Mtumiaji wa website huwa anatumia dakika zisizozidi tano katika kutafuta kilichomplekea kwenye Website, hivyo ukiwa kama Website Designer unatakiwa kuhakikisha unatumia muda huo ipasavyo kuwafanya watembeleaji kuendelea kubakia kwenye Website yako. Siku hizi tumeshaachana na ule mtindo wa kuwa na mlundikano wa vitu kwenye kurasa za mbele za website, vinapokuwa vichache zaidi basi ndiyo ubora wake.

Katika kuhakikisha tunaongeza mvuto huku tukiwarahisishia wateja kupata picha na vitu vyote wavitakavyo kwenye kurasa moja, Dudumizi tumefanya maboresho ya kimuonekano na mfumo kwenye website yetui. Katika maboresho haya, mambo yafuatayo yameboreshwa;

 • Kutumiwa kwa Video badala ya picha, kwa ushurikiano na partners wetu, tumeweza kupata Video yenye kuendana na matakwa ya Dudumizi
 • Kutumiwa kwa icons badaya ya maneno ili kujenga mazoea kwa watumiaji
 • Matumizi  ya mitandao ya uhifadhi ili kuboresha speed
 • Muonekano wa kazi umeboreshwa na kuondoa kazi zilizopitwa na wakati
 • Muonekano wa kwenye simu nao umeboreshwa

Munonekano wa huduma za Dudumizi kwenye simu

 

Muonekano wa mbele wa Dudumizi

 

Siku za karibuni, Dudumizi tulipokea maombi kutoka kwa kampuni ya 4 Bell inayoandaa matembezi ya Bagamoyo Historical Marathon wakiwa na kusudio la kutengeneza Website kwa ajili ya tukio hilo la Marathon (Marathon Website Design), na moja ya matakwa yao ni kuwawezesha watumiaji kujisajili na kufanya malipo online haswaa kwa kutumia njia za simu kama mpesa na Tigopesa. Muda ulikuwa mfupi, huku kukiwa na hitaji la integration ya payment jambo ambalo linahitaji umakini na kutokukosea.

Kama ilivyo ada yetu, timu nzima ya Dudumizi ilihakikisha inafanya kazi kwa kutumia maarifa yote mpaka Website inakuwa hewani. Na mnamo, Julai 27, tulikamilisha kazi na sasa Website ip hewani kwenye link https://bagamoyomarathon.co.tz

Features:

 • Online Marathon registration
 • Pesapal Payment Integration
 • Registrants Management
 • Registrants Export
 • Marathon Gallery
 • News/Blog

What we did:

Katika kuhakikisha tunawashirikisha bloggers wa Tanzania kutumia website zao kutengeneza kipato, timu ya Dudumizi, inakuletea DuHosting Affiliate program, ni program ambayo inakuwezesha kuingiza kipato kwa kuweka banners za Dudumizi kwenye blog yako.

Unachotakiwa kufanya ni kujisajili halafu utaactivate Affiliate program na kuanza kuweka banners zinazoendana na blog yako, basi System zetu zitaweza kukutambua,na kama kuna mtu ananunua huduma yoyote kupitia blog yako, basi utaweza kupata kipato.  Hii pia inajumuisha hata kwa mitandao jamii.

Video ya jinsi ya kujiunga na Affiliate inavyofanya kazi.

Katika kuongeza hamasa ya matumizi ya domain names, haswa kikoa cha .tz, rasiji ya .tz (.tz domain registry), imeandaa wiki ya .tz. Wiki huu huazimishwa kwa semina pia kupata maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya jinsi gani ya kuhakikisha WaTanzania wanaifahamu na kutumia domain za .tz.

Mwaka huu, mawakala wa .tz ambao ni Dudumizi Technlogies LTD pamoja na Extreme Web Technology, wamechagualiwa kuwakilisha mawakala wengine katika kutoa mada juu ya .tz.

Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuliwa na washika dau mbalimbali wa .tz wakiwemo, wafanya biashara, taasisi binafsi na za uma, mawakala na wengine wengi. Maadhimisho hayo yamefunguliwa leo tarehe 12/6/2017 jijini dar es Salaam katika hoteli ya New Africa na yataendelea hadi siku ya ijumaa tarehe 15/6/2016 ambapo itakuwa ni kilele chake na kuzinduliwa kwa karibu poral. Kilele hicho kitakamilishwa kwa uzinduzi wa Website kwa ajili ya huduma za Domain na Hosting ambapo itazinduliwa na Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kasim majaliwa huku ikienda sambamba na majadiliano pamoja na mada zitakazofanyika katika ukumbi wa msekwa jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Dudumizi akiwa pamoja na Afisa Huduma kwa Wateja walihudhulia na kuiwakilisha vyema Dudumizi. Fuatilia kwenye picha.

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua mambo ya kuzingatia kwenye usalama wa tovuti

Wawakilihi wa Mawakala wa .tz walifuatilia maswali toka kwa washiriki

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi mendaji wa rajisi ya .tz

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua jambo mbele ya Mkurugenzi mendaji wa rajisi ya .tz

Mtaalamu wa masuala ya Domain na huduma kwa wateja kutoka Dudumizi, bi Lucy Vicent mbele ya bana ya Dudumizi

Mtaalamu wa masuala ya Domain na huduma kwa wateja kutoka Dudumizi, bi Lucy Vicent mbele ya bana ya Dudumizi

Washiriki wa siku ya .tz wakifuatilia mada kwa umakini

Washiriki wa siku ya .tz wakifuatilia mada kwa umakini

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua historia ya Domain na Website

Mkurugenzi wa Dudumizi akifafanua historia ya Domain na Website

 Mr Nyoni akifafanua umuhimu wa matumizi ya domain name za kikao cha .tz kwa afya ya uchumi

Mr Nyoni akifafanua umuhimu wa matumizi ya domain name za  kikao cha .tz kwa afya ya uchumi

 

 Makamilisho ya utoaji mada kutoka kwa kampuni ya Dudumizi

Katika siku za karibuni, tumefanya maboresho ya kimfumo na kimuonekano katika Website ya Dudumizi Hosting (DuHosting). Muonekano huu ni muhimu katika kuendana na falsafa ya ubunifu na pia, kuendelea kutoa support kwa matumizi ya kikoa cha .tz. Website yako ya Hosting sasa itapatikana kwa www.duhosting.co.tz badala ya dudumizi.net ingawa watembeleaji wa Dudumizi.net watapelekwa kwenye website mpya moja kwa moja.

Katika mabadiliko haya , pia, tumemleta kwenu Dugon, Dragon aliyebeba umbo na maana nzima ya DuHosting. Lengo kuu ni kuweza kutumia myama huyu kufikisha ujumbe ikiwemo spidi, usalama, uhakika, upendo nk.

Katika maboresho haya, sehemu zifuatazo zimeboreshwa

1. Muonekano wa kurasa ya kwanza umeboreshwa, haswa kwa watumiaji wa simu, sasa utaweza kuweka order moja kwa moja
2. Kuongezwa kwa jukwaa la support ambapo unaweza kuuliza swali na kujibiwa na watu wengine akaweza kufuatilia

Muonekano wa Website Design and Hosting Support

Muonekano wa jukwaa la Support kwa wateja


3. Kuboreshwa kwa kurasa za ndani, mfano kuongezwa kwa kurasa za historia ya DuHosting

History for Website Hosting Company in Tanzania


4. Maboresho ya muonekano wa order kutoka kurasa wa kwanza kabisa

Cheap Website Design and Hosting Tanzania
Plan za Website Hosting, Serengeti sasa ipo kurasa ya mbele

5. Maboresho mengine mengi ya kimfumo

Ni mategemeo yetu sasa utafurahia matumizi ya tovuti yako pendwa.

Search your Domain

 

Follow us on Facebook

 • Website Hosting

 • 80000Tsh

 • /Year
  • 1Gb Web Space
  • Unlimited Email Accounts
  • Free Website Builder
 • Subscribe
Call us now