kampuni hiyo ilitengeneza Application ya simu kwa watumiaji wa Android. Application hii ilikuwa inawawezesha watumiaji kujifunza na kusoma kazi mbalimbali za kiswahili kama Misemo, methali, nahau na Vitendawili ambayo inajulikana kama Swahili Sayings (Misemo ya Kiswahili)

Application hii imepokea muitikio mzuri kutoka katika jamii ya watumiaji wa Kiswahili kwenye mtandao,  watumiaji wengi wamekuwa wakitoa maoni chanya juu ya kazi hii. Ingawa Application hii ilikua na vitu vingi vizuri, lakini pia ilikuwa inahitaji maboresho zaidi ili kuifanya iendane na mahitaji na mabadiliko ya tabio za watumiaji, haswa kimuonekano (User Interface), muingiliano na mtumiaji (user engagement) na machaguo ya mtumiaji (user selection) na pia kuongeza mvuto wa kwa mtumiaji ili aendelee kuitumia tena na tena.

Ili kuboresha hili, timu ya APE Network, iliitafuta Dudumizi Technologies LTD, ili kuangalia ni jinsi gani inaweza kuboresha Mobile Application yake na kuifanya iwe bora zaidi. Kama ilivyo kawaida yetu, tulitumia muda mwingi kuisoma na kuielewa, ili kuja na features zenye kutatua tatizo lililopo.

Timu ya Dudumizi kwa kushirikiana na Mkurugenz wa APE Network (mr Hermes Salla) tumeweza kukamilisha Application bora kabisa ya Kiswahili Duniani ambayo sasa inapatikana kwenye Playstore 

Features:

 • Kusoma Misemo, Methali, Nahau na Vitendawili
 • Kusikiliza Misemo, Nahau, Methali na Vitendawili kwa sauti
 • Uwezo wa kutuma maoni (comment) 
 • Uwezo kugawana (share) na wengiine
 • Uwezo wa kushiriki kwenye mijadala
 • Uwezo wa kuhifadhi taarifa uzipendazo
 • Uwezo wa kuona picha kulingana na aina ya taarifa

Tulichokifanya (what we have done)

 Muonekano wa App kwa picha

Muonekano wa mbele wa Application ya Swahili Sayings

Jinsi taarifa zinavyoonekana, sauti, picha na hata maoni

 

Unaweza kutuma maoni na ukafuailia ya wengine

Baadhi ya features kwenye menu ya Swahili sayings

Na mengine mengi yanapatikana kwenye Swahili sayings, Pakua App hii kutoka Playstore, pia kwa mahitaji ya App Development Tanzania, tuandikia kwa ajili ya kukutumia Free Quotation hapa

 

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe
Call us now